Tuesday, August 26, 2014

VITA YA TANZANIA KWANZA NA UKAWA SASA NI KUCHAFUANA TU,SOMA TUHUMA HIZI TANZANIA KWAZA WALIZOTUPA KWA MBOWE NA SLAA MUDA HUU

Pichani ni mwenyekiti wa kamati ya tanzania kwanza nje ya bunge ndugu AUGUSTINO MATEFU akizungumza na wanahabari muda mfupi uliopita        

        Katika kile kinachoonekana ni kuanza kuchafuana kwa wanasisasa badala ya kutafuta mwafaka wa kuwapatia watanzania katiba mpya Mwenyekiti wa kamati ya Tanzania kwanza nje ya bunge AUGUSTINO MATEFU ameibuka mbele ya wanahabari muda huu jijini Dar es salaam na kutoa tuhuma kali  juu  viongozi wanaoongoza umoja wa katiba Tanzania UKAWA kuwa wana msaada wa kifedha kutoka katika mataifa ya ulaya yanayowasaidia katika kuhakikisha kuwa Mchakato wa katiba haufanikiwi.

PICHA ZA DIMARIA AKIWASILI MAN U USIKU HIZI HAPA


Amenaswa: Di Maria akiwa kiri nyuma kushoto kwenye gari kuelekea viwanja vya mazoezi vya United

KIUNGO Angel di Maria amewasili viwanja vya mazoezi vya Manchester United, Carrington kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa Pauni 60 kutoka Real Madrid ya Hispania.
Nyota huyo wa Argentina aliyeng'ara kwenye Kombe a Dunia amewasili England huku viongozi wa Old Trafford wakiendelea na mazungumzo na Real Madrid juu ya kukamilisha uhamisho wa dau la rekodi Uingereza.

Di Maria, mwenye umri wa miaka 26, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake usiku huu ambao utamfanya alipwe Pauni 200,000 kwa wiki kwa zaidi ya miaka mitano, mshahara ambao pia utamfanya awe mchezaji wa pili kulipwa zaidi katika klabu hiyo baada ya Nahodha, Wayne Rooney. On the look out: Di Maria peers out of his United car as he arrives for the completion of his trasfer


Uhamisho wote utaigharimu United zaidi ya Pauni Milioni 90 na mchezaji huyo ataingia moja kwa moja katika kikosi kilichojeruhiwa cha Louis van Gaal kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu iliyopanda Ligi Kuu, Burnley.  

Monday, August 25, 2014

STORY KUHUSU SAID KUBENEA KULIPELEKA BUNGE LA KATIBA MAHAKAMANI IKO HAPA

Karoli Vinsent na Mwanahalisi Forum

    MWANDISHI mwandamizi wa Habari nchini  Saed Kubenea ameamua kuwa Mzalendo na Nchi yake Baada ya Kufungua kesi Mahakamani kwa lengo la Kuzuia Bunge la Katiba lisiiendelee haya ndio aliyasema mwenyewe Kubenea kuhusu hilo 

“Kwa muda wa siku tatu mfululizo sasa, kumekuwa na mjadala hapa MF kuhusu mimi kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Niseme wazi kwamba ni kweli nimefungua kesi hiyo; tayari kesi hiyo imepewa Na. 28/ 2014.

         Katika kesi hiyo, pamoja na mengine, nimeomba mahakama itoe tafsri sahihi juu ya mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba, chini ya vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011.

WAKONGWE WA REAL MADRID WALIVYOKWEA MLIMA KILIMANJARO

1
Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
2
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza mara baada ya kuwasili kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
3
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akigawa fulana maalum zenye nembo ya TANAPA na Real Madrid kwa mmoja wa wachezaji kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
4
Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Erastus Lufungulo akitoa neno la ukaribisho kwa wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid walipowasili kwa ziara fupi. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Elinas Palangyo, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bi. Devota Mdachi, Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete na Afisa Utalii Antipas Mgungusi.
5
Wachezaji wastaafu wa Klabu ya Real Madrid pamoja na wenzi wao wakiwa Hifadhi ya Kilimanjaro.
6
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete (mwenye fulana nyeupe na miwani) akiongoza msafara wa wakongwe wa Real Madrid kukwea Mlima Kilimanjaro
7
Wakongwe wa Real Madrid wakiwa katikati ya msitu wa Mlima Kilimanjaro
8
Eneo la Maporomoko ya Maji ambapo wachezaji wakongwe wa Real Madrid walifanikiwa kufika Mlimani Kilimanjaro.
10
Wachezaji wakongwe wa Klabu ya Real Madrid wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA mara baada ya kumaliza zoezi la matembezi mafupi ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

BREAKING NEWZ--WANAJESHI WANNE WA NEPAL WAKAMATWA NCHINI MUDA HUU BILA KIBALI,YUMO PIA KOMANDO WAO,CHEKI PICHA ZAO HAPA

Wanajeshi hao wa jeshi la nchi ya NEPAL wakiwa wanaonyesha vyeti vyao vya uanajeshi wa jeshi hili
        Idara ya uhamiaji Jijini Dare s salaam imewakamata raia 12 wa kigeni waliokuja nchi kinyume na sheria wakiwemo wanajeshi wanne wa  jeshi la NEPAL pamoja na nane kutoka nchini india walioletwa nchini kinyume na sheria kwa kisingizio cha maisha magumu nchini kwao.
  
     Raia  hao wamekamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya ESCOT iliyoko kijitonyama jijini Dar es salaam katika operation maalum iliyoendeshwa na idara ya uhamiaji Jijini baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo juu ya uwepo wa watu hao ambao waliwatilia mashaka.

Afisa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam GRACE HOKORORO akizungumza na mtandao huu kuhusu sakata hilo
         Wanajeshi hao wanne wa jeshi la NEPAL yumo pia komando mmoja wa jeshi hilo ambao nao wamedai kuletwa nchini kwa ajili ya kutafutiwa ajira ya maswala ya ulinzi katika nchi za Africa hivyo wakashukia Tanzania kama kituo kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.
        Akizungumza na mtandao huu muda mfupi uliopita afisa wa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam GRACE HOKORORO amesema  kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakipita katika nchi ya Tanzania na kupelekea nchi nyingine kama Africa ya kusini  kwa ajili ya kufanyishwa kazi zisizo halali


Picha mbili zikionyesha wanajeshi hao wakiwa katika nchi yao wakiwa wanalitumikia jeshi la nchi yao kabla ya kutimka na kuja nchini
      Aidha amesema kuwa watu hao wamekuwa wakiletwa na mawakala ambao wamekuwa wakiwatoa katika nchi zao kwa ahadi  la kuwatafutia kazi katika nchi hizi jambo ambalo amesema kuwa linatafsiriwa kama biashara ya binadamu ambapo mawakala waliowaleta watu hao hadi sasa hawajapatikana.
          
         Aidha Bi GRACE amewataka watanzania na watu wasamaria wema kuwafichia watu wanaowaficha watu kama hao kwani ni kinyume na sheria na baadae huleta madhara makubwa kama uhalifu na uuzwaji wa madawa ya kulevya.


Saturday, August 23, 2014

HILI NDILO KOMBE WALILONYAKUA REAL MADRID NDANI YA ARDHI TA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akimkabidhi Kombe Nahodha wa magwiji wa Real Madrid ya Hispania, baada ya kuwafunga magwiji wa Tanzania mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana

HIVI NDIVYO BURUDANI ILIVYOKUWA TAIFA,TANZANIA NA REAL MADRID


Reuben De La Red kushoto amefunga mabao matatu peke yake Real ikishinda 3-1 Uwanja wa Taifa
 MSHAMBULIAJI Reuben de La Red amefunga mabao matatu peke yake, magwiji wa Real Madrid wakiiangusha Tanzania Eleven 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
De la Red alimfunga bao moja Mwameja Mohamed kipindi cha kwanza na kipindi cha pil akamtungua mara mbili Manyika Peter, wakati bao pekee la Stars, Real walijifunga wenyewe kupitia kwa Roberto Rojas.
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alimkabidhi mpira De La Red baada ya mechi kabla ya kuwakabidhi Kombe Real Madird kwa ushindi huo.
Katika mchezo huo, ambao wachezaji waliingia na kutoka, Real Madird walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, De La Red akimalizia pasi ya Luis Figo.
Luis Figo akimtoka Athumani China
 Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia kwa kiungo Christian Karembeu, aliyezuia shambulizi la Tanzania na kuanzisha shambuizi zuri lililozaa matunda, akiuvuka msitu wa wachezaji wa wenyeji kwa umahiri mkubwa.
Tanzania Eleven ilisawazisha dakika ya 45 baada ya kona ya Mecky Mexime kuzua kizaa langoni mwa Real na Roberto Rojas akajifunga katika harakati za kuokoa baada ya Kali Ongala kuuparaza kwa kichwa. 
Beki wa Tanzania, Nsajigwa Shadrack kushoto akimtoka Fernando Sanz wa Real Madird


Kipindi cha pili, De la Red alifunga bao kwa pili kwa penalti dakika ya 81 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Habib Kondo kwenye eneo la hatari.
Awali ya hapo, Figo alimtoka vizuri beki Mecky Mexime na kuingia hadi kwenye eneo la hatari akiwa kwenye nafasi ya kufunga akampasia De La Red ambaye alipiga nje.
De la Red alikamilisha hat trick yake dakika ya 88 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Tanzania Eeleven. 
Wachezaji wa timu zote mbili wanatarajiwa kula chakula cha usiku na Mheshimiwa Rais Ikulu baadaye

INATISHAA--WEZI WACHOMWA KAMA MISHKAKI TABATA LIWITI LEO ASUBUHI


Pichani ni watu wanaohisiwa ni vibaka wakiwa wamechomwa moto na wananchi wenye hasira kali.
 
Picha nyingine pia ya watu wanaohisiwa ni Vibaka waliochomwa moto na wananchi wenye hasira kali 

Hizo ni picha ni za wezi ambao hufanya wizi kwa kutumia pikipiki. Inasemekana vijana hao wawili walikuwa kwenye pikipiki maarufu kama bodaboda walimnyang'anya mkoba binti mmoja leo alfajiri. 
            Watu walijitokeza na kuwakamata baada ya hapo waliwakata mikono na kuwachoma moto.
 Polisi walifika eneo la tukio na kuchukua miili ya watu hao.
 Tumeweka picha chache  kwa tahadhari nyingine zipo katika hali mbaya kiasi ambacho hatuwezi kuziweka hapo

USIPITWE NA HILI WALILOLIFANYA MANGULI WA REAL MADRID ASUBUHI YA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Meya wa manispaa ya konondoni YUSUPH MWENDA pamoja na baadhi ya wachezaji wa real madrid wakikata utepe kuashiria kuwa wamefungua rasmi duka hilo la vifaa mbalimbali vya umeme la TROPICAL CENTER lilopo jijini Dar es salaam
Ni duka kubwa la vifaa vya umeme ambalo limezinduliwa leo jijini Dar es salaam na wachezaji wa zamani wa timu maarufu duniani ya REAL MADRID duka ambalo liko maeneo ya Victoria hapa jijini .
Showroom hii ya vifaa mbalimbali vya umeme inaitwa TROPICAL CENTE imezinduliwa rasmi na meya wa kinondoni mstahiki YUSUPH MWENDA pamoja na wachezaji wa real madrid wa zamani ambao wapo hapa nchini kwa ziara yao ya kukuza utalii wa Tanzania na mahusiano mema ya timu na nchi hizi.


CRISTIAN KAREMBEU mchezaji wa zamani wa Real madrid akizungumza na kutoa shukrani zake baada ya hafla hiyo fupi iliyofanyika asubuhi ya leo jijini  dar es salaam ya kufungua rasmi duka kubwa la vifaa vya umeme la TROPICAL CCENTER jijini 
Wachezaji wa real madri wakiwasili katika uzinduzi huo leo

Friday, August 22, 2014

HABARI ILIYOTIKISA JIJI LEO--KAMISHNA KOVA AUNGURUMA AMWAGA SIMU KWA ALBINO WOTE DAR ES SALAAM,AWAAHIDI NEEMA,ANASA PIA MABILIONI FEKI-CHEKI STORY NZIMA HAPA

Kamishna wa polisi kand maalum ya dar es salaam Suleman kova akimkabidhi mwenyekiti wa chama cha albino Dar es salaam simu kwa ajili ya albino waishio jijini Dar es salaam
  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya D’Salaam limewashauri albino wanaoishi Jijini D’Salaam kuwa karibu sana na Jeshi hilo ili kurahisisha mawasiliano kati yao na Wakuu wa vituo vya Polisi vilivyo karibu na makazi yao au wanapofanyia usalama wao jijini D’Salaam.

       Pamoja na kwamba haijawahi kutoa tukio lolote dhidi ya Albino jijini D’Salaam kutokana na uhusiano uliopo lakini kwa sasa waongeze mawasiliano na Jeshi la Polisi kutokana na taarifa za uhalifu dhidi ya Albino katika baadhi ya mikoa hapa nchini.  
 Pia Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi D’Salaam SULEIMAN KOVA ameongea na Albino hao ofisini kwake na kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi kwa ujumla linaendelea na jitihada kubwa sana kupambana na maadui wa Albino ambao ni wahalifu na wengi wao wameishakamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo wengine wameishahukumiwa.  

         Albino wanatakiwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na Jeshi la Polisi hata kama hakuna tishio la aina yoyote wanalolijua katika maeneo yao ya makazi au wanapofanya shughuli zao za kikazi.

Katika kufanikisha zoezi hilo la mawasiliano ya haraka na Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Kanda Malum ya D’Salaam kwa kushirikiana na wadau kampuni ya SAPNA ELECTRONIC ametoa simu 20 kwa Albino ambao wameudhuria kikao ili iwe rahisi kwao kuwasiliana Jeshi la Polisi kwa namba 0787-668306 ambayo ipo katika chumba cha dharura katika Kikosi cha 999.  

                 Kamishna Kova anaendelea kuongea na wadau mbali mbali ili misaada zaidi ipatikane kwa walemavu wa ngozi ambao ni Albino ili waweze kupata simu za mikononi, mafuta maalum ya kupaka ngozi zao na msaada mwingine wowote ambao utafaa kwa Albino hao kupitia kwa namba 0715 – 009983 hii ni namba ya Kamishna mwenyewe ya oisi na namba nyingine ya Msaidizi wake katika suala la kuwasaidia Albino ni 0756-710179 ambayo ni ya SP. MOSES NECKEMIAH FUNDI.

          Aidha zipo jitihada za makusudi zinazofanyika kati ya Polisi Kanda Maalum ya Polisi D’Salaam na uongozi wa Mkoa na Kitaifa kwa manufaaa ya ulinzi na Usalama wa Albino wote.
        
           Hatua zingine za ziada za muda mfupi na mrefu ni uwepo wa program ya mafunzo maalum kwa Albino wa Jijini D’Salaam ili wapate mafunzo kupitia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa lengo la kupata uelewa wwa kutosha ili nao pia washiriki na kujua namna ya kutoa taarifa kwa lengo la kujikinga na maadui wao ambao wamegubikwa na tama za kujipatia mali, madaraka n.k. kwa njia za ushirikina.

 SABA WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ZA DOLA ZA KIMAREKANI WAKAMATWA
   

LIVE TOKA DAR ES SALAAM---RITA WAJA NA LENGO BORA KWA WATANZANIA,SASA NI TATHMIN YA MFUMO WA USAJILI,MATUKIO MUHIMU NCHINI-STORY KAMILI IKO HAPA

Mtendaji mkuu na Msajili Mkuu,wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Philip G,Saliboko Akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita katia ofisi za RITA jijini Dar es salaam
WAKALA wa Usajili na ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inatarajia kufanya tasmini ya mfumo wa Usajili,matukio muhimu ya Maisha na ukusanyaji wa Takwimu nchini tanzania.

 Mfumo huo ambao utatumika kuchukua taarifa muhimu za vizazi,vifo na Sababu zake,ndoa  na talaka.

 Akizungumzia Tasmini hiyo, leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi Habari Jijini ,Afisa Mtendaji mkuu na Msajili Mkuu,wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Philip G,Saliboko Alisema Tasmini hiyo itafanyika kikanda kwa siku kumi na tano (15) kuanzia tarehe 15 Semptemba hadi tarehe 30 mwaka huu na itajumuisha wadau wakubwa wa Masula ya usajili kutoka wizara ,Taasisi,Idara pamoja na Vyuo na wakala Mbalimbali za Serikali.

Waandishi wa habari mbalimbali wakiwa katika mkutano huu ambao umemalizika muda huu jijini Dar es salaam
Ambapo ameongeza kusema Tathmini itafanywa katika ofisi za Maafisa tawala wa Wilaya,Vituo vya Tiba ,Vituo vya Polisi,nyumba vya kutunzia Maiti,makanisa na kwenye Makazi ya Wananchi ambamo matuko hayo utokea.

Saliboko amewataka Watanzania kutoa ushirikiana mkubwa wakati wa Zoezi hili,kwani ndio njia pekee itakayoisaidia Serikali kufanya mipango yake kikaminifu.