Wednesday, September 30, 2015
VIDEO--Sheikh HEMED JALALA asimulia mkasa mzima aliyoyaona kwenye ibada ya HIJJA
Kiongozi Mkuu wa kiroho
wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA
ameibebesha mzigo wa lawama serikali ya Saudi Arabia kufwatia vifo vya watu
zaidi ya elfu nne vilivyotokea siku chache zilizopita wakati wa Ibada ya hija iliyofanyika
nchini humo huku akisema kuwa vifo hivyo ni uzembe wa wazi wa waandaaji wa
ibada hiyo.
Lawama hizo amezitoa
leo Jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili nchini Tanzania pamoja na
waumini wengine wa dhehebu hilo wakitokea katika ibada hiyo ambapo amesema kuwa
ni wazi mauaji yaliyotokea katika ibada hiyo ni ya kusikitisha sana na
yalitokana na uzembe wa waandaaji wa ibada hiyo kutokana na kasoro nyingi
zilizoonekana.
Amesema kuwa moja ya
sababu kubwa iliyosababisha mauaji ya waumini wengi ni kufungwa kwa njia kubwa
za kutoka na kuingilia wakati wa urushwaji wa mawe kumpiga shetani jambo ambalo
lilisababisha msongamano mkubwa wa watu na kusababisha vifo vingi.
Aidha Sheikh JALALA
ameongeza kuwa katika maeneo yote ya ibada hiyo kulikuwa kumezungukwa na kamera
eneo lote lakini watu walikuwa wakifariki kwa mfululizo kwa kila baada ya
dakika tatu lakini wahusika hawakuona na hakuna msaada wowote ambao ulikuwa
unatolewa na wahusika licha ya kuwepo kwa kamera kila kona.
Baada ya tukio hilo Sheik
jalala amesema kuwa kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa ni lazima serikali ya
Tanzania iungane na nchi ambazo zina idadi kubwa ya mahujaji ambao wanaenda
katika ibada hiyo waweze kushirikishwa katika mipango ya ibada hiyo ili kuweka
mipango ambayo itawafanya waumini kuwa salama wakati wa ibada hiyo kwa kuwa
hakuna mtu anayekwenda katika ibada hiyo kwa ajili ya kufa.
TOROKA UENDEEE--Sasa ni Kesho Dar es salaam,wote mnakaribishwa huko
Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri ni kuwa jana tumekurepotia habari za uzinduzi wa kampeni mpya ya mgombea wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA iliyopewa jina la TORIKA UJE ambayo ilipangwa kuzinduliwa leo Jijini Dar es salaam,Habari za ndani zinaeleza kuwa Watanzania wengi wamekuwa na maombi ya jinsi ya kufika kwenye shughuli hiyo jambpo ambalo limewalazimu waandaaji wa Tukio hilo kulifanya katika maeneo ya wazi ili watanzania wengi waweze kulishughudia.Habari za ndani ambazo tunazo sasa ni kuwa alhamis ndio tukio hilo litafanyika na hii ni moja ya Taarifa ambazo tunazo unaweza kupitia na kushare na wengine
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kinakualika katika mkutano wa mgombea Urais kupitia vyama vinavyounda ukawa mh. Edward Ngayai Lowassa utakaofanyika alhamisi ya tarehe 1 october katika viwanja vya tanganyika pekas kawe kuanzia saa nane mchana wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na maeneo jirani mnakaribishwa UKAWA tumaini letu..
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MWANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA IKULU DAR, AAGANA NA BALOZI WA MALAWI TANZANIA.
Tigo yatoa mchango wa madawati 700 kwa shule za umma mkoani Mbeya
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Nyanda za juu Kusini Jackson Kiswaga akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi madawati.
|
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein Aendelea na Mikutano Yake ya Kampeni katika Viwanja cha Garagara Mtoni Zanzibar,
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni Zanzibar kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua tena kuongoza Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohameid Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndg Yussuf Mohammed akizungumza na Wananchi na WanaCCM katika viwanja vya garagara mtoni wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na kuwatana Wananchi kumpigia kura Dk Shein, ili kuzidi kuleta maendeleo katika Visiwa vya Unguja na Pemba katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Miezi Mitano sasa Tazara Hawajalipwa mishahara,Muda huu Wameamua kukutana,soma hii
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
leo wameibuka na kudai kuwa sasa ni miezi motano hawajui wala kuonja ladha ya
mshahara huku kukiwa hakuna maelekezo wala kauli yoyote kutoka serikalini jambo
ambalo limezua taharuki kubwa ndani ya mamlaka hiyo na kusababisha wafanyakazi
wa shirika hilo kukutana kujadili hali hiyo inayowakumba.
Mtandao huu umekutana
na mkutano uliokuwa unafanyika ndani ya mamlaka hoyo ulioitishwa na chama cha
wafanyakazi wa reli nchini Tanzania TRAWU kikiwashirikisha wafanyakazi wote wa mamlaka
hiyo ambapo mada kuu katika mkutano huo ni kujadili hali ngumu waliyonayo
ambapo wamesema kuwa hadi sasa ni mwezi
wa tano hawajapata mishahara yao huku wakiwa wamelalamika serikalini bila
majibu ya kuridhisha.
Mwenyekiti wa chama
hicho MUSA KALALA amezungumza na mtandao huu kuhusu madhumuni ya mkutano huo
ambapo amesema kuwa lengo lao sasa ni kupaza sauti yao kuhusu mishahara ili serikali iweze kuwasikiliza na kuwasaidia.
Bwana MUSA amesema kuwa
huu ukiwa ni wakati wa uchaguzi ni lazima serikali itambue kuwa wafanyakazi wa
shirika hilo ni wapiga kura,na wanawahudumia wapiga kura hivyo kuwanyima haki
yao kwa muda mrefu kunaweza kusababisha matatizo makubwa kuelekea uchaguzi mkuu
wa mwaka huu.
Ameongeza kuwa kumekuwa
na matatizo makubwa yanayowakumba wafanyakazi wa mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja
na wengine kufukuzwa kazi au kusimamishwa kutokana na kuonekana wanadai haki
yao kwa kasi mbele ya jamii jambo ambalo amesema sasa uongozi wa chama hicho unaliangalia
ili waliofukuzwa waweze kurejea kazini mara moja.
Tuesday, September 29, 2015
Lowasa Yupo Dar es salaam tayari kufanya Tukio hili la kihistoria,Tizama hii
DK. JOHN POMBE MAGUFULI AUNGURUMA MTERA KWA KIBAJAJI, AWAAMBIA WANAMVUMI MSIDANGANYIKE
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika tarafa ya Mvumi jimbo la Mtera wilaya ya Chamwino leo wakati akiendelea na kampeni zake katika majimbo ya Isimani mkoani Iringa, Kibakwe na Mtera mkoani Dodoma, ambapo amewaomba wananchi hao kutohadaika na wagombea wanaowadanganya kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijafanya kitu kwa miaka 54
Dk. Magufuli amesema kuwaambia watanzania CCM haijafanya kitu kwa miaka 54 ni jambo ambalo linachekesha kwani Utulivu na amani tuliyonayo ni matunda ya uongozi bora wa viongozi wa serikali ya CCM waliopita wakiongozwa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere, “Wanapita kwenye barabara za lami zilizojengwa na serikali ya CCM tena nikizisimamia mimi John Pombe Magufuli, Wanatumia miundombinu ya mawasiliano na Umeme uliosambazwa kwa zaidi ya asilimia 40 nchini na serikali ya CCM lakini wanasema haijafanya kitu ni jambo la kushangaza.
Mbaya zaidi wamekuwa viongozi wa serikali tena wakiwa na nyazifa kubwa serikalini, sasa kama walishindwa kuwajibika na kuwatumikia watanzania wakiwa serikalini kwa nini hawakuondoka mapema, Lakini muda wote wakabaki CCM wakisifia mafanikio hayo ambayo leo wanayaponda. Si sawa kabisa hao wanatafuta madaraka kwa kutaka kuwadanganya watanzania nawaasa msikubali kudanganywa waongo hawa.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-MVUMI-DODOMA)
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Isimani mkoani Iringa Mh. Willliam Lukuvi katika mkutano uliofanyika kata ya Pawaga.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika mji wa Mvumi mkoani Dodoma leo.
JAJI LUBUVA amkwepa mbowe kiaina,ni swala la mabadiliko ya Tume
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imeshindwa kuzijibu tuhuma alizotoa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Tuhuma hizo ni zile za ubadilishaji holela kwa wakurugenzi ndani ya tume hiyo pamoja na Idara ya usalama wa Taifa kuhusika katika ufanyaji kazi pia kwenye tume hiyo.
Hayo yabainika leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kati ya watu wenye ulemavu na NEC mkutano huo wenye lengo la kuwapatia uelewa kuelekea uchaguzi mkuu ambapo mara baada ya mkutano huo waandishi wa habari walimfuata Mwenyekitiwa NEC Jaji mstaafu Damian Lubuva ili kutaka kujua kuhusu madai hayo ya Mbowe.
Lowasa Aendelea Kutikisa Tanga leo,Tizama Hii ya mchana
Msafara wa mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha democrasia na maendeleo chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vya UKAWA mchana wa leo imemlazimu kusimama muheza Tanga baada ya mamia ya wakazi wa maeneo hayo kuzuia msafara wake ili tu kumuona na kumsikia.Hapa kuna picha za awali ,picha zaidi za mikutano yake leo zitakujia baadae |
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA HAFLA YA UCHANGISHAJI FEDHA KWA AJILI YA UHIFADHI WA VYANZO VYA MAJI KATIKA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME YA MTERA, KIHANSI, KIDATU, NYUMBA YA MUNGU NA PANGANI.
Monday, September 28, 2015
Tizama alichokifanya Magufuli Nyumbani kwa MSIGWA Iringa
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Samora Manispaa ya Iringa wakati alipokuwa akiwaomba kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Dk. Magufuli amesema “Nipeni kura za ndiyo bila kubagua vyama vyenu kwa kuwa nitakuwa rais wa Watanzania wote wakati nikitekeleza majukumu ya kuwatumikia watanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Hata wale wa CHADEMA huwa mnasema (Peoples Power) mpeni Magufuli hiyo Power ili awe rais wa Watanzania wote” .
Dk. John Pombe Magufuli akizungumza zaidi na wananchi wa Manispaa hiyo amesema Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kujenga mahusiano ya Kidiplomasia na mataifa mbalimbali ndiyo maana Tanzania ina mahusiano mazuri na nchi nyingi duniani zikiwemo nchi jirani, Amesema kwamba mara atakapochaguliwa na kuwa kiongozi wa Tanzania atahakikisha anadumisha mahusiano hayo na kuifanya Tanzania kupiga hatua katika maendeleo ya Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa
Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa leo
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wa tatu kutoka kulia, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Abdallah Bulembo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa pamoja na wasanii wa Bongo Movie wakinyanyua mikono yao juu kama ishara ya Umoja ni Ushindi katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika mjini Iringa leo hii
Tanga Haina Mwenyewe--LOWASA nusura Asababishe maafa makubwa,mamia wazimia,picha zote zipo hapa
Wananchi waliolazwa chini baada ya kuzimia ni ndani ya mkutano ulioahirishwa Tanga uwanja ulikua mdogo sana. . |
TANGA
Chopa iliyombeba Lowassa imeshindwa kutua kwenye eneo la Mkutano kutokana na Umati wa watu waliojitokeza mda huu hapa Tanga
Hivyo imelazimika kwenda kutua airport kisha kurudi uwanjani kwa gari!!
Inaelezwa Tanga ya leo sio ile ya mwaka 47 watu wanataka
Wananchi waliolazwa chini baada ya kuzimia ni ndani ya mkutano ulioahirishwa Tanga uwanja ulikua mdogo sana. .
Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edwrad Lowassa amelazimika kuahirisha mkutano mjini Tanga baada ya maelfu ya wakazi waliojitokeza kushindwa kuenea ndani ya uwanja wa Tangamano jijini Tanga
Kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Tanga shughuli zote zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5,6,7, 8 zililazimika kusimama kwa muda baada ya maelfu ya wakazi wa jiji hilo waliojitokeza katika uwanja wa Tanagmano, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea kwa mkutano huo.
Licha ya juhudi zilizofanywa na viongozi wa UKAWA wakiongozwa Fredrick Sumaye za kujaribu kutuliza hali ya mambo kushindikana jambo lililomlazimu Mh.Edward Lowassa kulazimika kusitisha mkutano huo.
Je? Nini kauli ya Chadema baada ya mkutano huu kuvunjika, John Mrema ni meneja kampeni wa Chadema.
Uamti huo wa wakazi wa jiji la Tanga ulionekana dhahili ulionekana dhahili kuwashinda maafisa wa taasisi ya mslaba mwekundu redcros mjini Tanga.
Akiwa jiji Tanga katika siku yake ya kwanza ya kampeni alifanya mikutano katika maeneo ya Bumbuli Mombo kabla ya kuhitimisha katika uwanja wa Tanagmano mjini Tanga ambapo aliahidi kuboresha sekya ya afya ndani ya siku miamoja baada ya kuapishwa.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU CELINA KOMBANI, DAR, KUZIKWA KESHO MOROGORO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mume wa marehemu Celina Kombani, aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ahmad Pangolani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro. |
Mkutano wa Kampeni Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Shein, Viwanja vya Bungi Zanzibar
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Shamsi Vuai Nahodha akisalimiana naViongozi wa CCM wa Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuwasili katika viwanja vya mkutano wa hadhara wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika viwanja vya mpira bungi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili katika viwanja vya mpira bungu kuhudhuria Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
Wanachama wa CCM wakiingia katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakiwa na picha za Wagombea
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla alipowasili katika viwanja vya Bungu kuendelea na Kampeni zake za kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Sunday, September 27, 2015
Picha za wakina LOWASA na UKAWA walichokifanya nyumbani kwa MREMA Vunjo
Mgombea ubunge jimbo la Vunjo Mhe. James Mbatia akiongea na wananchi wa Kahe jimbo la Vunjo katika viwanja vya Oria shule ya msingi leo Jumapili 27/09/2015 |
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa na Mhe. Fredrick Sumaye wakiwasili katika viwanja vya Oria shule ya msingi na kupokelewa na mgombea wa ubunge kwa jimbo la Vunjo kupitia NCCR Mageuzi,leo Jumapili 27/9/2015 |
Uzalendo wamshinda Mgombea wa CCM JOHN MAGUFULI ataja live jukwaani wanaokihujumu chama chake
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, jana aligeuka mbogo baada ya kuamua kuwataja hadharani watu wanaohujumu kampeni zake kwa kujifanya mchana wako pamoja na usiku wakigeukia upande wa upinzani.
Akiwahutubia wananchi wa mkoani Shinyanga jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage, Dk. Magufuli, alisema kuna mamluki wanaokihujumu chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Saturday, September 26, 2015
Tizama jinsi LOWASA alivyowasili Hai kwa MBOWE kwa kishindo
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati alipowasili eneo la Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI. |
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015. |
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015. |
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015. |
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015. |
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015. |
Subscribe to:
Posts (Atom)