Monday, October 2, 2017

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA: PSPF YAFUNGUA OFISI MPYA PEMBA NA UKEREWE



MFUKO wa Pensheni wa PSPF,  umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
“Mtakumbuka kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka,  huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”
Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”
Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,
hapa makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.
Aliwataja washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu, (MCB).
Alisema, PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.
Miongoni mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na maafisa wa PSPF.
“Kwa kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa uchapakazi wa namna hii.” Alisema.


Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.


Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.

 Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa na Bi.Elizabeth Shayo, (kulia), makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.


 Elizabeth Shayo, (katikati), Afisa Huduma kwa wateja wa PSPF, akitoa maelezo kwa Mwanachama aliyefika kupatiwa huduma.

Afisa wa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. January Iman Buretta, (kushoto), akizungumza na wanachama wa Mfuko huo waliofika makao makuu kupatiwa huduma Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza jana, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.

 Ntimi Mwakajila, Afisa wa Huduma kwa njia ya simu, (Call Centre), Mfuko wa PSPF, akiwa kazini
 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Fatma
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, (mbele), Meneja Masoko, Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Fatma Elhady, (wapili kulia), na maafisa wa kitengo cha huduma kwa njia ya simu wakiwahudumia wateja wa Mfuko kwenye kituo hicho.

 Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, akizungumza na mmoja wa wateja waliofika kupatiwa huduma
  Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi, (kulia), akipokea nyaraka kutoka kwa  Meneja wa Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi.
 Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi, (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja wa Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laima Maghimbi.


MFUMO WA ‘DROPWALL’ KUSAIDIA TAKWIMU MASHULENI

Meneja Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua akiongea mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam wakati wakimtambulisha mfumo mpya wa kieletroniki wa ‘Dopwall’. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Eagle Analytics, Rose Funja ambao ni wasimamizi wa mfumo huo.
Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Eagle Analytics, Rose Funja ambao ni wasimamizi wa mfumo huo akifafanua machache mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam jinsi mfumo huo unavyofanyakazi. Pembeni ni Meneja Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua. Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam. MFUMO mpya wa kieletroniki wa ‘Dopwall’ umezinduliwa nchini na unatajwa kuwa utasaidia kupunguza mdondoko wa elimu kwa wananchi wa kike nchini. Licha ya hali hiyo pia inatajwa kuwa mdondoko wa wanafunzi kwa shule bado ni tatizo nchini ambapo kwa kipindi cha mwaka 2015 wanafunzi 61,488 waliripotiwa kuacha masomo. Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Eagle Analytics, Rose Funja, alisema kuzinduliwa kwa mfumo huo kusaidia wazazi na walezi kujua hali ya maendeleo ya shule wanasoma watoto wao ikiwemo kuwa na uwezo wa kuhoji kupitia vikao vya wazazi na bodi za shule. “Serikali kupitia wizara mbalimbali ikiwemo Serikali za Mitaa wameboresha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za kielimu ambazo ni msingi wa mapambano dhidi ya mdondoko wa wanafunzi. Pamoja na jitihada hizo matumizi ya taarifa kama hizo katika kuboresha utendaji wa kila siku wa watumishi wa umma na ufanyaji wa maamuzi hayatoshelezi au hakuna kabisa katika idara za serikali,” alisema Funja Kwa upande wake Meneja Ufuatiliaji na Tathimini mradi wa Data kwa Maendeleo ya Jamii wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Geofrey Chambua, alisema mfumo wa kieletroniki wa ‘Dropwall’ unalenga kuongeza matumizi ya taarifa zinazokusanywa na wadau mbalimbali ikiwemo serikali. “Ubunifu wa mfumo huu umedhaminiwa na mradi wa Data fot Local Impact (DLI) ikiwa ni moja kati ya miradi mitatu ya takwimu inayosimamiwa na MCC pamoja na PEPFAR. Udhamini wa dli uliwesha uchunguzi wa mdondoko mashuleni katika wilaya za Mbeya na Nzega chini ya mwongozo wa TAMISEMI. “Kampuni ya Eagle Analytics inayotengeneza mfumo wa Dropwall ni kampuni changa. Mhandisi Rose na timu yake kupitia ubunifu wao wa kubaini uwezekano wa mwanafunzi kuacha masomoni mmoja wa washindi 12 wa shindano la ubunifu lililoratibiwa na DLI ikishirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) mwaka 2016,” alisema Dk. Chambua.

Idris Sultan ‘aula’ filamu yenye bajeti ya shilingi bilioni 38

  •   Itashutiwa katika miji ya Berlin, London, Paris, Cape Town na Acapulco, Mexico

Mastaa wakubwa duniani kama Eric Dane wa Lastship ,Gerard Depardieu wa Life of Pie,  Thomas Kretschmann wa Avengers Pearl Thusi  wa  Quantico…kushiriki




NYOTA ya aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Mtanzania Idris Sultan, inaendelea kung’ara  baada ya ‘kupata shavu’ la kushiriki filamu yenye bajeti ya dola za Kimarekani milioni 17 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 38.


Idris pamoja na Mtanzania mwingine Ernest Napoleon, wataungana na mastaa wakubwa  duniani kama Eric Dame, mwigizaji Mmarekani, Gerard Depardieu wa Ufaransa, Thomas Kretschmann wa Ujerumani na wengine wengi kucheza filamu hiyo ya ujambazi wa kimataifa.

Filamu hiyo itakayojulikana kwa jina la ‘The Blue Mauritius’, inahusu majambazi watano wa kimataifa ambao wanasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika ya Kusini, kwa ajili ya kuiba vitu mbali mbali vyenye thamani kubwa duniani.

Idris na mwenzake Ernest Napoleon, watasafiri kwenda katika jiji la Cape Town nchini Afrika kusini mapema mwakani kwa ajili ya filamu hii  kubwa kuwahi kuwahusisha Watanzania.



“D Street inayo furaha kubwa kugeukia vipaji vya waigizaji wa Kiafrika kwa kuwaunganisha na waigizaji wa kimataifa kama itakavyokuwa kwa ‘The Blue Mauritius’,” anasema Dexter Davis, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya D Street Media Group ya Marekani, inayoanda filamu hiyo

Kwa mujibu wa Davis, filamu hiyo itasambazwa siyo tu Marekani, bali pia katika majumba makubwa ya sinema dunia nzima.

“Ernest na Idris watang’ara, tunasubiri kwa hamu kuwaona tena kwenye skrini kubwa wakifanya makubwa,” anasema Davis
Mapema mwaka huu, wawili hao walicheza filamu iliyojulikana kama ‘Kiumeni’ ambayo pia Ernest alikuwa ni mzalishaji na kushirikiana na Daniel Manege kuiandika. Filamu hiyo ilishinda katika Tamasha la Timataifa la Filamu la Zanzibar ambalo Idris na washiriki wenzake walihudhuria
 “Ninayo furaha kubwa kufanya kazi na Idris katika filamu kubwa kama hii ya The Blue Mauritius. Ni mwaka wa pekee kwa mimi kufanikiwa kufanya kazi na D Street. D Street inabadilisha upepo kwa Afrika inapokuja kwenye suala la kutengeneza filamu,” anasema Ernest 
Kwa upande wake Idris anasema, “Nilikutana Dexter Davis kwenye Maonyesho ya Filamu ya Kimataifa ya Zanzibar mwezi Julai na nilifurahishwa na namna ambavyo amevutiwa na vipaji kutoka Afrika. Alivutiwa kufanya kazi na mimi baada ya kuona ushiriki wangu katika filamu ya ‘Ballin; On the Other side of the World’ na miezi miwili baadaye nilishiriki Katina filamu moja ya Kimarekani. Filamu hizi mbili zimenifanya niweze kufanya kazi nchini Marekani jambo ambalo nilitamani sana,” 
Filamu hiyo inatarajia kuanza kuzalishwa mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka ujao (2018). 

Sunday, October 1, 2017

Tigo donated 1000 Mobile Smartphones for Mobile Birth registration for Lindi and Mtwara Regions

A RITA official explains to dignitaries including the Minister for Information, Arts, Culture and Sports Hon Dr. Harrison Mwakyembe, the Lindi Regional Commissioner Geodfrey Zambi, Tigo MD Simon Karikari and others  how the mobile birth registration works. This was during the launch of the Mobile Birth registration exercise for Lindi and Mtwara regions that happened in Tandahimba district in which Tigo donated 1,000 smartphones to ease the exercise.


Tandahimba residents line up to register their chidren.
Tigo MD Simon Karikari greets the audience
Tigo MD Simon Karikari addresses guests at the launch of the Mobile Birth Registration exercise for Lindi and Mtwara regions in Tandahimba district
Minister for Information, Arts, Culture and Sports Hon Dr. Harrison Mwakwyembe hands over a birth certificate to a resident of Tandahimba District during the launch of the mobile birth registration exercise for Lindi and Mtwara region. Looking on is the Tigo MD Simon Karikari (c) and other officials. Tigo donated 1,000 smartphones in  support of the child registration and certification  exercise.





Children perfom for guests during the launch of mobile birth registration exercise in Tandahimba.




Lindi Regional Commissioner Geodfrey Zambi, Minister for Information, Culture and Sports Dr Harrison Mwakyembe and RITA Advisory Board Chairperson Hamisi Dihenga show off one of the phones donated by Tigo.














Minister for Information, Culture and Sports Dr Harrison Mwakyembe hands over a phone donated by Tigo to Lindi Regional Commissioner Geodfrey Zambi. Left is RITA Advisory Board Chairperson Hamisi Dihenga.

TAMASHA LA TIGO FIESTA LAFANA MKOANI TABORA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza kuhusu usalama wa watu na mali zao ulivyoimalishwa  kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora wakati wa tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana.




Benpol akiwapagawisha wakazi wa Mkoa wa Tabora katika Tamasha la Tigo Fiesta katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora



Msanii wa bongo fleva Mr Blue akitumbuiza kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora wakati wa tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jana.

Chege akitumbuiza kaaika jukwaa la Tigo Fiesta

Darasa akitumbuiza kaaika jukwad la Tigo fiesta mapema usiku wa kuamkia leo mkoani  Tabora.

Omg Dimpoz akiburudisha wakaz wa Tabora waliojitokeza kwa wingi katika viwanja via 

Jux akitummbuiza wakazi wa Tabora.

Jux katika jukwaa la Tigo Fiesta  katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora 

Maua Sama akiimba kwa hisia 




Maelfu ya wakazi wa Tabora wakiwa katika Tamasha la Tigo Fiesta mapema usiku wa kuamkia jana.

TANZANIA HAINA BUDI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGTALI KUJITANGAZA KIMATAIFA

Na Jumia Travel

Wakati dunia ikisherehekea siku ya Utalii Duniani, Jumia Travel imebainisha kwamba matumizi ya tekinolojia za kisasa hususani mtandao wa intaneti una manufaa makubwa katika kuvitangaza vivutio vya kitalii kimataifa.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea nchini Tanzania, Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Umma wa Jumia Travel Kimataifa, Bw. Abdesslam Benzitouni ameweka wazi kwamba Tanzania haina budi kutumia ipasavyo njia zote za kidigitali ikiwemo mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Youtube na Instagram kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watumiaji.

MAHAKAMA YAAMURU MSHITAKIWA HARBINDER SETHI AKATIBIWE HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI NDANI YA SIKU 14

Harbinder Sethi

Na Dotto Mwaibale

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kwa mara nyingine mshtakiwa Harbinder Sethi akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ndani ya siku 14.

Korti imesema iwapo hilo halitatekelezwa, mkuu wa gereza afike mahakamani kujieleza. Sethi yupo mahabusu katika Gereza la Segerea.

DC HAPI ATOA MAAMUZI HAYA KWA MUWEKEZAJI WA KITUO CHA MAKUMBUSHO

Mkuu wa wilaya ya kinondoni mh. Ally Hapi  jana amefanya ziara ya kutembelea soko la makumbusho na kuongea na wafanya biashara pamoja na wakazi wa maeneo ya karibu ili kufahamu changamoto zilizopo katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi akitoa ufafanuzi wa jambo furani  katika ziara yake iliyofanyika jana katika soko la  Makumbusho jijini Dar es salaam.

Katika mkutano huo wafanya biashara na wakazi wa kata ya makumbusho walipata nafasi ya kutoa kero zao na kuhoji mambo mbalimbali yakimaendeleo katika soko hilo na kupatiwa majibu ya papo kwa hapo na jopo alilokuja nalo mkuu wa wilaya huyo.

Mh. Hapi ametoa agizo kwa meneja msimamizi wa mradi wa makumbusho ambae amemuwakilisha muwekezaji kupeleka nyaraka zote za malipo waliyofanya katika ulipaji wa kodi, na pia wamepewa muda wa mwezi mmoja tu kulipa deni lote wanalodaiwa na manispaa ambalo ni zaidi ya million 70.
 Meneja Msimamizi Mradi wa Makumbusho (Muwekezaji) Bw. Haidary Salumu akitoa ufafanuzi juu ya mashitaka yanayomkabili kuhusu kuwanyanyasa wafanya biashara wadogo wa eneo hilo
Lakini pia mkuu wa wilaya huyo ametoa agizo kwa jeshi la polisi kuweza kuwakamata watuhumiwa  wanne ambao ni Shabani, Bonzo, Deo na Scorpion kwa makosa ya kuwaonea wafanya biashara wadogo wanauza maji, pipi karanga, sigara katika kituo hicho kwa kuchukua bidhaa zao na kuwataka watoe hela ndipo wapewe bidhaa  zao.

Aidha mh. Hapi aliendelea kusisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajiri ya kuwakomboa wanyonge hivyo haitakaa kimya kuona wananchi wake wanaonewa, hivyo kutoa agizo kwa polisi kumkamata mtu anayeitwa Morel mkazi wa mbezi juu ambaye anasifika kwa kudhurumu watu ardhi na wananchi kukosa kwa kushitaki kwa kuwa ni mtu mwenye fedha.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni Bw. Abubakari Kunga akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya elimu ya uraia na haki za wananchi. 
Na lingine aliloagiza mkuu wa wilaya ni kusitishwa mara moja zoezi la ukusanyaji fedha kwa pikipiki na boda boda ambalo lilikuwa likitekelezwa na muwekezaji huyo ambalo limeonekana likiwaumiza wananchi hao kwa kutozwa fedha nyingi kinyume na mkataba waliyokubaliana na manispaa ambao ndio waliowapa kibali hicho. Na kutoa agizo ifikapo jumaa tatu apeleke nyaraka zote zinazoonyesha makusanyo waliyokusanya toka mwanzo mpaka sasa na kutakiwa kuzilipa fedha hizo zote.

Lakini pia muwekezaji huyo kuambiwa aache mara moja zoezi lake la kuweka walinzi katika eneo hilo ambao wamekuwa wakiwaonea wafanya biashra wadogo na kusababisha ugomvi na wizi katika eneo hilo kwani wakina shabani wakiwachukulia vitu wanaenda kuviweka ofisini kwake, na kusisitiza kazi ya ulinzi na usalama ni ya serikali na siyo ya muwekezaji.
Na mwisho OCD wa kinondoni amepewa kazi na mkuu wa wilaya huyo ya kuhakikisha polisi waliyotumika kuwakamata wafanyabiashara wadogo kwa kisingizio cha uzululaji na kuwapeleka kituoni na kuwachaji fedha wachukuliwe hatua mara moja ya kufikishwa mahakamani kusomewa mashitaka.


Kumbilamoto: Ugonjwa wa Kipindupindu umepungua Vingunguti

Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni mlezi wa Kata ya Vingunguti katika masuala ya usafi Msongo Songolo amewataka wananchi wa kata hiyo mtaa wa Miembeni kuendelea kuyatunza mazingira kwa kufanya usafi kwani kufanya hivyo kuna faida kubwa ikiwemo kupunguza gharama za matibabu.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam katika Jumamosi ya usafi ya mwisho wa mwezi ameeleza kuwa suala la usafi hupelekea kuepuka gharama za matibabu kwa magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu, pia ili taifa liwe na watu wenye afya lazima watu wawe wasafi.

" Wananchi wanao wajibu wakufanya usafi kama wakiendelea kuwa wachafu shughuli za kiuchumi zitashindwa kufanyika"
Kwa upande wake Diwani Mwenyeji wa Kata ya Vingunguti ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amepongeza wananchi kushiriki katika suala la usafi na kueleza kuwa Vingunguti ya zamani siyo ya sasa kwani hata maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu yamepungua huku ripoti zikieleza ni watu wawili tu ndiyo wameripotiwa kuugua wakati hna mahema ya wagonjwa yameondolewa Vingunguti.

Naibu Meya Kumbilamoto ameongeza kuwa wataendelea kumualika mlezi wao katika kila mtaa ili kuhamasisha suala la usafi kwa kila mwana Vingunguti.

" Leo tumeanza na Mtaa wa Miembeni kwa kumualika mlezi wetu, tutaendelea kufanya hivyo kwa mitaa mingine ili kuhakikisha tunakuwa na Vingunguti safi" Alisema Kumbilamoto

ANGALIA HAPA KUJUA KILICHOJIRI KATIKA MATEMBEZI YA AMANI YA KUMUENZI MJUKUU WA MTUME IMAM HUSSEIN

Dhehebu la Shia Ithnasheria nchini leo limefanya matembezi ya amani yaliyoanzia kituo cha mabasi Ilala Boma na kuelekea mpaka msikiti Al Ghadiir uliopo Kigogo jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kuenzi na kukumbuka mchango wa  Imam Hussein.
Akiyazungumzia matembezi hayo kiongozi mkuu wa Shia Ithnasheria Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa ni matembezi yenye faida kwa waislamu na wasiokuwa waislamu kwa kumuenzi mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume Mohamad ambaye alifariki kwa kuwatetea wanadamu bila kuangalia itikadi zao za kidini, kikabila rangi, madhehebu nk.


Aliendelea kwa kusema kuwa ni kitendo cha ajabu sana kwa mtu kujitolea maisha yake kwa ajiri ya watu wengine, na kwa Imam Hussein alikufa akiwa yeye na familia yake na wengine ni watoto wadogo walio chini ya umri wa miezi sita wote waliuwawa na hii ni katika kukomboa dunia ya leo ambayo imebujikwa na mambo mengi yasiyo mazuri kama ugaidi, wizi, magomvi yasiyo na tija kwao.

Aidha Sheikh Jalala alisisitiza kuwa kitendo kilichofanywa na Imam Hussein 
kinatufundisha wanadamu wa leo kujenge tabia ya kupendana, kuhurumiana, kusaidiana pamoja na kuheshimiana bila kuangalia itikadi zetu za kidini, kisiasa, kikabila nk. Kwani Imam Hussein alifanya ukombozi huo ili tusibaguane ila tuwe na umoja kati yetu sisi na majirani zetu hata na marafiki zetu na watu wote tunaoishi katika jamii moja.
Hivyo kupitia matembezi haya watanzania watajifunza mengi kwani hii sio kwa waislam tu bali watu wadini zote walipewa nafasi ya kujifunza mengi toka kwa Imam huyo ambaye aliishi katika kipindi kibaya ambapo hakukuwa na upendo, amani ilitoweka lakini yeye alisimama na kupingana na hali hiyo na siyo kwa faida yake tu bali ni kwa dunia nzima iweze kuwa huru na watu waishi vizuri kama mapenzi ya mungu yanavyotuamauru tufanye.

Na mwisho alipenda kuwasisitiza Watanzania kuendelea kulinda Amani tuliyo nayo, Umoja wetu pamoja na mshikamano na tusikubali kuvipoteza hivi vitu kwani ni nuru yetu tuliyopewa na mungu, kwani watanzania ni watu tusiojua kubaguana kikabila, kidini, kimaumbile hata kwa vipato vyetu bali tunaunganishwa na nguzo zetu kuu ambazo ni Amani, Umoja na mshikamano wetu.