Sunday, March 19, 2017

Erick Shigongo…Paul Makonda Hafai Kuwa Kiongozi Kwa Anachodaiwa Kufanya Clouds FM



From @ericshigongo – Wiki Chache zilizopita nilimsifia Paul Makonda hapa, lakini kwa anachodaiwa kukifanya Clouds usiku, nafuta sifa nilizompa! Hafai kuwa kiongozi. Kwa Mahali tulipo kama taifa hatuhitaji kiongozi wa aina hii hata kidogo.
Nampenda sana Rais John Pombe Magufuli, sipo tayari kuona rais wangu anatukanishwa na iasi hiki na matendo yanayofanywa na Mkuu wa Mkoa.
NITAMPINGA MAKONDA KILA ANAPOFANYA YASIYOSTAHILI NA NITAMTETEA RAIS WANGU ANAPOTUKANISHWA!
E.J Shigongo

MUUNGANO WA MADAKTARI,WAUGUZI KENYA (KMPDU) WAWAKATAA MADAKTARI WA TANZANIA


Umoja wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya ‘Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists’ Union’ (KMPDU) umepinga vikali hatua ya Serikali ya Kenya kuleta madaktari kutoka Tanzania wakati Kenya ina madaktari wengi ambao hawaajiriwa.

Taarifa Rasmi ya Clouds Media Kuhusu kuvamiwa na RC MAKONDA


TAARIFA KUTOKA ACT WAZALENDO

TAARIFA KWA UMMA
UTANGULIZI:

Ndugu waandishi wa Habari, kwanza nawashukuru kwa kuitikia wito wetu leo 
na kufika hapa ili kuchukua ujumbe tunaotaka kuutoa na kuuwasilisha kwa 
umma. Tuna mambo mahsusi matatu tunayopenda umma ufahamu. Nayo ni 
haya yafuatayo;-

Saturday, March 18, 2017

SHULE ZA TUSIIME ZAGUSWA NA INTER SCHOOL DEBATE COMPETATION,WANAFUNZI NAO WAJINYAKULIA ZAWADI MBALIMBALI.


Meneja Msaidizi wa Shule za Tusiime Bwana Laurent Gama akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi waliokuwa washindi katika mashindano ya Inter school Competetion Yaliyokutanisha shule nne za Jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kuwapambanisha wanafunzi wa shule hizo kutoa hoja na kutetea hoja zao .

Michuano ambayo inadhaminiwa na kituo cha Channel ten Pamoja na wadau wengine mbalimbali,Inter school Competetion imetajwa kama moja ya mashindao ambayo yana msaada mkubwa katika kuwajenga wanafunzi wa secondary kutumia Lugha na kupanga hoja zao jambo ambali litawasaidia baada ya kumaliza masomo yao.

Meneja Msaidizi wa Shule za Tusiime Bwana Laurent Gama akimkabishi kitita cha shilingi million Moja Mwanzilishi wa mashindano hayo ambaye pia ni mwakilishi wa kituo cha Chanel Ten Bwana Shukuru Ngongoje Ikiwa ni baada ya Shule za Tuusiime kutangaza kuunga mkono Juhudi za Kuwakutanisha wanafunzi mbalimbali wa Shule za Tanzania katika kupambana katika mashindano ya Debate.

Wanafunzi mbalimbali kutoka shyule nne za Dar es salaam zilizoshindanishwa leo zikiwemo,Feza,Jitegemee,Tusiime,pamoja na Kibasila Secondary ambapo washindi mbalimbali wamejinyakulia zawadi katika mashindano hayo
John Kishefu ambaye ni mwalimu mwandamizi wa Taaluma Tusiime akiwapa maneno wanafunzi ambao wamehudhuria katia mashindano hayo.
Meneja Msaidizi wa Shule za Tusiime Bwana Laurent Gama akizungumza.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu yatembelea kampuni ya simu za mkononi Tigo.

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwasili kwenye ofisi za Tigo Jijini Dar Es salaam leo

Mkurugenzi Mtendaji  wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiwakaribisha wajumbe wa kamati ya kudumu ya Miundo mbinu, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Tigo Kijitonyama leo.

Tigo, RITA kuanza awamu ya nne usajili wa watoto Geita, Shinyanga

Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Harrison Mwakyembe akionesha mojawapo ya simu 800 zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ili kufanikisha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, uzinduzi wa zoezi hilo kwa awamu ya tatu ulifanyika Septemba  mwaka jana mjini Iringa. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
Na Mwandishi wetu.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA)pamoja na UNICEF inategemea kuzindua awamu ya nne ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Geita na Shinyanga mapema wiki ijayo.

WANANCHI WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo, Kisare Matiku Makori kwa kuweka utaratibu wa kusikiliza kero zao kwa ajili ya kuzitafutia utatuzi.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti  jijini Dar es Salaam jana walisema utaratibu anaoufanya mkuu huyo wa wilaya unapaswa kuigwa na viongozi wengine kwani unakwenda na kasi ya kazi ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu.

LAPF WATOA REFLECTOR JACKET 500 KUSAIDIA BODA BODA WILAYANI KISARAWE MKOANI PWANI

 Muonekano wa jengo la mikutano la Halmashauri ya 
Wilaya ya Kisarawe.
 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (wa pili kulia), akimkabidhi moja ya jaketi angavu (Reflector Jacket) kati ya majaketi 500 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda katika hafla iliyofanyika wilayani humo jana. LAPF imetoa majaketi hayo kwa ajili ya kusaidia waendesha bodaboda ili waweze kutambulika wakiwa katika shughuli zao za kila siku.Kutoka kushoto ni Meneja wa Mfumo wa Uchangiaji wa Hiari wa LAPF, Hanim Babiker, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, William Gama na Meneja wa LAPF, Kanda ya Mashariki,  Lulyalya Sayi. 

JUKATA WAMKOMALIA RAIS MAGUFULI,WATAKA MCHAKATO WA KATIBA UREJESHWE HARAKA

 Jukwaa la Katiba Tanzania leo limemtaka Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa nafasi yake kulitangazia Taifa rasmi Tarehe rasmi ya kurejeshwa kwa mchakato wa kupata katiba mpya ikiwa ni pamoja na kuchapishwa kwa tangazo lake katika gazeti maalum la serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa JUKATA Bwana Deus Kibamba wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maamuzi ya mkutano mkuu  uliomalizika hivi karibuni uliokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja na wadau mbalimbali jinsi ya kurejesha mchakato wa katiba Tanzania ambao unaoinekana kukwama,
Kibamba amesema pamoja na maazimio mbalimbali yaliyamuliwa na wadau wa mkutano huo umeona kuwa Rais wa Tanzania kwa nafasi yake ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kurejesha mchakato wa katiba nchini ili watanzania waendelee na mchakato huo baaada ya kusimamishwa kupisha uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka Juzi nchini.


Kibamba amesema kuwa Rais pamoja na waziri husika wanawajibu wa kufufua mchakato wa katiba kwa sasa kwani umetumia fedha nyingi za watanzania na mchakato huo haujakamilika.

Aidha kibamba amesema kuwa mkutano huo kwa kauli moja uliamua kuchagua wajumbe mbalimbali wanaohusika na maswala ya katiba kufanya mchakato wa kukutana na Rais wa Tanzania kuhakikisha kuwa wanamshawishi na kumpa maoni yao kuhusu jinsi ya kufufua mchakato huo kwani ni ukweli kuwa watanzania sasa wanahitaji katiba mpya ambapo pia Jukata wametangaa kusaidiana na serikali katika mchakato huo wa katiba ikiwa ni pamoja na kuhamasisha watanzania kuwa na hari tena ya kujitafutia katiba mpya.

Friday, March 17, 2017

TFF: Azam FC itasonga mbele CAF

MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, aliyeambatana na Azam FC kuelekea mchezo wake wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows, amesema wanauhakika mkubwa wa timu hiyo kusonga mbele kwa raundi ijayo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Karia ameambatana na kigogo mwingine wa TFF ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo, James Muhagama, wote kwa pamoja wakiwa na imani kubwa na timu hiyo ambayo iliondoka na ushindi wa bao 1-0 nyumbani.

Balozi aipa tano Azam FC, atoa mkono wa ushindi vs Mbabane

BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mh. Richard Lupembe, ameweka wazi kuwa Azam FC ni moja ya timu zinazowatia moyo kama Watanzania wanoishi nje ya nchi, huku akiipa mkono wa ushindi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows ya Afrika Kusini.

Thursday, March 16, 2017

SIKU MOJA KABLA YA UCHAGUZI TLS,TUNDU LISSU AKAMATWA

Mbunge na Mwanasheria wa chama cha Democrasia na maendeleo Chadema Tundu Lissu amekamatwa na polisi asubuhi ya leo na kusafirishwa kutoka Dodoma kuja Dar es salaam kwa kile ambacho Kinatajwa kuwa alipitisha muda wa Kufika mahakamani,.Soma Ujumbe wake Kabla hajakatwa hapa

*Anaandika Tundu Lissu*
Wandugu wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma. Najiandaa kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS. Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC Dodoma.
 Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS. Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi. Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania. Nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia. 

Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii. Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani mwingine aliye salama??? Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama??? Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii. Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu. Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu. 

Hiki ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza hili nene. Msikubali kuyumbishwa. Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu. Nawatakieni kila la kheri. I'll think of you all wherever they'll take me to, wherever I'll be incarcerated. 

This too shall pass. The race of man shall rise again. It always has. Nimemwambia na mke wangu naye aende Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences. All the best. TL