Wakazi
wa Mtaa wa Migombani, Uliopo Katika kata ya Segerea Manispaa ya Ilala
Jijini Dar Es Salaam wakiwa wamelizunguka gari la Afisa Mtendaji wa Kata
ya Segerea aliyefika majira ya saa tisa kamili mchana huu na kutangaza
kusitisha uchaguzi wa serikali ya mitaa kimya kimya.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Segerea (katikati mwenye shati la draft) akiwa
kawekwa mtukati mara baada ya kuja na kutaka kusitisha uchaguzi bila
sababu ya msingi. waliomzunguka ni wakazi wa mtaa wa segerea wakimuhoji
afisa mtendaji huyo sababu ya kutaka kusitisha uchaguzi huo wakati
hakukuwa na vurugu wala kero ya aina yoyote iliyojitokeza katika kituo
cha kupigia kura cha Migombani.
Wakazi wa Mtaa wa migombani wakumzuia afisa mtendaji kuondoka hadi pale atakapotangaza tena kuwa uchaguzi unaendelea
Msimamizi
wa Uchaguzi wa serikali ya Mtaa wa Migombani katika Kituo cha uchaguzi
wa Migomabni akielezea sababu za kusimamisha uchaguzi huo kwa muda
kutokana na kusubilia barua ya kumtaka kuendelea na uchaguzi kutoka kwa
afisa mtendaji wa Kata ya Segerea aliyetaka kujaribu kusitisha Uchaguzi
huo kwa kisingizio cha Kutumwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Segerea, Akiandika barua ya kutamka kuwa uchaguzi
unaendelea mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kutaka afisa huyo
kueleza sababu za msingi za kutaka kujaribu kusitisha uchaguzi
huo.Pembeni ni wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishuhudia kuwa afisa
mtendaji huyo anaandika ipasavyo hiyo barua.
Hii
ndio barua aliyokuwa akiandika afisa mtendaji wa kata ya segerea
inavyosomeka ambapo baadae alienda nayo ofisi kwa kuongozana na wakazi
wa migombani kwaajili ya kugonga muhuri wa kata kuthibitisha kuwa
uchaguzi unaendelea
Afisa
mtendaji wa Kata ya Segerea (Mwenye shati la drafti) akiongea na wakazi
wa mtaa wa migombani mara baada ya vurugu kutaka kutokea mara baada ya
afisa mtendaji wa kata ya segerea kujaribu kusitisha uchaguzi bila
sababu za msingi
Wakazi
wa Mtaa wa migombani, Kata ya Segerea wakimzuia Afisa mtendaji huyo
kuondoka mpaka atangaze tena kuwa uchaguzi unaendelea.