Tuesday, March 27, 2018

UBA Sustains Strong Performance with Growing Contribution and Market Share from Africa


  • Official%2BPicture%2Bof%2BGMD%2B-CEO%2Bof%2BUBA%2BPlc%2B%2B-Kennedy%2BUzoka

  • Declares Profit Before Tax of N105.3 billion 
  • Recommends N0.85 Total Final Dividend for the Year

United Bank for Africa Plc has announced its audited results for the financial year ended December 31, 2017, showing significant growth in the contribution and market share from its pan-African subsidiaries, among other positive trends in the financial performance.

The pan-African financial institution’s audited results showed that gross earnings grew substantially to N462 billion, up by 20 percent from N314 billion recorded in the corresponding period of 2017.

According to the report released to the Nigerian Stock Exchange on Friday, the Group delivered a strong 16% year-on-year growth in profit before tax of N105 billion, compared to N90.6 billion in the 2016 financial year. The Profit After Tax also leaped to N78.6 billion, an 8.8% year-on-year growth compared to N72.3 billion in 2016.

The Bank’s subsidiaries outside Nigeria contributed a third of the Group’s top-line and 45% of the profit for the year, a remarkable improvement from 31 percent contribution made by the ex-Nigeria offices in 2016. This, according to market analysts affirms the success of the Bank’s expansion strategy, with target of 50 percent contributions by 2020.

The Bank’s Operating Income grew to N326.6 billion, a 20.6 percent increase compared to N270.9 billion recorded in 2016. This, according to analysts, affirms the capacity of the Group to deliver strong performance through varying economic cycles and challenging business environment.

The audited results also showed that the Bank’s Total Assets peaked at N4.07 trillion, translating into 16.1 percent year-on-year growth from the figure of N3.50 trillion recorded as at 2016 financial year. In the 2017 financial year, the Bank’s Net loans achieved a prudent 9.7 percent growth at N1.65 trillion, while the customer deposits grew to N2.73 trillion, representing 10 percent YoY growth on N2.49 trillion recorded in 2016 financial year.

Reflecting a strong internal capital generation, the Bank’s shareholders’ fund also soared 18.2 percent to N529.4 billion in the 2017 financial year.

Subject to the approvals of the shareholders, the Board of UBA Plc proposed a final dividend of 65 kobo per every share of 50 kobo each. This final dividend proposal is in addition to the 20 kobo per share interim dividend paid after the audit of the 2017 half year financial statements, thus putting the total dividend for 2017 financial year at 85 kobo per share.

Commenting on the result, Kennedy Uzoka, the GMD/CEO, said: “the results, underlines the success of our strategy of expanding across Africa, diversifying revenues and capturing the broader business opportunities inherent in Africa’s growth. The results reinforce the sustainability of our business model and the capacity to deliver superior long-term return to shareholders, as the economic and business environment improve.”

“In 2017, we made strong progress in our strategic initiative of dominating transaction banking across all our countries of operation, gaining market share in all lines of our business. Even as the non-oil sectors of our largest country of operation, Nigeria, remained relatively weak, we still grew earnings by 20% to N462 billion, a third of which is attributable to non-funded income,” he further noted.  

Also speaking on UBA’s financial performance and position, the Group Chief Finance Officer(GCFO), Ugo Nwaghodoh said; “In a period of high interest rates, we achieved a relatively low 3.7% cost of funds. This operational efficiency reflects the benefit of our rich pool of stable savings and current account deposits. The net interest margin stabilized at 7%, even as yields on treasury assets dropped in the last quarter of 2017. Our core transaction banking offerings gained strong momentum, with income from these business lines growing by double digits.”

“We remain committed to our responsible approach to balance sheet management, with focus on growing risk asset and broader balance sheet in a profitable and prudent manner. Amidst a subdued Nigerian credit market, we grew our loan portfolio by 10%, leveraging our robust liquidity and capitalization to support good businesses through this challenging economic cycle. We closed the year with a Basel II capital adequacy ratio of 19% and a liquidity ratio of 50%, well ahead of 15% and 30% regulatory requirement respectively. Our disciplined approach to lending and broader risk management continues to uphold our asset quality.” 

Apart from the strong financial performance in 2017, UBA Group proved its leadership on the continent as the Banker Magazine crowned the Group, “African Bank of the Year 2017”.  To further demonstrate the group’s strength and dominance in the financial sector on the continent, four of UBA Group’s operations in Africa also led contenders in their respective countries to emerge the Best Bank of the Year 2017 in their respective markets. UBA Congo, UBA Tchad, UBA Gabon and UBA Senegal emerged the Best Bank of the Year in Congo, Tchad, Gabon and Senegal, reinforcing the strong franchise of the Group across its chosen markets in Africa.

United Bank for Africa Plc is a leading financial services group in sub-Saharan Africa, with presence in 19 African countries, as well as the United Kingdom, the United States of America and France.
From a single country operation founded in 1949 in Nigeria, Africa's largest economy, UBA has emerged as a pan-African provider of banking and other financial services, to c.10 million customers globally, through one of the most diverse service channels in sub-Sahara Africa; 632 business offices, 1,750 ATMs, some 13,500 PoS, and a robust online and mobile banking platform.
UBA was the first Nigerian bank to make an Initial Public Offering (IPO), following its listing on the NSE in1970. It was also the first Nigerian bank to issue Global Depository Receipts (GDRs). The shares of UBA are publicly traded on the Nigerian Stock Exchange (NSE) and the Bank has a well-diversified shareholder base, including foreign and local institutional investors as well as individual shareholders.

MICHUANO YA COPA COCA-COLA UMISSETA 2018 YAZINDULIWA MKOANI DODOMA

Waziri Jafo akigawa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za sekondari zitakazoshiriki. Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo, akiongea wakati wa uzinduzi huo. Waziri Jafo akikagua moja ya timu na kugawa vifaa kwa baadhi ya shule za sekondari
Waziri Jafo katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa UMISSETA baada ya uzinduzi.
Wakazi wa Dodoma walijitokeza kushuhudia uzinduzi.

Mashindano ya shule za sekondari ya UMISSETA ngazi ya mkoa yamezinduliwa mkoani Dodoma, na mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Waziri wa TAMISEMI,Selemani Jafo.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari,walimu, viongozi mbalimbali wa mkoa na michezo.

Mbali na uzinduzi,Waziri alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari zilizokuwepo kwenye uzinduzi huo.Vifaa hivyo vya michezo vimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano haya,ambapo mwaka huu imepanga kutoa vifaa vya michezo kwa shule 4,000 za sekondari zilizopo sehemu mbalimbali nchini.

Waziri Jafo, alisema kampuni ya Coca-Cola kwa kudhamini mashindano hayo kutafanikisha jitihada za kuendelea kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi wa michezo ya soka ,mpira wa kikapu na pia kupitia mashindano haya kutaibuliwa vipaji vya wanariadha watakaotamba katika kipindi cha miaka ijayo. 

 “Nafahamu kuwa udhamini wa Coca-Cola wa mashindano haya unamalizika mwishoni mwa mwaka huu,lakini natoa ombi maalum iangalie uwezekano wa kuendelea kuongeza kipindi cha kutoa udhamini .

Mashindano haya ya UMISSETA ni tanuru ya kuibua vipaji na rekondi ipo ya wachezaji wazuri wa soka waliofanya vizuri na wanaoendelea kufanya vizuri katika michezo mbalimbali,vipaji vyao viliibuliwa katika mashindano haya wengi pia wamechezea baadhi ya klabu kubwa za soka za Yanga na Simba”alisema. 

Waziri Jafo,alitoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini mashindano ya michezo kuanzia ngazi za chini,na kusisitiza kuwa sekta ya michezo inazidi kukua ambapo hivi sasa lengo lake sio burudani bali ni biashara kubwa na ushahidi wa suala hili upo wazi. 

Jafo pia alishauri kamati ya maandalizi ya mashindano haya ya UMISSETA ,kwa miaka ijayo ihakikishe uzinduzi wake ngazi ya kitaifa unafanyika mkoani odoma badala ya mkoani Mwanza ili yaendane na mkakati wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ya kuhamishia shughuli za serikali katika mji wa makao makuu ya nchi. 

Kwa upande wake Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo,alisema kampuni ya Coca-Cola inajivunia kuwa mdhamini wa mashindano haya kwa kipindi cha miaka 3 mfulilizo na inaamini vipaji vingi vimeibuliwa na vitaendelea kuibuliwa .

”Udhamini wetu katika mashindano haya tumejikita katika kutoa vifaa vya michezo kwa wachezaji wanaoshiriki kuanzia ngazi ya mkoa hadi ngazi ya taifa,kutoa mafunzo kwa makocha wanaofundisha timu na zawadi kwa timu zinazofanikiwa kufanya vizuri”,alisisitiza 

Shayo alisema mbali na uzinduzi wa UMISSETA ngazi ya mkoa uliofanyika mkoani Dodoma utafanyika katika mikoa ya Kagera,Tanga,Mtwara,Singida na Zanzibar ambapo uzinduzi kwa ngazi ya taifa utafanyika mkoani Mwanza ambapo pia mashindano haya yatafanyika.

MECHI YA MBEYA CITY NA YANGA YAPIGWA TAREHE SOMA HAPA KUJUA ..


Tokeo la picha la mbeya city vs yanga
Mechi namba 199 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mbeya City na Yanga iliyopangwa kufanyika Mei 1, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya itapangiwa tarehe nyingine.

Uamuzi wa kuipangia tarehe nyingine ni kukidhi matakwa ya Kanuni inayotaka nafasi kati ya mechi moja na nyingine isiwe chini ya angalau saa 72.

Kwa mujibu wa ratiba, Yanga itakuwa na mechi dhidi ya Simba itakayofanyika Aprili 29, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA

Monday, March 26, 2018

MAALIM SEIF ALIPONGEZA BARAZA LA MAASKOFU KWA WARAKA WAO

KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amelipongeza Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kutoa waraka mzito wa ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka.
 Tokeo la picha la maalim seif leo
Waraka huo ulitolewa mwishoni wa wiki iliyopita ambao mbali na kuzungumzia masuala ya kiroho, umetaja changamoto tatu na kuzifikisha kwa waumini wake “ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.”

Changamoto zilizotajwa katika waraka huo uliopewa jina la “Taifa Letu Amani Yetu” na kusainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini ni hali ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa na masuala mtambuka likiwamo suala la Katiba Mpya.

Akizungumza leo Machi 26, 2018 jijini Dar es salaam wakati akisoma maazimio manne ya Kamati ya Utendaji ya Taifa ya chama hicho iliyokutana leo, Maalim Seif amesema anafarijika kuona  viongozi wa dini  wanakemea mambo ambayo hayaendi sawa nchini.

“Nimefarijika kuona viongozi wa taasisi za dini wakizungumza pale ambao wanaona mambo hayaendi sawa. Tusitafsiri  kwamba wanafanya siasa, hapana ni haki yao kukemea, ” amesema Maalim Seif.
Amesema angetamani kuona viongozi wengine wa dini  wakionyesha misimamo kama maaskofu hao.

Aidha, Maalim seif amemponda Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba kwa kitendo cha kuwavua uanachama wanachama nane na kupoteza sifa za kuwa wabunge jambo ambalo wamepambana hadi kurudishiwa uanachama baada ya kudai haki yao mahakamani.

Maalim amesema kwa sasa wanafanya jitihada za kisheria ili kuwarudisha wabunge hao Bungeni wakati kesi yao ya msingi ikiwa inaendelea mahakamani.

WAKAZI WA WILAYA YA MKINGA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI WA SHIRIKA LA KITAIFA LA WATER MISSIONS INTERNATIONAL TANZANIA

 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Ndunguru (wa tatu kutoka kushoto) akiongoza wadau mbalimbali kufungua bomba wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Mkinga mkoani Tanga.
Wadau wa mradi wa maji wa Mkinga wakibeba ndoo kwa pamoja wa hafla ya uzinduzi wa mradi.
Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International Tanzania, Isack Abdiel, akielezea mradi huo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wanafunzi na wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo.
Kisima cha maji kilichokuwa kinatumika kabla ya mradi mpya.
Sehemu ya miuondombinu ya mradi mpya.

                            Na muandishi wetu
Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na kusambaza huduma za maji la Water Missions International Tanzania, mwishoni mwa wiki limezindua mradi mkubwa utakaonufaisha vijiji 7 vya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga utaowawezesha wananchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa matumizi yao na matumizi mengineyo na shughuli za kiuchumi. 

Kwa kipindi cha muda mrefu wilaya ya Mkinga imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji salama, kutokana na kutokuwepo na vyanzo vya uhakika vya maji katika eneo hilo.

Vijiji 4 vya Mkinga, Mtenguleni, Mwakihonda and Karoyo vimekuwa vikitegemea kupata maji ya bomba kutoka tanki la zamani la kusambaza maji kutoka kijji jirani cha Parangukasere, ambalo limekuwa halitoshelezi mahitaji ya maji kwa wakazi wa vijiji hivyo. 

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga,Mhandisi Michael Gregory Ndunguru,ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo alisema “Leo ni siku ya kihistoria kwa wakazi wa Mkinga,kuzinduliwa kwa maradi huu wilayani hapa kutawezesha wananchi kupata maji safi ya uhakika wakati wote, kwa niaba ya serikali nalishukuru shirika la Water Missions International Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania ya kukabiliana na changamoto za uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali nchini”. 

Mhandisi Ndunguru, alisema mradi huu utanufaisha maisha ya mamia ya wananchi wakazi wa Mkinga na kupunguza adha kwa wanawake ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kifamilia . 

Alitoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano wa shirika hilo sambamba na kutunza miundo mbinu itakayowekwa katika maeneo yao ili kuwezesha mradi kuwa endelevu. 

 “Mradi huu muhimu hapa Mkinga pia utaimarisha afya na kupunguza uwezekano wa kutokea magonjwa mbalimbali yanayosababisha na ukosefu wa maji na matumizi ya maji yasiyo salama kwa kuwa hivi sasa tuna uhakika wa kupata maji salama,”alisisitiza. 

Kwa upande wake,Mratibu wa Huduma za Maendeleo wa Shirika la Water Missions International Tanzania ,Isack Abdiel alisema “Tunayo furaha kuzindua mradi wa maji katika wilaya ya Mkinga ,ukiwa ni mwendelezo wetu wa kuunga mkono serikali ya Tanzania kuboresha upatikanaji wa maji ya uhakika na salama kwenye jamii zenye upungufu wa maji nchini, tunayo imani wananchi mmeupokea vizuri na mtaulinda ili uwe mradi endelevu ili unufaishe mpaka vizazi vijavyo”. 

Aliwashukuru watendaji wa serikali,mashirika yasiyo ya kiserikali inayoshirikiana nayo na wadau wote ambao wamefanikisha jitihada za kuanzisha mradi huu wilayani Mkinga. Shirika la Water Missions International Tanzania, lilianza kufanya kazi nchini mnamo mwaka 2013, likiwa limejikita katika kuendesha miradi ya kuondoa kero ya maji kwenye jamii ,sambamba na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu miradi ya maji.

Hadi kufikia sasa shirika limefanikisha miradi ya maji katika mikoa zaidi ya 6 nchini,ikiwemo mikoa ya Dodoma, Arusha, Geita, Kagera na Tanga. 

Ofisi za makao makuu ya Water Missions International Tanzania nchini yapo jijini Dar es alaam na ndipo inaporatibiwa miradi yote ya maji inayoendeshwa na shirika nchini .

Tanzania ni nchi ya 10 kuwa na miradi ya shirika hili.Baadhi ya nchi nyingine linapoendesha miradi ya maji ni Kenya, Uganda, Malawi, Haiti, Honduras, Mexico, Peru, na Belize.

TPDC YAIMARISHA SEKTA YA AFYA KIDUNDAI, LUSHOTO

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidundai, Ndg. Waziri Mdoe (Kushoto) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni nne kutoka kwa mwakilishi wa TPDC, Ndg. Asiad Mrutu (Kulia). Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya jengo la zahanati inayoendelea kujengwa katika Kijiji hicho. 

Na Mwandishi Wetu.

Katika jitihada endelevu za utekelezaji wa dhana ya uwajibikaji kwa jamii, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambalo ni Shirika la Mafuta la Taifa kwa mujibu wa Sheria ya Petroli (2015) limeendelea kuitekeleza dhana hiyo kwa vitendo kwa kutoa vifaa vya ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kidunda Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. 

Katika tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, TPDC imeweza kukabidhi hundi ya Shilingi milioni nne ambazo Kijiji kiliomba kusaidiwa ili kuwezesha ujenzi wa zahanati hiyo ambapo kwa mujibu wa serikali ya Kijiji, fedha hizo zitawezesha manunuzi ya mizunguko ya nondo 40 yenye futi 40 kila moja, mifuko ya saruji, matofali na gharama za kumlipa fundi ambapo mpaka kufikia hapo zahanati itakuwa imefanikiwa kuezekwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari mara baada ya kumaliza makabidhiano, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidundai kilichopo Kata ya Vuga, Waziri Mdoe alisema “kwa niaba ya halmashauri ya kijiji, tunayo furaha isiyo kifani kwa ndugu zetu kutoka TPDC kwa moyo wa kutoa walioonyesha kwa kusaidia ujenzi wa zahanati yetu ambayo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji hicho ili kuondokana na adh ya kutembea umbali wa kilomita nane ili kupata huduma ya afya”. 

Mdoe aliongezea kuwa, ni matumaini ya kijiji kwamba TPDC litaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika Kijiji cha Kidundai kwani mahitaji yao ni mengi yakiwemo maji, barabara na shule.

Akikabidhi mfano wa hundi kwa Mwenyekiti wa Kijiji kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Asiad Mrutu ambaye ni Mjiolojia alisema “kipekee nimshukuru Mwenyekiti na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji kwa ushirikiano waliouonyesha toka tulipofika siku ya kwanza katika Kijiji hiki tukiwa na lengo la kutafuta eneo la uwekezaji, niseme tu kuwa huu ni mwanzo na tutaendelea kushirikiana bega kwa bega kusukuma gurudumu la maendeleo ya Kidundai mbele.” 

Pamoja na kukabidhi hundi hiyo, Mrutu aliusisitiza uongozi wa Kijiji kuchanganua gharama za miradi ya maendeleo iliyopo katika mipango ili kurahisisha pale ambapo mdau wa maendeleo anaetaka kuchangia kufahamu ni kiasi gani kitatosha badala ya kueleza mahitaji kwa ujumla, hii itasaidia kupata msaada kirahisi na pia kupata msaada unaokidhi mahitaji ya mradi husika. 

Mchango wa ujenzi wa zahanati hiyo umekuja baada ya TPDC kufanikisha zoezi la kupata ardhi kwa ajili ya miradi ya kimkakati ya utafiti wa mafuta na gesi hapa nchini kwa lengo la kuongeza kiasi cha gesi asilia nchini ambacho kwa sasa ni futi za ujazo trilioni (TCF 57.538) na upatikanaji wa mafuta ili kuweza kulihakikishia taifa nishati ya kutosha kwa ajili uzalishaji wa umeme, vyombo vya usafiri, matumizi ya nyumba na kuhakikishia nishati ya kutosha kwa maendeleo ya viwanda nchini.

UBER IMEZINDUA HUDUMA MPYA YA uberPOA JIJINI DAR ES SALAAM

Dar es Salaam, 26.03.18…..Leo kampuni ya Uber imetangaza ujio wa huduma mpya ya uberPOA huduma hii ni ya bei nafuu inayolenga bajaji ikiwa ni juhudi za kupiga jeko huduma ya uberX jijini Dar es Salaam. Huduma hii mpya, ambayo wateja wataanza kufurahi kuanzia leo, itatolewa na bajaji au tukutuk ambazo zinatumia mafuta kidogo. uberPOA itawapa wasafiri wa sasa na wapya fursa ya kutumia huduma ya bei nafuu wanapofanya safari zao jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia huduma hii, Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, Bw. Alfred Msemo amesema, ‘Leo tunafuraha kubwa tunapozindua huduma hii ya uberPOA ambayo ni ya bei nafuu itakayotolewa na bajaji. Tuna furaha kwa sababu uberPOA inawapa wasafiri uhuru wa kuchagua huduma ya usafiri ambayo ni ya bei nafuu zaidi. Ujio wa huduma hii ni mkakati endelevu wa juhudi makusudi za kutumia ubunifu utakaoimarisha huduma tunazotoa katika kuafikia dhamira yetu ya kutoa usafiri salama, wa uhakika, na kwa bei nafuu jijini Dar es Salaam.”
uberPOA itatumia bajaji ambazo kwa ujumla hazina gharama kubwa ya matengenezo. Huduma ya UberPOA itatolewa sanjari na huduma ya sasa ya uberX inayotolewa na magari madogo ya aina ya sedan. “Tuna imani kwamba wasafiri jijini Dar es Salaam wana haki ya kuwa na uhuru wa usafiri ambao wangependa kutumia wanapofanya shughuli zao katika jiji letu, usafiri ambao ni wa bei nafuu na wenye  kuleta ufanisi mkubwa katika maisha yao - uberPOA inatoa fursa hii.” Ameongeza Bw. Msemo.
Bei ya chini ya uberPOA itakuwa Tsh 1,500, Tsh 400 kwa kila KM, Tsh 80 kwa kila dakika, nei ya chini kabisa ambayo msafiri anaweza kulipa ni Tsh 2,000 na ada ya kughairi safari ni Tsh 2,000. “Kampuni ya Uber tunaamini ya kwamba wasafiri na washirika wetu wana kila sababu ya kujua nauli watakayolipa na namna wanavyotumia Uber katika shughuli zao za kila siku.” Amesema Bw. Msemo.
Wakati wa kuzindua huduma hii ya UberPOA, kampuni ya Uber imekariri kwamba imeweka mkakati utakaowahikikishia madereva kiasi fulani cha mapato katika kipindi hiki wanapozindua huduma hii hapa jijini. Ili wasafiri wapate huduma hii, wanatakiwa kufungua programu yao ya Uber ambapo watakuwa na nafasi ya kuita usafiri wa UberPOA au UberX. Kwa sasa huduma ya uberPOA inapatikana maeneo ya Mwenge, Sinza, Kijitonyama, Mikocheni A, Mwananyamala, Kinondoni, Namanga, Msasani, Oysterbay, Masaki & Kigamboni ingawa huduma hii inasambaa maeneo mengi katika siku za baadaye.

Uber imejijengea utaratibu wa kuzindua bidhaa mpya, hali ambayo inaleta upatikanaji wa huduma aina mbalimbali ambazo zitakuwa na tija kubwa kwa wasafiri na madereva washirika. Katika nchi jirani ya Kenya, tayari kampuni ya Uber imezindua huduma kadhaa kama vile uberCHAPCHAP, uberX na UberSELECT. Katika miji mbalimbali duniani kampuni ya Uber inatoa huduma kama vile uberMOTO, UberXL, UberBLACK, UberCHOPPER, UberASSIST, UberEXEC na UberPool.

Sunday, March 25, 2018

KITUO CHA SAUTI YA JAMII CHAIBUKA NA MBINU MPYA YA KUTOA ELIMU BILA MKUSANYIKO, ILI KUKWEPA CORONA

Wakati serikali ya Tanzania ikiungana na mataifa mengine duniani katika kusitisha mikusanyiko isiyo ya lazima, hii ikiwa ni pamoja na kuweka zuio la mikutano, semina na makongamano mbalimbali ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa hatari wa Corona unaoisumbua dunia kwa sasa.

Mkurugenzi wa Kituo cha Sauti ya Jamii Kipunguni Selemani Bishagazi akibandika kipeperushi katika moja ya bajaji, hii ikiwa ni moja ya kampeni yao waliyoipa jina la Waelimishe bila Kuwakusanya.

Katika kutii na kutekeleza agizo hilo la serikali Kituo cha Sauti ya Jamii kilichopo kata ya Kipunguni jimbo la Ukongo jijini Dar es salaam kupitia kitengo chake cha msaada wa kisheria (Paralegal) wamefanya majaribio ya kampeni yake mpya waliyoipa jina la Waelimishe bila kuwakusanya. 

Akiongea na Habari 24 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo 
Bw. Selemani Bishagazi amesema kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa kubandika vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali zinazoonyesha madhara ya Ukeketaji, Rushwa ya Ngono, Mimba na ndoa za utotoni pamoja na kuwahamasisha wanawake kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi.

 "Vipeperushi hivi tunaviweka maeneo ambayo lazima wanajamii wafike kupata huduma, lengo ni kuendeleza kutoa elimu ili kuzuia ukatili katika mazingira haya haya tunayoishi bila mikusanyiko kama ilivyoagiza Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutofanya semina wala mikutano ili kukabiliana na Corona". alisema Bishagazi

Ameongeza kuwa inabidi tuendelee kufahamu kuwa baadhi ya watumishi wa serikali ndiyo wapo likizo, lakini watekelezaji wa vitendo vya ukatili hawajaenda likizo wapo na wanaendelea na mambo yao kama kawaida.

Katibu wa Kituo cha Sauti ya Jamii Kipunguni Sada Shifta akibandika kipeperushi katika bodaboda, ikiwani muendelezo wa kampeni ya Waelimishe bila Kuwakusanya.

Hivyo kwa kuwa nasi tunamafunzo yakutosha hatutaweza kuacha jamii ikapotea na ndio maana tumeamua kutumia njia hii mbadala ya kutoa elimu kwa jamii iliyotuzunguka.

Ameendelea kusema kuwa wamekuwa wakitoa elimu hasa kwenye mitandao ya kijamii na kugundua kuwa walengwa wakubwa wa vitendo hivi ni watoto ambao hawana simu janja(smart phone), hivyo njia hii ya vipeperushi itakuwa sahihi kuwafikia na kuwaelimisha kuhusu Viashiria, Madhara, Mbinu za kujiokoa na wapi mahali sahihi pa kutoa taarifa.

Na mwisho ametoa wito kuwa wadau wajitokeze kuibeba kampeni hii ili isambae kwenye Kata zote zilizopo ukonga ukizingatia huu ni  mwaka wa ukeketaji katika maeneo mengi ya jimbo hilo.



Baadhi ya vipeperushi vikiwa vimebandikwa katika maeneo mbalimbali ya biashara katika kata ya kipunguni.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Kipunguni wakisoma jumbe mbalimbali zilizobandikwa na viongozi wa Kituo cha Sauti ya Jamii Kipunguni.

DJ Luke Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV 2018

Turn off for: Swahili
Matokeo ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Lucas Mukami (DJ Luke) ibuka mshindi wa Urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV kwa kura 315, dhidi ya Liberatus Mwang'ombe, aliepata kura 262. akifuatiwa na Rebeca 24.
VICE PRESIDENT Joha 352 Joyce 248. SECRETARY Cleopatra 311 Omby 214 Dotto 70. ASST SECRETARY Saria 360 DMK 23. ASST. TREASURY Magret 263 Mikidadi 329.... BOARD Mashaka 413 Zena 296 Jabil 330. Pius 454 Asha 386 Hamza 295 Ruth 250.

UZINDUZI WA DUKA JIPYA TECNO-EXPERIENCE CENTER SAMORA

             
Kampuni ya simu za mkononi, TECNO inayofanya kazi chini ya TRANSSION HOLDINGs imezidi kutanuwa wigo  wa soko la simu nchini kwa kufungua duka jipya maarufu  “Experience Center’’ Dar es salaam, Samora, jumamosi  24/03/2018, uzinduzi huo ulihudhuriwa na naibu waziri mawasiliano na uchukuzi mheshimiwa Atashasta Nditiye,  watu maarufu, wageni waalikwa, wadau wa TECNO kutoka mtandaoni na nyanja mbalimbali nchini.
 
Mgeni rasmi Naibu waziri mawasiliano na uchukuzi Mheshimiwa Atashasta Nditiye alishiriki zoezi la kukata utepe pamoja na mkurugenzi mkuu wa TECNO Bwana Xu pamoja na meneja wa Clouds media group Ruge Mutahaba

Mheshimiwa pia aliweza kuzunguka  sehemu mbalimbali za duka hilo kujionea huduma mbalimbali zinazopatikana,ni wazi TECNO imekua chachu ya kukuza Teknolojia na mawasiliano ambapo aslimia 94 ya wananchi wana mawasiliano nchini, lakini napongeza kitendo cha watumiaji kupewa elimu ya namna ya kutumia simu janja kuepuka uhalifu, nawapongeza sana TECNO ”alisema Naibu waziri Nditiye.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa TECNO nchini, Daniel Xu alisema “Ni furaha kujumuika nanyi katika uzinduzi wa duka la TECNO “Experience Center”, wateja watapata fursa ya kununua bidhaa, kupewa elimu ya bure kuhusiana na matumizi,sifa na mifumo mbalimbali ya simu, lakini pia huduma ya matengezo “after sales service” kupatikana papo hapo dukani.

Uzinduzi huu unatoa fursa nyingine ya ajira kwa vijana wa kitanzania ili kuwainua kiuchumi, ambapo zaidi ya vijana 500 wa kitanzania wameshaajiliwa kwenye kampuni ya TECNO,Mkurugenzi Xu alimaliza.
Pia sherehe hzio zilipata ugeni kutoka kwa wanamuziki na mastaa tofauti tofauti ikiwemo mchekeshaji almaarufu kama JayMondy, ambapo alijuimika na wadau wa TECNOkupitia kurasa zake za mtandaoni. Kulikua na michezo, elimu na burudani kabambe na bahati nasibu.

Naibu waziri Nditiye akiendesha zoezi la bahati nasibu,na baadaye alikabidhi zawadi kwa wateja waliojishindia zawadi kabambe kupitia droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa kwa hisani ya TECNO.

Naibu waziri Mh. A. Nditiye, Mkurugenzi wa TECNO na meneja masoko Franck Luo, wakiwa na baadhi ya washindi wa bahati nasibu.

Kampuni ya TECNO inawakaribisha katika duka lao jipya linalopatikana Samora, Posta.

Saturday, March 24, 2018

NAPE NAUYE AKUMBUSHIA KITENDO CHA KUTISHIWA BUNDUKI NA WANYAMA WASIOPENDA HAKI

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amezungumzia tukio la kutishiwa bastola wakati akitaka kuzungumza na waandishi wa habari nje ya Hoteli ya Protea lililotokea baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Nape amekumbushia tukio hilo la Machi 23, 2017 na kuandika, “mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwenyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi.”

Katika ujumbe huo Nape aliweka picha yake ya video akizungumza na waandishi wa habari nje ya hoteli hiyo kueleza masuala mbalimbali, huku akiwataka vijana kudai haki zao bila woga.

Mtu aliyemtishia bastola Nape alikuwa pamoja na wenzake wawili ambao kwa pamoja walikuwa wakimlazimisha arudi kwenye gari lake na kuondoka, lakini mbunge huyo aligoma na ndipo (mtu huyo) aliporudi nyuma na kuchomoa bastola kutoka kiunoni  kisha kumtishia kabla ya kutulizwa na mwezake.

Baada ya tukio hilo watu hao walitoweka eneo hilo muda mfupi baadaye.

Kufuatia tukio hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema mtu aliyemtishia bastola Waziri huyo wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hakuwa askari wa Jeshi la Polisi.

Soma: Mwigulu: Aliyemtishia Nape bastola si polisi

Mwigulu alieleza hayo baada ya kufungua mkutano wa kazi wa mwaka wa maofisa waandamizi wa polisi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi wa Jeshi la Polisi  uliofanyika mjini Dodoma.

Hata hivyo, Mwigulu alikataa kueleza kwa undani kuhusu mtu huyo kwa kubainisha anatoka taasisi gani wala jina lake.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ATOA ONYO KALI KWA WAANDAMANAJI WA MANGE

Tokeo la picha la polisi wakifanya mazoezi
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotumia vibaya mitandao hiyo kufanya uharifu ikiwemo kuhamasisha maandamano yasiyo halali.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Naibu Kamishina Ahmed Msangi ametoa onyo hilo hii leo wakati akizungumza na askari waliokuwa kwenye mazoezi mbalimbali yaliyofanyika katika uwanja wa polisi Mabatini Jijini Mwanza.
Baadhi ya askari walioshiriki mazoezi hayo wameeleza kwamba yanawasaidia kuwa imara wakati wote na hivyo kutimiza vyema majukumu yao.
Kauli hii inakuja baada ya taarifa mbalimbali kuzagaa mitandaoni zikihamasisha wananchi kufanya maandamano ya amani Aprili 26 mwaka huu, siku ambayo ni Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo tayari maandamano hayo yamepigwa marufuku na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
BMG Habari-Pamoja Daima!