.
Friday, February 28, 2014
TAARIFA MUHIMU KUTOKA AZAM TV JUU YA KUONYESHA MECHI YA YANGA LEO
Tumepokea maswali na simu nyingi sana zikiuliza kama
Azam TV itaonesha mechi kati ya Yanga na Al Ahal leo, jibu ni kwamba HAPANA... Ukweli ni kwamba tulipokea maombi toka kwa agent
aliyenunua pambano kwa niaba ya Watu wa Misri ambaye aliomba Azam TV impe
gharama za kuzalisha ili kuweza kupeleka feed yenye ubora wa kimataifa North
Africa & Middle East na ikiwezekana kuonesha nchini Tanzania. Katika vikao
vyote na Agent Azam TV iliweka wazi kuwa ipo tayari kuzalisha bure na hata kama
ikibidi kuonesha delayed sawa kwa kuwa Yanga walionesha wazi kuzuia Live
Coverage nchinikwa kuhofia mapato kupungua.
Bahati mbaya Yanga waliikataa Azam TV na kuamua
kutoa pesa waliyolipwa kukilipa kituo kimoja nchini ambacho ndicho kilichopewa
kandarasi kwa malipo licha ya kutokidhi vigezo vya watu wa Egypt ambao walitaka
angala 8 Camera OB na Azam TV iliwapa 10 Camera OB with HD Feed
Kwa taarifa hii tungependa kuwaarifu wateja wetu
kuwa Azam TV ilikuwa tayari kuwapa Yanga na Agent ushirikiano wote ili pesa yote
waliyopewa na Watu wa Misri iingie klabuni lakini wao wameamua kuitumia kulipia
production iliyo sub-standard ili mradi tuu kuinyima fursa Azam TV
Pamoja na haya yote Azam TV inaitakia kila la kheri
klabu ya Yanga kwenye mchezo wake wa leo, na inaamini matatizo hayapo kati ya
Azam na Yanga kama taasisi bali mtu mmoja mwenye nguvu ndani ya Yanga
JAMANI JAMANI MTOTO HUYU ANAITAJI MSAADA WENU WATANZANIA,INATISHA SANA,ONYESHA UPENDO KWA KUMSAIDIA.samahani kwa picha ila ndo ukweli
Mtoto Adolotea Njavike (1.4) ambaye kichwa na kiwiliwili vimeungana baada ya kupata ajali ya moto akiwa na mama yake mzazi.
UGONJWA WA MIGOMO WAANZA TENA TANZANIA--WAFANYAKAZI WA TRL LEO WATANGAZA MGOMO USIO NA KIKOMO,SOMA WANACHOKIDAI
WAFANYAKAZI WAKIFUATILIA KWA MAKINI
MKUTANO HUO, WOTE KWA UMMOJA WAO WAMEAZIMIA KUTOFANYA KAZI MPAKA
FEDHA YAO YA MWEZI WA KWANZA MPAKA WA TATU ILIPWE TENA KATIKA ONGEZEKO
WALILOAHIDIWA KATIKA VIKAO MBALIMBALI.
WAFANYAKAZI
WA SHIRIKA LA RELI HAPA NCHINI MAPEMA HII LEO WAMEWEKA VIFAA VYAO VYA KAZI
CHINI NA KUISHINIKIZA UONGOZI WA SHIRIKA HILO KUWALIPA STAHILI ZAO KAMA
ILIVYOKUBALIWA NA WAZIRI MKUU,
|
KAMPENI ZA KALENGA NA MIZENGWE YAKE,DIWANI WA CCM AKUTWA NA BANGO LA CHADEMA
SERIKALI YATANGAZA AJIRA ZA WALIMU 36,071
KATIKA
kukabiliana na uhaba wa walimu nchini serikali imetangaza kuajiri walimu wapya
36,071 ambapo watapangiwa vituo vya kazi mwezi ujao.
Hatua
hiyo ni mikakati ya serikali katika kukabiliana na uhaba wa walimu ambapo sasa
watakuwa na upungufu wa walimu 21684 kutoka 57755 iliyokuwepo kabla ya kutanga
ajira hizo mpya.
Naibu
waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Kassim
Majaliwa, alisema jana kuwa walimu hao watasambazwa katika shule za msingi na
sekondari nchini.
Alisema
taratibu zote za ajira kwa walimu hao wapya zimekamilika na kwamba mwezi ujao
wote walioajiriwa watakuwa wamepangiwa vituo vyao vya kazi.
YANAYOENDELEA DAR ES SALAAM MUDA HUU
Thursday, February 27, 2014
VITA YA KISIASA SASA IPO JIMBO LA KALENGA--CCM YAFANYA KUFURU KWENYE KAMPENI,MWIGURU NCHEMBA ATUA,AZINDUA KAMPENI SASA NI MWENDO WA SEMA NIKUSEME
Mgombea
Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey William Mgimwa akibebwa Juu
na Wanachama/wapenzi wa CCM mara baada ya Kuwasili Viwanja Vya
Stendi-kata ya Ifunda.
Mapokezi
Mazito yakiendelea ya Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Kijana Mgombea
Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa kwenye uwanja wa
Stedi-Kata ya Ifakara hii leo wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni
za Ubunge Jimbo la Kalenga.
TFF, POULSEN WAKUBALIANA KUVUNJA MKATABA
Uamuzi
huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na
Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
Rais
Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa
ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu
wa vijana.
Naye
Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka
mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za
Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia
benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa
kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.
|
MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KITETO,LHRC YAJA NA TAMKO KALI,SOMA HAPA,BAADHI YA VIONGOZI WAHUSISHWA
BAADHI YA MADHARA MAKUBWA YALIYOJITOKEZA KATIKA MGOGORO HUO |
Wednesday, February 26, 2014
REPORT MAALUM---INASIKITISHA SANA MAISHA YA BIBI AZIZA WA KIJIJI CHA MIJONGENI TANGU NYUMBA YAKE IZOLEWE NA MAFURIKO SASA AMEHAMIA CHOONI,MAISHA YAKE YOTE NI CHOONI.ENYI WATANZANIA TUNSAIDIENI HUYU
Ijumaa ya February 22 majira ya 7 kasoro dakika kadhaa nawasili kijiji cha Mijongweni wilayani Hai. |
Safari yangu hii ni kutizama maenedeleo ya Bib Aziza Mohamed aliyekuwa akiishi chooni baada ya nyumba yake kuezuliwa na mvua yenye upepo mkali ghafla milangoni nakutana na kufuri. |
Hata pale nilipomwacha siku ya kwanza kufika ,Chooni ambako bibi huyo alihamishia makazi yake pia kulikuwa na kufuri. |
MEYA A DAR ES SALAAM AONYESHA WASIWASI WAKE JUU YA RASIMU YA PILI YA KATIBA
Mwenyekiti wa jumuia ya serikali za mitaa nchi Didas Masaburi amelalamikia kitendo cha kutojumuishwa kipengele kinacho husiana na serikali za mitaa katika katika rasimu ya katiba mpya inayotarajiwa kujadiliwa hivi karibuni bungeni mjini Dodoma.
TAARIFA MUHIMU KUTOKA TFF KUHUSU MECHI YA TWIGA STARS NA ZAMBIA.SOMA
Timu ya Taifa ya Zambia (Shepolopolo) inatua nchini kesho mchana (Februari 27 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Tanzania (Twiga Stars) itakayochezwa keshokutwa (Februari 28 mwaka huu).
Shepolopolo yenye msafara wa watu 29 itawasili kwa ndege ya Fastjet ikitokea Lusaka na itafikia kwenye hoteli ya Accomondia kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.
Waamuzi wa mechi hiyo kutoka Burundi wakiongozwa na Ines Niyosaba wamewasili nchini leo asubuhi wakati Kamishna Fran Hilton-Smith kutoka Afrika Kusini atawasili kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South African Airways.
BREAKING NEWZ---KINACHOENDELEA MLIMANI CITY MUDA HUU---UZINDUZI WA KAMPENI YA TAIFA YA KUSAMBAZA UELEWA WA RASIMU YA PILI YA KATIBA YA TANZANIA KWA WANANCHI
Mgeni Rasmi Bi.Maafudha Hamidu akiwa amewasili katika ukumbi
burudani za muziki wa kiafrika maarufu kama makilikili kikiwa jukwaani kwaajiri ya mapokezi ya mgeni rasmi
Baadhi ya Watu wakiwa wanampokea mgen rasmi kwa kupiga makofi
Tuesday, February 25, 2014
MKUU WA WILAYA YA IGUNGA YUPO ZIARANI,LENGO KUHAMASISHA WANACHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA (CHF)
TANROADS WATANGAZA NAFASI ZA KAZI MPYA.HIZI HAPA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF WORKS REGIONAL MANAGER’S OFFICE-KILIMANJARO VACANCIES ANNOUNCEMENT
TERMS AND CONDITION OF SERVICE:
Appointment will be contract terms of two years, renewable subject to satisfactory performance.
1.POSITION TITLE: SHIFT IN CHARGE-(2 POSITIONS)
SCOPE OF POSITION:
Successful applicant must be read to work on “shift” basis including weekends and public holydays. They should be willing to work for considerable lengths of time away from their permanent stations with minimum supervision.
PICHA NNE ZA CHADEMA NA KAMPENI ZA KUSAKA UBUNGE HUKO KALENGA,
Mgombea akisalimia |
Mgombea Grace Tendega akisalimia |
Kamanda Mawazo akiwa na makamanda wa Magulilwa wakiimba na kucheza kabla ya mkutano wa kampeni |
Katibu Mkuu akifurahia jambo na mtoto mdogo wa Kijiji cha Magulilwa baada ya mkutano wa Magulilwa |
HIKI NDICHO KIKOSI KIPYA CHA TAIFA STARS KILICHOTANGAZWA LEO KUIVAA NAMIBIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Namibia (Brave Warriors) itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE,HUU NDIO UFAFANUZI ULIOTOLEWA LEO NA BARAZA LA MITIHANI.SOMA HAPA
UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013
Baraza la Mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance).
Monday, February 24, 2014
SOMA TAMKO ALILOTOA WAZIRI NYALANDU,AMTIMUA MKURUGENZI WA WANYAMAPORI
Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo:
samahani kwa picha hizi hali inatisha sana-----PICHA ZA USTADHI ATENGANISHA KICHWA NA MWILI WA MTOTO JAMALI SALUM LIPAKALE HUKO MBAGALA CHARAMBE HIZI HAPA !!
mwili wa marehemu mtoto Jamali aliechinjwa na ustadhi mbagala charambe mianzini
TAARIFA MUHIMU TOKA TFF.SOMA
Fomu za wagombea kwa ajili ya uchaguzi
wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam zimeanza kutolewa leo
(Februari 24 mwaka huu).
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu
hizo zinazotolewa Idara ya Habari (Maelezo) ni Alhamisi (Februari 27 mwaka huu)
saa 9 alasiri.
Ada kwa wagombea wa nafasi za
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini
Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu
zinapatikana kwa sh. 20,000.
Kwa mujibu wa Ibara ya 21(e)(i), sifa ya
elimu kwa wanaowania nafasi za Mwenyekiti hadi Katibu Msaidizi ni diploma au
digrii ya uandishi wa habari. Kwa nafasi nyingine kwa mujibu wa Ibara ya
21(e)(ii) ni cheti cha ngazi yoyote katika uandishi wa habari.
Tunawahimiza wanachama wa TASWA
kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili waweze kuwania nafasi hizo.
Boniface
Wambura
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TASWA
Subscribe to:
Posts (Atom)