Wednesday, December 3, 2014

HABARI NJEMA KWA VIJANA WOTE WA CCM TANZANIA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiWaFwbo12uNipQs5a1g0b26G6uTWkMZ9MooXD0Mw8UBbTHdNB2_9Le77IRGghhWbMjElTfrAezVwOPNnrODJ4ySVBa6am_k_dvIpkryGxKKXYgnlREtKV5QRVudZDRVx2mcINPF-9v2LE/s1600/MMGM1359.jpg
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Mboni Mhita (kushoto) akipokea Kadi Maalum ya pongezi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya UVCCM,Zainab Katimba.
 Makamu Mwenyekiti wa UVCCM achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Afrika Kanda ya Afrika Mashariki
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgRONcG28i_GuP2vbKn-93SEiWzWFLC3BWEymYXAwwRT3ax6tbIZeq5XKAUHanDugWtK51VKtFTZoHO-wIcdN5xTrvhDUj39qIlM9-OI43PZVf2PQp3ViIbHqcAwjepfH56MvAhntZ43Ms/s1600/MMGM1318.jpg
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Mboni Mhita (katikati) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) pamoja na baadhi ya vijana wa Mkoa wa Dar es salaam leo,juu ushindi wake alioupata katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Barani Afrika,ambapo yeye amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja huo kwa upande wa Afrika Mashariki.Uchaguzi huo ulifanyika Mwishoni mwa mwezi uliopita katika Jiji la Johannesburg,nchini Afrika Kusini.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg5Y3FYEJRJcRt5-AMObcwzJ540fPOKhVJJkkM-L8DfSNqdazP9jk1ryRDvnvQP1jjRTMB4MykbKaBlM7u8fKkrAugM0o7JsHl6I5qoCwHUEQItPqPAx1fXR88u-zj-j8kuqevEvp5J6fM/s1600/MMGM1313.jpgKushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCC - Bara,Mfaume Kizigo na Kulia ni Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya UVCCM,Zainab Katimba

HABARI HII KUTOKA DAR ES SALAAM LEO HUTAKIWI KUIKOSA


Maandamo ya Wanafuzni Pamoja na Wanaharakati wakipinga unyanyasaji wa Kijinsia wakiwasili makao makuu ya TGNP Jijini Dar es Salaam picha na Suleiman Magari
 Na Karoli Vinsent
         WITO umetolewa kwa Jamii kupinga vikali Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake, Vijana  pamoja na watu wenye ulemavu ili kuikomboa Jamii kutoka kwenye Vitendo hivyo.
     
Rai hiyo imetolewa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  Bi Lilian Liundi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Wiki ya kupinga Vitendo vya Ujangili iliyoanza mwezi Novemba 25 mwaka huu ambapo Be Liundi alisema kwa sasa jamii inachangamoto kubwa sana kuhusu vitendo vya  ukatili wa Kijinsia ambayo inaifanya jamii kuishi katika hofu kubwa hususani wakina wanawake na vijana pamoja na watu wenye Ulemavu .

ESCROW INAENDELEA--SETHI WA IPTL APIGA MKWARA MZITO JUU YA MITAMBO KUTAIFISHWA



Wakati masikio ya Watanzania yakiwa yameelekezwa Ikulu kusikia maamuzi ya Rais Jakaya Kikwete juu ya
maazimio manane yaliyotolewa na Bunge kuhusu sakata la uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunt
ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi, ameibuka na kudai kuwa anamuachia Mungu yote yaliyotokea.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwa simu katika mahojiano maalum na NIPASHE kuhusu mambo yaliyojitokeza katika mkutano wa16 na 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wakati wabunge walipokuwa wakijadili kashafa ya uchotaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

OPERATION DELETE CCM INAENDELEA,PICHA ZIKO HAPA

unnamed
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kisumba, Jimbo la Kalambo, mkoani Rukwa, katika mfululizo wa mikutano ya ziara ya Operesheni Delete CCM katika vijiji vya mkoa huo.
unnamed1
Naibu akikumbatiana na mzee ambaye alikuwa mmoja wa wasikilizaji kwenye mkutano wa Operesheni Delete CCM uliofanyika katika Kijiji cha Samazi, mkoani Rukwa. Mzee huyo ambaye alitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba, alisema kuwa aliguswa sana na maneno ya Mwalimu.
unnamed2
Naibu Katibu Mkuu akiagana na wananchi wa kijiji cha Kisumba baada ya mkutano huo wa hadhara kijijini hapo.
unnamed3
Naibu Katibu mkuu na msafara wake wakishiriki chakula walichoandaliwa na wenyeji wao katika Kijiji cha Samazi Jimbo la Kalambo, baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ikiwa ni mwendelezo wa mikutano mfululizo wa Operesheni Delete CCM mkoani Rukwa

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI AFUNGUA MAONESHO YA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA YANAYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA BANANA LEO ASUBUHI

unnamed1Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) Bw. Charles Chacha akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama wa anga Tanzania na namna Tanzania ilivyofanikiwa kupunguza idadi ya ajali za ndege.

BENKI YA NBC YATOA MISAADA KWA WAGONJWA WALIOLAZWA MUHIMBILI

Mdhibiti  Uhalifu wa Kifedha wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Thomas Mgonja (kushoto) akikabidhi msaada wa sabuni kwa Enesi Sanga ambaye mtoto wake amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wafanyakazi wa idara ya udhibiti wa uhalifu wa kifedha ya benki hiyo walikwenda hospitalini hapo jijini Dar es Salaam jana kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwa ni sehemu ya mpango wa NBC wa kuhudumia na kurudisha sehemu ya faida waipatayo katika shughuli za kijamii.
Mdhibiti  Uhalifu wa Kifedha wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Thomas Mgonja (kushoto) akikabidhi msaada wa sabuni kwa Flora Mgawa ambaye mtoto wake amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wafanyakazi wa idara ya udhibiti wa uhalifu wa kifedha ya benki hiyo walikwenda hospitalini hapo jijini Dar es Salaam kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwa ni sehemu ya mpango wa NBC wa kuhudumia na kurudisha sehemu ya faida waipatayo katika shughuli za kijamii.

Tuesday, December 2, 2014

WAFAHAMU KWA SURA ZAO NA SIFA ZAO WABUNGE WALIOSIMAMA KUWATETEA WATUHUMIWA WA ESCROW BUNGENI

                                  Huyu  ni   Amina   kisangi 

Huyu ni miongoni mwa wabunge waliochangia hoja ya ESCROW alhamisi jioni. Kwanza alijisahau kama pale alikuwa bungeni na kuishia kutoa mipasho inayoonyesha dhahiri kuwa alikuwa amelewa pombe!


Hata pale alipopewa taarifa na Deo Filikunjombe alisema haipokei na kuishia kusema eti Deo na wenzake wa PAC wachunguzwe kama wanafaa kuwepo CCM na kuwa kamati ya PAC ni UKAWA.


Baadhi ya maneno yake namnukuu "Mheshimiwa mwenyekiti, hawa watu wa PAC wachunguzwe kama ni wana CCM kweli.Hii ripoti ya PAC inaonyesha kuwa PAC ni UKAWA. Hizo pesa za ESCROW ni za IPTL wakila au wakigawa nyie inawauma nini?"


Huyu  ni   ASUMPTA  Mshana  ni  kati ya  wabunge  waliongoza  kwa  kuongea  mambo  ya  siyo  ya  msingi  ndani  wakati  wa   mjadala  wa   EScrow  yeye  bila  aibu  alisimama  na  kuwatetea  wezi  wa  Escrow  lakini  cha  kusikitisha  jimbo  analoongoza  la  NKENGE  huko  mkoani  kagera   ni    jimbo  ambalo  linakabiliwa  na  umasikini  mkubwa  sana  tena  wa  kutisha  lakini  yeye  bila  mshipa  wa aibu  anasimama  na  kuwatetea  watumiwa  waliyochota  mabilion   ya  fedha.wabunge  kama  hawa   ni  mizingo   mitupu  isiyokuwa  na
 faida  kwa  wananchi !!!!  wakati  wananchi  wake  wanakunywa  maji    machafu   huko  jimboni  kwake  yeye  yupo  bungeni  anatetea  wezi  kwa  nguvu  zote
  Anaitwa Mhe  Simbachawene  huyu   mbunge  alikuwa  anawtetea  watuhumia   kwa  kutumia akili  sana  na   wakati mwingine  kujenga hoja  ili watuhumiwa  waweze  kupenya  mfano  alikuwa  yupo   mstari  mbele  kupendekeza  maazimio  dhaifu  ambayo  yasinge  toa  adhabu  kali  kwa watuhumiwa  hao  wa  ESCROW  ,Tunaweza  kusema  kuwa  ametumia fani yake  ya  sheria  kutetea  wezi  wakati  wa  mjadala  wa  Escrow  ndani  ya  bunge

LHRC WATAKA KAULI YA SPIKA MAKINDA ISIPUUZWE,NI ILE YA WABUNGWE KUHONGWA ILI KUITETEA ESCROW,STORY NZIMA IKO HAPA


 Mkurugenzi  wa utetezi na maboresho ya sera wa  LHRC HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam juu ya sakata hilo

Baada ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ANNA MAKINDA juzi wakati akifunga bunge kutoa kauli kuwa kuna baadhi ya wabunge waliopitishiwa  fedha wakati wa mdadala wa sakata la ESCROW kwa lengo la kusema uongo na kutetea wizi huo kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wameibuka na kusema kauli hiyo sio ya kupuuzwa ni ya kuchunguzwa na kufahamu ukweli uko wapi.


Hoja hiyo imeibuliwa leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini dar es salaam ambapo mkurugenzi wa wa utetezi na maboresho ya sera wa LHRC amesema kuwa hoja hizi kuwa kuna baadhi ya wabubge sio wasafi ni hoja nzito na hazifai kupuuzwa na kupitwa hivi hivi hivyo kituo chao kinazitaka mamlaka zinazohusika kuanza uchunguzi mara moja kujua kama kuna wabunge waliofanya kitendo hicho na wakipatikana waunganishwe katika sakata la ESCROW kwani nao ni wezi mali za watanzania.

 Mkurugenzi  wa utetezi na Maboresho ya Sera wa  LHRC HAROLD SUNGUSIA katikati,kulia kwake ni HAMIS MKINDI ambaye ni Afisa Program dawati la uangalizi wa Bunge na uchaguzi huku kushoto akiwa ni afisa programu dawati la uangalizi na serikali HUSSEN SENGU wote kutoka LHRC wakizungumza na wahabari leo jijini Dar es salaam

Aidha kituo hicho kimelitaka bunge kuichukulia kwa uzito wa aina yake kauli hiyo ya spika ili kama kuna baadhi ya wabunge waliochukua pesa ili kutetea wezi wa pesa za escrow wawachukulie hatua za kinidhamu wabunge hao.

Mbali na kauli aliyoitoa spika MAKINDA vile vile mbunge wa sikonge mh SAID MKUMBA akichangia katika mjadala ule pia alisikika akisema kuwa “Nasikia kuna watu wanapita pita wakigawa fedha mbona kwangu hawapiti”kauli ambayo inawapa wasiwasi wananchi kuwa kuna baadhi ya vitendo vya rushwa ndani ya bunge ili kuwaficha waovu ndani ya bunge.
Katika mjadala uliomalizika wiki jana ulishuhudia baadhi ya wabunge wakibishana kwa maneno huku wengine wakijaribu kutetea kile ambacho kinaitwa ni wizi wa wazi wa hela za account ya tegeta ESCROW huku wengine wakitaka wahusika wawajibishwe.

Katika hatua nyingine LHRC wameipongeza kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali chini ya mwenyekiti wake mh ZITTO KABWE kwa kazi nzuri waliyoifanya hadi hapa walipofikia nikazi kubwa na wanapaswa kupongezwa kwa kuwafichuo watu wanaotafuna mali za watanzania.

MIAKA MIWILI YA FASTJET TANZANIA HAYA NDIO MAFANIKIO YAKE


Kampuni ya ndege ya fastjet, ambayo ni Kampuni yenye gharama nafuu kote Afrika, imeadhimisha miaka miwili ya kutoa usafiri wa anga barani Africa.

Fastjet ilianza biashara ya usafiri wa anga hapa Tanzania tarehe 29 Novemba 2012, ikifanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro na Mwanza kupitia ndege yake aina ya A319.

Tangu wakati huo, Fastjet imepanua wigo wa mtandao wake nchini Tanzania pamoja na kuanzishwa kwa njia yake ya tatu kwenda  Mbeya. Kwa sasa safari za Kimataifa za ndege hii ni pamoja na safari ya  Dar es Salaam kwenda Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Lusaka nchini Zambia, Harare nchini Zimbabwe na Entebbe nchini Uganda.

Hadi sasa, ndege imeshasafirisha zaidi ya abiria 870,000 katika safari zake 8,200 ilizofanya zenye umbali wa takribani kilomita milioni 6.5 – ambapo utendaji wake kwa ujumla umevutia kwa asilimia 90 kwa mwaka 2014 kwa kuwa usafiri wenye uhakika na wa kuzingatia muda. Kampuni imejijengea kuwa ni ya uhakika, kuaminika na ya usafiri wenye gharama nafuu.

TAARIFA MBILI MUHIMU TOKA TFF LEO


MIKOA MITANO YATAKIWA KUWASILISHA USAJILI COPA 2014
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitaka mikoa mitano kuwasilisha usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2014 kabla ya Desemba 5 mwaka huu.

Mikoa hiyo ambayo haijawasilisha usajili wake hadi sasa kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza Desemba 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni Arusha, Dodoma, Katavi, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Mjini Magharibi na Simiyu.

Kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya michuano hiyo, mkoa ambao hautawasilisha usajili wake kwa ajili ya uhakiki wa umri wa wachezaji utakaonza Desemba 10 mwaka huu utaondolewa katika fainali hizo zitakazomalizika Desemba 20 mwaka huu.

Wachezaji watakaobainika kuzidi umri hawataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 15. Kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya michuano kuhusu idadi ya wachezaji, kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 20 na wasiopungua 16.

Hivyo, kila timu inatakiwa kuhakikisha inakuwa na idadi hiyo ya wachezaji, kwani kikanuni wakipungua 16 itaondolewa kwenye mashindano.

Timu 16 kwa upande wa wavulana zitashiriki katika fainali hizo wakati kwa upande wa wasichana ni timu nane. Mikoa iliyoingiza timu za wasichana kwenye fainali hizo ni Arusha, Dodoma, Ilala, Kinondoni, Mbeya, Mwanza, Temeke na Zanzibar.

Monday, December 1, 2014

USIPITWE NA PICHA HIZI KUTOKA CHADEMA LEO

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Muze, Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa, katika mfululizo wa mikutano ya ziara ya Operesheni Delete CCM

KUTOKA TFF LEO--TAIFA STARS MABORESHO YAINGIA KAMBINI

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kimeingia kambini leo (Desemba 1 mwaka huu) Bulyanhulu mkoani Shinyanga kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij, Stars Maboresho itapiga kambi mkoani humo hadi Desemba 6 mwaka huu ambapo itarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa.

HIVI NDIVYO TIGO WELCOME PACK ILIOVYOWAPAGAWISHA WAKAZI WA KIGOMA

Msanii wa kundi la Origional Comedy Emanuel Mgaya (Masanja) akiburudisha kwenye tamasha la Tigo welcome pack lililofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Msanii wa Bongo Flava Sunday Mjeda (Linex) akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo welcome pack lililofanyika uwanja wa lake Tanganyika mjini Kigoma.
Msanii Alex Chalamila maarufu kama MCRegan akiburudisha katika tamasha la kuhamasisha matumizi ya mtandao wa simu ya mkononi ya Tigo lililofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Msanii nguli wa hiphop nchini Joseph Haule a.k.a Prof J akitumbuiza kwenye tamasha la Tigo welcome pack huku akisindikizwa na wasanii wa kundi la Origional Comedy kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.