Monday, March 6, 2017

WABUNGE WATATU WAPAMBA KONGAMANO LA MUZIKI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mbunge na Katibu Mkuu  Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Amina Nassoro Makulagi (kulia), akizungumza katika Kongamano la Siku moja la wadau wa muziki nchini lililoandaliwa na Tanzania Music Foundation (TMF) na kufanyika Ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo  na Rais wa TMF, Dk.Donald Kissanga.
 Mbunge, Halima Bulembo, akizungumza kwenye kongamano hilo.
 Mbunge, Kiteto Zawadi Koshuma akichangia jambo kwenye kongamano hilo.

Wavuvi wa Kijiji cha Nungwi Wanalalamikia Uvuvi Haramu Katika Bahari Yao na Kwenda Maeneo ya Mbali Kuvua.

Mwananchi Mvuvi swa Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya makampuni katika ukanda wao wa bahari ya nungwi kwa kutumia bunduki na mishare wakati wa uvuvi wao na kuwakimbiza samaki katika maeneo hayo na wao inawalazimu kwenda kuvua seheme ya mbali na eneo hilo kutokana na samaki kukimbilia maeneo mengine, wameitaka taasisi husika kulichunguza hili. ili mkuepusha uvuvi huo haramu katika pwani yao.

HATUTAKUBALI TLS KUJIINGIZA KATIKA SIASA-MWAKYEMBE


Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt Harrisson Mwakyembe amesema Serikali haiwezi kuona Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinajiingiza katika siasa na kama TLS wanataka hivyo, basi Serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha Wanasheria.

Picha - ASKARI POLISI WAKIWAKABILI WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI BARIADI WALIOANDAMANA KATIKATI YA BARABARA

Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maandamano ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko Bariadi mkoani Simiyu-Picha zote kwa hisani ya Simiyu News blog

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi iliyoko Bariadi mkoani Simiyu wakiandamana katikati ya barabara kuu ya Bariadi-Lamadi, mjini Bariadi wakishinikiza kurudishwa Mkuu wa shule yao ambaye alikuwa amepewa uhamisho Deus Toga, ambapo alikuwa amepelekwa shule ya sekondari Giriku na kuletewa Mkuu wa shule mwingine Paul Lutema ambaye walimkataa.

Sunday, March 5, 2017

BAWACHA WATOA MSAADA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD


Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) jana wametoa msaada wenye thamani ya Sh 900,000 katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ikiwa ni katika maadhimisho ya wiki ya Wanawake Duniani.
Akikabidhi msaada huo leo, Mbunge wa Vitu Maalum Chadema Suzan Lyimo amesema msaada huo ni pamoja na kifaa cha kuwekea nguo za wagonjwa chenye thamani ya Sh 600,000.
Picha na Vicent Macha

KONGAMANO LA WANAWAKE LA ACT WAZALENDO LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM


 Chama cha ACT wazalendo kupitia ngome ya wanawake act wazalendo wamefanya kongamano kubwa la kitaifa lililofanyika Jijini Dar es salaam ikiwa ni moja na shughuli ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.

Kongamano hilo lililohuduriwa na mgeni rasmi Esta Joel Kyamba ambae ni katibu ngome ya wanwake ACT Wazalendo liliweza kuwakutanisha wanawake toka sehemu mbalimbali lengo likiwa ni kujiandaa kuadhimisha cku ya wanawake duniani ambayo kilele chake kitafikiwa tarehe 8 ya mwezi huu wa tatu.
PICHA NA VICENT MACHA

Kongamano limewaweka pamoja wadau mbalimbali toka sehemu mbalimbali kama mwakilishi wa NSSF na daktari wa magonjwa ya kansa wanawake wajasilia mali pamoja wanawake wenye ulemavu kuweza kuwatia moyo na kuweza kuongea nao kuhusiana na changamoto wanazokutana nazo na jinsi wanavyoweza kuzikabiri.

SOPHIA SIMBA ATANGAZA KUNG'ATUKA UENYEKITI UWT

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na  wanawake wa umoja huo wakati wa maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es salaam.

“Mimi Sophia Simba, nimeamua kutogombea kwa hiari yangu mwenyewe nimeamua kutogombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wanawake Taifa UWT katika uchaguzi ujao,”amesema Sophia Simba.

Sophia Simba ametaja sababu zilizomfanya asigombee kuwa ni azma yake ya kuutumikia umoja huo kwa muda wa vipindi viwili tu na si zaidi ya hapo.

Aidha, amesema kuwa akiwa ndani ya UWT amebahatika kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwa sababu alianzia nafasi ya ukatibu wa tawi la Kaskazini NDC.

Hata hivyo amesema kuwa anamshukuru mungu kwa kumjalia kushika nafasi mbalimbali kwa kuwa amekuwa mbunge kwa muda wa miaka 22
PICHA NA VICENT MACHA

WEMA SEPETU AMTEMBELEA MBUNGE GODBLESS LEMA


Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye hivi sasa amehamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametimiza hadi yake kwenda kuonana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema ambaye amepata dhamana siku ya Ijumaa na kutoka gerezani.


Wema Sepetu juzi alisema atakwenda Arusha kuonana na Mbunge huyo ambaye amekaa ndani kwa zaidi ya miezi mitatu na kusema ni faraja kwao saizi kuona ametoka na kuja kuendeleza mapambano


"Ni faraja kwetu kwamba sasa umerudi mtaani kuendeleza mapambano, kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe, mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke. For that sake, kesho (jana) i'll be in Arusha kuonyesha Solidarity" alisema Wema Sepetu


Baada ya Wema Sepetu kufanikiwa kuonana na Mbunge wa Arusha Gobless Lema amefunguka na kusema saizi anajisikia furaha na amani kuwa ndani ya chama hicho
"Finally Met my brother, aisee Chadema inanipa furaha mimi. Nina amani ya moyo... Ona Venye nacheka .... It was A Good Day...."aliandika Wema Sepetu

NECTA YAENDELEA KUWATANGAZIA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOTUMIA VYETI VYA WATU WENGINE



Na Eleuteri Mangi, MAELEZO
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.

MAKONDA ASHIRIKI IBADA KATIKA KANISA LA KKKT KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM

SeeBait

Viongozi wa dini pamoja na waumini wa Dini ya Kiristo jijini Dar es Salaam wametakiwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuwaukoa vijana katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya hapa nchini. 

Saturday, March 4, 2017

CDEA yaendesha mafunzo ya IIDEA 2017 kwa wabunifu mavazi na urembo wa Afrika Mashariki

CDEA yaendesha mafunzo ya IIDEA 2017 kwa wabunifu mavazi na urembo wa Afrika Mashariki Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye sekta za ubunifu na biashara IIDEA 2017,mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development East Africa -CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ tawi la Afrika Mashariki. 

Awali akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza washiriki kwa kuchaguliwa kwenye mradi huo ambao ni wa kwanza na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao kuzingatia yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko nje ya mipaka ya nchi zao wanazotoka. 

Mafunzo hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria na mbinu tofauti za kupata ufadhili. Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo Bibi Santa Anzo na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika. 

Washiriki hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja na kujitengenezea majinna (branding). Mafunzo hayo ya siku nne, yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba ya hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na simbi ambazo zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi zao hizo. Kwa upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo. 

Mradi huo pia unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) unaratibiwa na CDEA kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la kukuza ujuzi na elimu ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda. Kwa sasa mafunzo hayo ya Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) yameanza na masuala ya ubunifu wa mavazi na urembo ambapo pia yatafuatiwa na mafunzo mengine ikiwemo Muziki na filamu. Tazama hapa matukio mbalimbali ya picha ya mafunzo hayo:
Washiriki ambao ni wabunifu kutoka Afrika Mashariki akiwemo Andrew Kalema, Joyce Gerald (katikati) na Makeke Jocktan wakifuatilia mafunzo hayo
Washiriki na wataalamu wakibadilisha mawazo wakati wa semina magunzo hayo

MZEE ALINANOSWE ANAWATAFUTA NDUGU ZAKE WALIOPOTEZANA MIAKA KUMI ILIYOPITA

 Mzee Alinanoswe Aspain Mwambapa mzaliwa wa Tukuyu Mbeya anawatafuta ndugu zake wakiwemo kaka zake na dada zake  baada ya kupotezana nao kwa Zaidi ya miaka Kumi iliyopita.

Kwa mujibu wa Mzee huyo ameuomba mtandao huu kumsaidia kuwatafuta dada zake ambao ni Eni Aspain Mwambapa anayeishi Dar es salaam,pamoja na Buni Aspain Mwambapa Mkazi wa songea kwa sasa.
Wengine ambao mzee Alinanoswe anawatafuta ni kaka zake Ismail Aspain mwambapa Pamoja na Obole Aspain Mwambapa ambao wote walipotezana Takribani miaka Kumi iliyopita.
 
Mzee huyo ameueleza mtandao huo kuwa alitengana na ndugu zake hao mwaka 2001 Chunya mbeya na kutimkia Pwani ambapo mpaka sasa anaishi huko,ambapo sasa anatamani kurejea nyumbani kwake lakini hajui jinsi gani ya kuwapata ndugu zake na sasa anaishi kwa wasamaria wema walioamua kumhifadhi.

Mzee huyo alizaliwa mwaka 1961 Tukuyu mbeya.
Kwa mweye kumjua mzee huyu atoe Taarifa kwa namba zifuatazo ili akutanishe na ndugu yake ,
Namba

0713 562954 Augustino Michael
0789682901 Lister Godfrey
0789421644 Frank Michael
0718 528632 Frank Michael
0769 56 2954 Augustino Michael.

JUKATA WAHITIMISHA MKUTANO WAO WA KATIBA


Bw. Othumani Masoud Othuman aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar akitoa maoni yake katika mkutano huo
 Na Vicent Macha

Jukwaa la katiba nchini Tanzania JUKATA jana limefikiia kilele cha mkutano wake mkuu wa katiba kwa kuweza kuwaalika wadau mbalimbali akiwemo Bw. Othumani Masoud Othuman akielezea kero na changamoto zilizopo kwenye katiba kwa upande wa tanzania visiwani. 

Pamoja na prof. bertha o.koda yeye akielezea kuhusu mchango wa wanawake katika kukwamua mchakato wa katiba mpya ya tanzania bara mkutano huo uliodumu kwa muda wa siku mbili uliodumu kwa muda wa siku mbili uliweza kufanyika Land Mark Hotel jijini Dar es salaam.
Deus Kibamba Mwenyekiti wa Jukata akitoa mada
Bw. Othumani Masoud Othumani yeye alijikita zaidi kwenye muungano na kusema kuwa muungano huu haupo sawa kwa maana katiba inaibeba sana tanganyika kuliko zanziba akatolea mfano kwamba jambo linapokuwa ni la kuhusu zanzibar linakwenda kujadiliwa bungeni na wabunge wangi wakipinga basi linatupiliwa mbali kwa kuwa baraza la wawakilishi waliopo bungeni haliwezi kushindana na wabunge wa bara kwa kuwa wao ni wengi na watashinda tu.