Thursday, August 31, 2017

RC. MAKONDA KUANZISHA KAMPENI YA KUCHANGIA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda ameanziasha rasmi kampeni ya kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu katika jiji la Dar es salaam.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari Mh. Makonda alisema kuwa mahitaji ya walimu ni zaidi ya ofisi 402 hiyo ni kwa walimu wa sekondari na shule za msingi.

Na ujenzi huo unatarajiwa kuanza tarehe 5 mwezi wa 9 na lengo la mkutano huu ni kuitambulisha kamati itakayosimamia zoezi hilo likiwa chini ya mwenyekiti wa kamati hiyo Canal Charles Mbuga akiwakilisha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Katika ujenzi huo JKT imetoa vijana 300 watakao jitolea kujenga ofisi hizo pamoja na jeshi la Magereza wao wakiwa wametoa skari pamoja na Wafungwa watakao saidia kufyatua matofali pamoja na kujenga, bila kusahau Jeshi la Polisi pamoja Channel Ten watakao saidia kuitangaza kampeni hiyo.

Aidha Mh. Makonda alisisitiza kuwa bado mahitaji ni mengi na huu ni mwanzo tu hivyo wanaombwa wadau, wananchi na wapenda maendeleo kujitolea vitu kama Kokoto, Mchanga, Nondo, Cement, Mabati nk.

Pia wananchi wote wanaweza kuchangia huduma hiyo kwa benki ya CRDB akaunti namba 0150296180200 na mchango wao utakuwa umesaidia kujenge ofisi za walimu pamoja kuboresha elimu yetu kwani ukimuwezesha mwalimu utakuwa umeokoa wanafunzi ili waweze kupata elimu bora.

Na mwisho Mkuu wa Mkoa alipenda kuwashukuru wale wote waliowezesha hatua za awali kuweza kukamilika za kuanza kwa ujenzi huu na kwa baadi ya mashirika yaliyojitolea kwa dhati kama TBA pamoja NIC.

SHEIKH JALALA - AKITOA UFAFANUZI WA NAMNA YA KUSHEREKEA EID EL HAJJ

WAKATI  Waumini  wa Dini Kiislam nchini wakiungana na wenzao Duniani kesho  wakiwa wanasherekea sikuku ya Eid  El Hajj,Waumini hao wametakiwa kusherekea sikuku hiyo kwa kuhakikisha wanadumisha amani na upendo katika jamii.

Pia wametakiwa kuhakikisha wanafanya mambo ya kumpendeza mungu katika sikuku hiyo na kuacha kufanya mambo ya kumchukiza Mungu .
Sheikh Mkuu wa Shia Ithnasheria Hemed Jalala akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheria Tanzania, Sheikh Hemed Jalala wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia sikuku hiyo, ambapo amesema sikuku hii ni nembo kubwa kwa waislam ,basi hawana budi kuhakikisha wanaijenga jamii isiyokuwa na aina yoyote ya vurugu.

“Nawaomba waislam tutumie sikuku hii katika kujitafakari na kuhakikisha tunailinda amani yetu hapa nchini Tanzania ,kwa kuleta umoja na mshikamano huu kwetu,na tusikubali kufarakana katika jamii”Amesema Sheikh Jalala.
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria mkutano ulioandaliwa na msikiti wa Al Gadar uliopo Kigogo jijini Dar es salaam

Kiongozi huyo wa kiroho ameenda mbali kwa kuwataka waislam kututumia sikuku hii muhimu kwa kusherekea kwa  kufanya maasi jambo analodai linakwenda kinyume na sheria za dini ya kiislam.
“Mtu anayemkosea Mungu  Siku ya sikuku ya Eid mtu huyu ni kama amemkosea mungu siku ya kiama”amesema Shekh Jalala.

Sheikh Jalala pia ameitaka serikali kuhakikisha wanatumia rasilimali zilizopo hapa katika nchi za  Afrika  zitumike katika kutatua tatizo la ajira.

“Bara la Afrika bado linalinasumbuliwa na matatizo mengi sana ikiwemo umasikini,bado linasumbuliwa na maradhi bado Afrika inasumbuliwa na njaa,basi tunawaomba viongozi wa Afrika kutumia rasilimali zilizopo katika maneno yetu zitumike katika kutatua matatizo ya ajira ili ipatikane jamii yenye kufanya kazi”ameendelea kusema Sheikh Jalala.
 Hata Hivyo,Sheikh Jalala amewataka pia waislam ambao walikwenda kufanya Hija kutumia njia hiyo katika kuhakikisha wanaijenga jamii nzuri isiyo kuwa na aina yoyote ya fujo na mfarakano katika jamii.


ASKARI WANAWAKE WA JKT MGULANI WAFANYA USAFI WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TEMEKE.

 Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama baada ya kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo kuhusu shughuli ya usafi  waliofanya katika Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho nchini.

SABABU YA EID-AL-ADHA KUITWA 'SIKUKUU YA KUCHINJA'

Na Jumia Travel Tanzania

Eid al-Adha ni miongoni mwa sikukuu kubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu ukiachana na Eid- al-Fitr inayosherehekewa kila mwaka duniani kote. Kwa mwaka huu sikukuu hii inatarajiwa kusherehekewa siku ya Ijumaa ya Septemba mosi ambapo kwa waumini wa dini hiyo ni kipindi cha kujitolea, kuonyesha ukarimu kwa marafiki, familia na watu wenye uhitaji.

Kama zilivyo sikukuu nyingine kuna baadhi ya watu huwa hawajui ni kwa nini huwa zinaseherehekewa namna zinavyosherehekewa. Jumia Travel kupitia makala haya imekukusanyia mambo ya msingi kuhusu maana ya sikukuu hii na namna ya kusherehekea.

MAMIA WAMIMINIKA KUJISAJILI KATIKA MFUKO WA FIDIA (WCF) IKIWA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI JENISTA MHAGAMA


Meneja Matekelezo  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na kulipa michango leo Agosti 31, 2017.

Khalfan Said
MUITIKIO wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema leo Agosti 31, 2017.
Itakumbukwa ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.
“Kwakweli tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa agizo alilolitoa kwani limetoa msukumo mkubwa, waajiri wengi wamejitokeza kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko.” Alisema Bw. Luvena
K-VIS Blog ilishuhudia idadi kubwa ya waajiri wakiwa wamejitokeza leo Agosti 31, 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho kwa waajiri kutekeleza agizo la Mheshimiwa waziri, wakiwa wamejazana kwenye ofisi za WCF  kujisajili na kuwasilisha michango, ambapo kazi hiyo ya kuwahudumia ilikuwa ikiongozwa na Meneja Matekelezo - WCF, Bw.Victor Ruvena.
 Waajiri, wakihudumiwa na maafisa wa WCF, leo Agosti 31, 2017.

 Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe, (kulia), akimkabidhi cheti cha usajili Bw.Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refregerator ya jijini Dar es Salaam.
 Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kushoto), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.
 Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, akimsikiliza Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, (kushoto), akimuhudumia Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe,(kushoto), akimuhudumia Bw. Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refrigeration, ya jijini Dar es Salaam.
 Meneja Matekelezo  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwasikiliza waajiri waliofika leo Agosti 31, 2017 ili kupatiwa huduma ya usajili na uwasilishaji michango katika Mfuko huo.
 Maafisa wa WCF (kulia), wakimsikiliza Mama huyu mwajiri aliyefika kupatiwa huduma.



Wednesday, August 30, 2017

NAFL signs MoU with TAFFA to Boost Trade Facilitation


Ms Nadia Abdul Aziz, President of National Association of Freight and Logistics – NAFL (Dubai)signs an MoU with Tanzania Freight Forwarders association President Stephen Ngatunga to boost trade facilitation between Tanzania and U.A.E during the closing ceremony of the Global Logistics Summit 2017 in Dar es salaam


The National Association of Freight and Logistics (NAFL) and Tanzania Freight Forwarders Association have signed a Memorandum of Understanding (MOU), which will enable the two national bodies to work together in promoting efficiency in transit transport and trade facilitation.
The agreement was signed in Dar es Salaam by the newly elected NAFL President, Ms Nadia Abdul Aziz and Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA) President who is also FEAFFA Vice President Mr. Steven Ngatunga in the presence of other stakeholders in freight and logistics fraternity to boost bilateral relations between the two countries.

With the conclusion of 2017 Global Logistics Summit- Tanzania edition 23 – 26th August in Dar es salaam,  The MoU aligns with both association’s objective to facilitate growth of the logistic services industry, which is identified as one of the key contributors in each country’s economic diversification drive.
The move is part of NAFL latest efforts to try seal the deal to host FIATA (International Federation of Freight Forwarders Associations) World Congress in Dubai in 2020.
The NAFL President, Abdul Aziz is currently on overdrive mode in pitching Dubai’s capabilities, innovations and world class reputation. Suggesting to host the event at the same time as Expo2020 will only add to the prominence Dubai can bring to such a congress.
“We strongly believe that bringing the congress to Dubai during Expo2020 would bring the FIATA delegates a chance to secure even more investments, opportunities and deals during a 2020 edition of the event, as well as the other various things that will be exhibited and enjoyed during that time due to Expo2020,” she said.
If NAFL wins the bid to host the 2020 World Congress, it will place Dubai as a significant global hub in the freight and logistics landscape across the globe.
And to win such a prestigious bid, NAFL board is seeking full support of relevant government and semi government entities who will support them to showcase the unique business opportunities in the UAE.
If successful, it would be the first time the prestigious global event has been held anywhere in the region, counting the Middle East, Africa and Asia.
The objective of attending the GLS –TZ 2017 was also to discuss latest initiatives of NAFL and increase NAFL’s logistics network as well as boost its ambitious plan of winning the FIATA World Congress 2020 bid.
Nadia who is also the first Emirati woman from the freight and logistics industry to run the association says NAFL aims to reach newer and bigger heights in coming months.
 “We will always focus on promoting the UAE’s excellent infrastructure, airports, airlines, ports and logistic freezones to investors when we travel for global conferences.
NAFL president has made bringing the International Federation of Freight Forwarders Associations (FIATA) World Congress to Dubai in 2020 the cornerstone of her leadership of NAFL.
"The cooperation comes as part of TAFFA’s commitment to support national strategic plans. Over the coming period, we will implement the memorandum signed to pave the way for one of the greatly beneficial trade partnerships for Tanzanian logistics," he added.
The NAFL & TAFFA MoU also looks to create training opportunities within the logistics industry in the view of increasing Tanzania’s expertise in freight forwarding as it bids to become a regional hub hence creating a win-win situation for both entities concluded Mr. Ngatunga. 

VIDEO ANGALIA YALIYOJIRI KWENYE RIPOTI YA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU

Leo ikiwa ni tarehe 30 ya mwezi agosti mwaka 2017 kituo cha sharia na haki za binadamu kimezindua ripoti yake ya biashara ya mwaka 2016 iliyofanyika kwenye hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo uliudhuriwa na wadau mbalimbali toka taasisi binafsi na serikalini lengo likiwa ni kupata elimu juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye sekta ya viwanda na makampuni mengi hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bi. Helen Kijobisimba akikata utepe wakati akizindua Ripoti ya Biashara ya 2016 katika hotel ya Protea Courtyard mapema leo jijini Dar es salaaam.
Akiwasirisha ripoti hiyo mwanasheria wa Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu Bw. Pasiasi Mloe alisema utafiti huo umefanyika katika mikoa 14 ya hapa nchi kwenye viwanda na makampuni mbalimbali.

Miongoni mwa vitu hivyo ni baadhi ya wafanyakazi wa viwandani na kwenye baadhi ya makampuni kutokuwa na mikataba ya kazi, au mikataba inakuwepo na badala yake anabaki nayo muajiri hali inayofanya wafanyakazi kukosa haki kwenye maeneo yao ya kazi.
Mwanasheria wa Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu Bw. Pasiasi Mloe akiwasirisha ripoti hiyo mbele ya meza kuu pamoja na wageni waalikwa kwenye tafrija iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam
Lakini pia baadhi ya makampuni kutokuwepo na vyama vya wafanyakazi hali inayofanya wafanyakazi kukosa utetezi pale muajiri anapokwenda kinyume na makubaliano, au vyama vinakuwepo lakini vinasimamiwa na waajiri hali inyofanya waajiriwa kushindwa kupata ututezi wowote.

Aidha bwana mloe alisisitiza kuwa wafanyakazi walio wengi kwenye viwanda na makampuni hayo hawajui umuhimu wa mifuko ya hifadhi kuwa inaweza kuwasaidia pale wanapopata tatizo wakiwa kazini hali inayofanya kukosa fidia zao pale wanapopata kilema cha kudumu au tatizo lolote linalofanya wasiweze kufanya kazi tena.
Wafanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu.
Lakini pia tatizo lingine ni kwa upande wa usawa wa kijinsia  kwani makampuni mengi yamesema kuwa hayapendi kuajiri wanawake kwenye kampuni zao kwani hawaamini kama wanaweza kufanya kazi sawa na wanaume, na ndio sababu kwenye viwanda vingi wameajiriwa wanaume wengi na wanawake wapo wachache.

Na kitu kingine wamejaribu kuangalia wakazi wa karibu na migodi pamoja na viwanda je wananufaika vipi na rasirimali hizo kwa kuwa karibu nazo, ikiwa ni kupata ajira na huduma nyinginezo za msingi.



                                            click hapa kuangalia tukiozima lilivyokuwa..

                       

Tigo yakabidhi kisima chenye thamani ya 18m/- kijiji cha Rorya Mara


Mkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kanda ya ziwa, Ally Maswanya akizungumza na wanahabari na wananchi kabla ya kukata utepe wa uzinduzi wa kisima mapema mwishoni wa wiki iliyopita.



Mbunge wa Rorya- Lameck Airo akipampu maji wakati wa sherehe za uzinduzi wa kisima chenye thamni ya Tsh.18/- milioni kilichodhaminiwa na kampuni ya Tigo.


Mkuu wa wilaya Rorya- Samson Chacha akitwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha  Nyasoro, Penina Bailes

iMkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kanda ya ziwa,Ally Maswanya,akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Nyasoro kata ya Bukwe halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoani Mara,Patero Opiyo mara baada ya uzinduzi wa kisima kilichochibwa kwa udhamini wa Tigo chenye thamani ya Tsh.18/- milioni 


Mbunge wa Rorya- Lameck Airo akizungumza na wanahabari na wananchi kabla ya kukata utepe wa uzinduzi wa kisima 


Wanachi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kisima jana.

SASA INAWEZEKANA KUWEKA VITUO VINGI VYA KUSIMAMA UNAPO TUMIA PROGRAMU YA UBER

Kampuni ya Uber nchini Tanzania imezindua zana mpya kwenye programu yake ya Uber inayowapa wasafiri nyenzo za kuweka vituo vingi vya kusimama wanapokuwa safarini. Tafsiri yake ni kwamba kipengele hiki kinawarahisishia wasafiri utaratibu wa kuweka vituo vingine vya kusimama wanaposafari kwa wakitumia mfumo wa Uber.  
Akizungumzia maboresho haya, Meneja Msimamizi wa Uber Nchini Tanzania, Bw. Alfred Msemo amenukuliwa akisema “Programu hii inawaondolea wasafiri na madereva kero ya kubadilisha mahali wanakoenda mara kwa mara, hususan inapotokea kwamba safari ina vituo vingi vya kusimama. Sambamba na kuwasaidia madereva ambao hawana uwezo wa kubadilisha vituo vya kusimama, maboresho haya yanasaidia katika mchakato wa kuendelea na safari kwa sababu vituo hivi vitakuwa ni mwendelezo wa safari.” Mwisho wa Nukuu.
Wasafiri wanaombwa kuingia katika akaunti zao za Uber ili waweze kutumia zana hii na kuita gari. Kupitia kwa zana hii sasa wasafiri wanaweza kugusa alama ya “+” iliyo karibu na kisanduku cha mahali anakoenda “Ungependa kwenda Wapi” ili waongeze kituo kingine cha kusimama wakati wowote wanapokuwa safarini. Kadhalika wasafiri wanaweza kuongeza au kuondoa kituo cha kusimama wakiwa safarini. Kufanikisha hili, wasafiri wanatakiwa kuongeza, kubadilisha, au kuondoa mahali wanakoenda kwenye skrini ya safari iliyo kwenye programu ya Uber.
Kipengele hiki kimetusaidia kurahisisha utaratibu wa kushukisha wasafiri njiani. Ima unaenda kwenye mtoko na ungependa kuwachukua marafiki zako njiani ukielekea katika uwanja wa ndege, au unarudi nyumbani baada ya shughuli zako mjini na ungependa marafiki zako washuke njiani, sasa haya yote yako kiganjani mwako,” amesema Bw. Mr. Msemo.
Jinsi ya kutumia kipengele hikii:
Screen Shot 2017-08-21 at 4.35.11 PM.png

MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 30 YA DROO YA JUMAPILI YA JACKPOT YA TATU MZUKA AKABIDHIWA FEDHA ZAKE

 Balozi wa Mchezo wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kushoto), akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 30 mshindi wa droo ya Jumapili ya Jackpot ya Tatu Mzuka, Tausi Mashombo jijini Dar es Salaam jana, aliyojishindia kutoka katika mchezo wa Tatu Mzuka ambao umejizolea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea Jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.

JKT MGULANI YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE NA KUFANYA USAFI

 Mkuu wa   Kikosi  cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) namba 831 KJ Mgulani, Luteni Kanali, Zacharia Godfrey Kitani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu askari wa kikosi hicho kujitolea damu na kufanya usafi  katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote. 

Tuesday, August 29, 2017

KAMPUNI YA ITEL TANZANIA YAMWAGA VIFAA MBALIMBALI VYA MASOMO SHULE YA MSINGI UHURU ARUSHA

Meneja masoko Kanda ya kaskazini; Noel Mgasa akizngumza wakati wa utoaji vifaa vya masomo pamoja na bidhaa za mahitaji ya msingi kwa wanafunzi 76 wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Uhuru jijini Arusha.
 Kampuni ya simu za mkononi ya itel kwa kushirikiana na balozi wake Irene Uwoya, imetoa Msaada wa vifaa vya masomo pamoja na bidhaa za mahitaji ya msingi kwa wanafunzi 76 wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Uhuru jijini Arusha.

Afisa hABARI WA itel  Fernando Wolle Akizungumza katika hafla hiyo
Akikabidhi vifaa hivyo mwishoni mwa wiki balozi wa itel Irene Uwoya alisema jamii inapaswa kufahamu kuwa wapo wahitaji ambao wanataakiw kukumbukwa na jamii yao iliyowazunguka.
“Napenda kuwaasa Watanzania wenzangu kwamba kuna watu wanahitaji elimu lakini kuna vitu wanakosa vya kuwasaidia wapate hiyo elimu, suala la msingi ni kujitahidi mahali sahihi pa kupeleka msaada huo, sisi kama itel, tumeona ni vyema tuanze  kuleta hapa lshule ya Uhuru lakini tutaendeleza jitihada hizi kwasababu tunaamini elimu ndio kila kitu” Alisema Uwoya.
Balozi wa Itel Tanzania Msanii Irene Uwoya akimkabishi  Mwalimu mkuu  shule ya msingi Msingi Uhuru jijini Arusha.Zurina Rajabu msaada wa Vifaa mbalimbali
Naye  Meneja masoko wa kampuni ya itel  kanda ya Kaskazini Bwana Noel Mgasa alisema  wameamua kutoa msaada huo kutokana na shule hiyo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wenye uhitaji.
“Kimsingi tumeamua kutoa msaada huu kwa kuona umuhimu wa jitihada zinazofanywa na walimu wa shule ya msingi Uhuru na wadau wengine wanaojali umuhimu wa elimu,na sisi tumeanzia Arusha lakini tutafika mpaka mikoa mingine” Alieleza Mgasa.

Kwa upande wake Afisa habari wa kampuni ya itel  Fernando Wolle alisema wametoa msaada huo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya kampuni ya itel na jamii nzima ya Kitanzania.
“Hatuwezi tukajisifu kwamba ni sisi tuliotoa msaada huu, msaada huu unatokana na kuaminiana kati ya itel na Watanzania, kwa kifupi ni kwamba kama ulishawahi kununua simu ya itel basi wewe ndiye uliyewezesha, naomba tu Watanzania endeleeni kutumia simu zetu na kwa sasa tunayo itel S31, ukinunua basi unaunga mkono jitihada hizi” Alisema Wolle.
Akieleza kuhusu msaada huo Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Uhuru Zurina Rajabu alisema kampuni ya itel haijakosea kutoa msaada huo katika shule yake kutokana na uhitaji walionao.
“Tuna jumla ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili 76, kwahiyo itel hamjakosea kabisa kuja hapa Uhuru kutoa msaada huu, hawa watoto ni binadamu kama walivyo wengine, na wengine tunawafundisha mpaka wanakuwa kawaida na wangine waliomaliza wana maisha mazuri tu kwahiyo tunaomba ushirikiano zaidi” Alisema Rajabu.


Shule ya msingi Uhuru ilianzishwa mwaka 1946 na mpaka sasa ina wanfunzi zaidi 1500 na kati yao wanafunzi 76 wana ulemavu wa akili.

PICHA ZOTE ZA HAFLA HIYO ZIPO HAPA---