Monday, November 24, 2014

HII NI ZAIDI YA BURUDANI YA TAMASHA LA TIGO WELCOME PACK WILAYANI KAHAMA MWISHONI MWA WIKI

Msanii wa vichekesho Masanja akitumbuiza kwenye uwanja wa Taifa Wilayani Kahama,wakati wa tamasha la Tigo Welcome Pack




Msanii wa vichekesho Lucas Mhavile a.k.a Joti akitumbuiza kwenye uwanja wa Taifa Wilayani Kahama,wakati wa tamasha la Tigo Welcome Pack.

ANNA MAKINDA AANZA KAZI,TIZAMA MALUMBANO YA LEO HAPA,


MHE  MAKINDA 

Mbatia: Naomba kuwasilisha hoja, ofisi yako ilipokea ripoti maalamu kuhusu Escrow na umiliki. Taarifa hii ilikua siri mpaka itakapowasilishwa bungeni na turiarifiwa taarifa ya PAC haijakamilika na tumepata taarifa ripoti hiyo inagawiwa kama njugu na baada ya kutoa taarifa polisi wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja na inavyoonekana taarifa hio imeibiwa na ina muhuri wa katibu mkuu na kwa mujibu wa maelezo taarifa hio imeibwa. Katiba ya jamhuri 1977 linaainisha bunge lina mamlaka ya kusimamia fedha za umma, kitendo cha kusambazwa mitaani wakati bado haijatolewa rasmi inadhiirisha kuna watu wamejipanga kushusha heshima ya bunge. Kwa kua kumekua na jitihada nyingi zinazolenga kuzuia bunge kushindwa kufanya kazi yake, kwa kutumia kanuni ya 51 naomba kutoa hoja bunge lisitishe shughuli zake za sasa na kujadili ripoti hio

Makinda: Hamna hoja hapo na kaeni msome kifungu cha 51, ofisi ya bunge imeshirikiana na polisi ili muhusika asitoke mpaka aeleze mAshine gani zimetumika naikithibitika amefanya atapata kifungo cha miaka mitatu. Tukipata taarifa ya polisi tutachukua hatua na hamna ubabe hapa ninaoufanya.
Order paper imebadilishwa hivyo litajadiliwa humu ndani, nchi inaendeshwa kwa taratibu na kazi inaendelea hivyo hatuwezi kujadili kitu ambacho hakijaishwa.

MIONGOZO MINGI SANA

Mnyaa: Jambo aliloliomba mbatia na mjadala huu ni mpana na halihusiani tu na kusambazwa nyaraka na wengi wameshachafuliwa ikiwemo na wewe kuchukua dola 1,000,000/=, kwa heshima tunaomba uruhusu mjadala huu angalau kwa nusu saa.

Tundu Lissu: Mheshimiwa spika, nashukuru kwa fursa na kwa kuwa ni suala la kikanuni, ni vizuri turidhike kama hOja ya Mbatia ina haja kujadiliwa ama laa. Kanuni ya 51: Umeridhika na hili suala na ndio maana umempa nafasi Mbatia, tunajadili yanayotokea na vizuri jambo lizungumzwe ili hii hali isafishwe.

Makinda: Naheshimu profession yako lakini pia na wewe uheshimu taratibu, polisi wanaendelea na wakimaliza spika atapanga.

Ole Sendeka: Kamati itawasilisha lakini jambo hili jambo hili linahitaji kutendewa haki, nna mashaka, bunge litapata muda gani kusoma ripoti. Ripoti ipatikane kwa wabunge rasmi ili siku ya kuwakilisha tuweze kujadili

Makinda: Tunafanya utaratibu mpate ripoti mapema

UMESKIA HII--WANA CCM 350 WAJIUNGA CHADEMA

Wananchi wapatao 350 waliokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida wakiwa wameshika kadi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku wakila kiapo cha uzalendo baada ya kujiunga na chama hicho kwenye moja ya mikutano ya 'Operesheni Delete CCM' uliohutubiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, mwishoni mwa wiki.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu akiwalisha kiapo cha uzalendo wanachama wapya katika Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida waliohama kutoka Chama Cha Mapinduzi, katika moja ya mikutano 'Operesheni Delete CCM', uliofanyika mwishoni mwa juma kijijini hapo
 TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA AFISA HABARI WA CHADEMA TUMAIN MAKENE

KATAA UNENE FAMILY WAADHIMISHA MWAKA MMOJA

Kundi linalojulikana kwa jina la Kataa Unene Family (KUF) linaloongozwa na mwanadada Angel Msangi limeadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake na kujiwekea malengo ya kusaidia idadi kubwa zaidi ya wenye uhitaji wa afya bora kwa kula kwa afya na mazoez
Kundi hilo lenye wanachama 30 limeadhimisha mwaka kwa kufanya mazoezi ya pamoja ikiwa ni pamoja na Aerobics, Kuogelea na Kucheza dansi katika Gym ya Rio iliyopo jijini Dar es Salaam na baadae kupata chakula cha pamoja cha usiku

Akizungumza katika sherehe hiyo ya maadhimisho ya mwaka mmoja, kiongozi wa kundi hilo Angel Msangi amesema anafarijika kuona watu wanapungua na kuwa na miili na ngozi nzuri kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu na kuwa na nia kutoka moyon

Sunday, November 23, 2014

PICHA YA ESCROW IMENOGA--KUTOKA CUF MUDA HUU SOMA WALICHOTANGAZA

Mwenyekiti wa cuf IBRAHIMULIPUMBA akiwasili makao makuu ya chama kukutana na wanahabari mapema leo
Chama  cha wananchi CUF leo muda huu kimewataka waziri mkuu wa Tanzania mh MIZENGO PINDA,mwanasheria mkuu wa Tanzania jaji Fredrick werema,waziri wa nishati na madini profesa SOSPETER MUHONGO,pamoja na katibu mkuu wa wizara ya  nishati na madini bwana ELIAKIM MASWI kuachia ngazi mara moja au kufukuzwa kazi kutokana na wao kuonekana wazi kuwa wanautetea ufisadi wa mabilioni ya escrow unaoendelea nchini.


         Akizungumza na wanaandishi wa habari mapema leo makao makuu ya chama hicho mwenyekiti wa CUF profesa IBRAHUIM LIPUMBA amesema kuwa viongozi hao wamekuwa mstari wa mbele kuonyesha wazi kuwa hawako tayari kuona wahusika wa ufisadi huo wakiadhibiwa hivyo hawana sifa ya kuendelea kuiongoza nchi kwani hawana maslahi kwa wanachi huku akiitaka TAKUKURUI nao kuwachunguza viongozi hao kama wanahusika na ufisadi huo.
Hapa akizungumza na wanahabari
“hivi karibuni tulimsikia waziri mkuu akiwadnaganya watnzania kuwa fedha zilizopo kwenye account ya tegeta ESCROW sio mali ya umma bali ni mali ya kampuni binafsi kauli ambayoni ya uongo na yakujaribu kuficha maudu hayo”amesema lipumba

       Aidha CUF wameitaka TAKUKURU kuwakamata mara moja vigogo JAMES RUGEMALIRA ambaye mtandao huu pia umesharipoti kuhusika kwake pamoja na HARBINDER SINGH SETH na kuwafungulia mashtaka ya rushwa mna wizi wa mali ya tanesco kwani hawa ndio wahusika namba moja wa kuzigawa pesa hizo kama zao.

           Aidha lipumba ametaka pia mkuruygenzi wa tanesco pamoja na bodi nzima ya tanesco kufutwa mara moja kwa kuwa haikutimiza wajibu wake wa kulinda maslahi ya shirika wanaloliongoza.

         Katika hatua nyingine chama hicho kmesema kitafanya maandamano ya nchi nzima baada tu a mjadala huo kumalizika bungeni kuwashinikia viongozi waliohusika kuwajibika na pia kuwapongeza wabunge waliosimamia kuonyeshwa kwa ufisadi huo.


Saturday, November 22, 2014

MOVIE YA ESCROW YAFIKIA PATAMU,KIKAO CHA SIRI DODOMA CHAVUJA,SOMA HAPA

      Imeandika na Josephine B Mramba

Dondoo Kutoka Kikao cha Ndani ya Baraza la Mawaziri kilichofanyika jana Dodoma kilichofanyika Ofisi za TAMISEMI.
Kikao rasmi cha kujadili sakata la IPTL/ESCROW namna wahusika watakavyowajibishwa au kuokolewa.
1.Misimamo ya Mawaziri tofauti tofauti.

MADUDU MENGINE HAYA HAPA--MWAKYEMBE SASA KITANZINI AHUSISHWA NA UFISADI HUU,SOMA HAPA



*Wajiandaa kuuza haki za kuiendesha kwa bei ya kutupa
*Wathamanisha ardhi, maji Sh milioni 246 kwa miaka 33
*Thamani halisi ni Sh bilioni 85, ni mkataba hatari kwa usalama
*Mwekezaji anapewa ‘bure’, TPA kukopa mtaji Sh bilioni 306
*Dk. Mwakyembe ahusishwa, Kigogo adaiwa kuhongwa bilioni 1

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeingia katika kashfa nyingine nzito kutokana na mpango wake wa siri inaoukamilisha wa kubinafsisha mlango wa Bandari ya Dar es Salaam katika eneo liitwalo Gerezani Creek kwa miaka 33 kuanzia mwaka huu.

Mpango huo unaosukwa kwa siri kubwa chini ya mkataba unaopendekezwa; imebainika kuwa kisheria ni mbovu, hauna maslahi kwa taifa na unahatarisha usalama wa Tanzania.

Mkataba huo ulipaswa kutiwa saini Septemba 6, mwaka huu, lakini inaelezwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TPA, ameukataa.

lilipowasiliana na Simbakalia, alisema: "Ahaaaa, ahaaaa ahaaa, bwana, hayo mambo ya Bandari sitaki kuyazungumzia, ongea na Mwenyekiti au Kaimu Mkurugenzi wa Bandari. Sitaki swali zaidi." Akakata simu.

PICHA---HII NDIO HARUSI YA MBUNGE DAVID KAFULILA HUKO KIGOMA

 

Kwenye historia ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kuna historia nyingine inaandikwa ambapo Mbunge mwingine amefunga Ndoa.
Tumezoea Wabunge wetu wakipewa nafasi ya kuchangia jambo ndani ya kikao cha Bunge huwa wanaanza kwa pongezi, utasikia hivi; “.. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge au Waziri………
Jumatatu kikao cha Bunge kitaendelea na nadhani hautoshtuka ikitokea Mbunge hata mmoja akisema hivi; “… Nimpongeze sana Mheshimiwa David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini kwa kufunga ndoa siku ya Jumamosi..”

Yes.. Ni kweli.. Mbunge huyo amefunga ndoa leo Kigoma, ujumbe alioandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook ni huu hapa; “..Bwana Harusi David Kafulila akiwa na msimamizi wa ndoa yake Deo Filikunjombe na marafiki zake David Silinde na Mwami..” halafu kuna picha aliyoiweka akiwa na Wabunge hao.
Endelea kufuatilia HABARI24 BLOG kwa taarifa zaidi mtu wangu.
Zitto 

RAIS KIKWETE AZIDI KUIMARIKA KIAFYA


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns
Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika
mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete
anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa
maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais
Profesa Mohamed Janabi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume wiki iliyopita.Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Picha na Freddy Maro.

Friday, November 21, 2014

TANGAZO MUHIMU TOKA TFF USIKU HUU


 




Watoto wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika kesho Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa ajili ya kusaka kombaini ya mkoa.

         Mkusanyiko wa kusaka kombaini hiyo kwa ajili ya timu itakayoshiriki mashindano ya Taifa yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao uko chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

Wachezaji hao wataanza kujaribiwa saa 1 hadi saa 5 asubuhi. Mashindano ya Taifa yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu.


REGNALD MENGI ATOA NENO LEO,LISOME HAPA


BW;REGINALD  MENGI



VIONGOZI MLIOCHAGULIWA...Wananchi waliwamini wakawapa kura zao. Leo baadhi yenu mnawasaliti waliowachagua kwa kutetea wezi wa fedha za umma

Acha Mungu aitwe Mungu. Amewaweka hadharani wasiofaa kupata kura yeyote 2015 kwa kutetea wezi wa fedha za umma

MAMIA WAMUAGA MWANDISHI WA HABARI WA NEW HABARI 2006 LTD, MAREHEMU INOCENT MUNYUKU


Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.

WALICHOKIFANYA KINANA NA NAPE HUKO LIWALE LINDI HIKI HAPA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.


 Wananchi wa Liwale wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia kuwa wapinzani kwenye mikoa hiyo hawajai hata kiganjani hivyo wananchi wasipoteze muda kwa wapinzani.