Monday, June 30, 2014
breaking newzz--PICHA--NAIBU KATIBU MKUU CUF BARA ANUSURIKA KATIKA AJALI
Naibu Katibu m kuu mpya wa CUF pia Mbunge wa viti Maalum Magdalena Sakaya akimshukuru Mungu baada ya kunusurika katika ajali na Lori kwenye makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere Dar leo jumatatu ambapo ajali hiyo imetokea,magdalena sakaya amechaguliwa juzi kushika nafasi hiyo ya unaibu katinu mkuu wa CUF baada ya JULIUS MTATIZRO kutolewa katika nafasi hiyo
TCRA YAKABIDHIWA CHETI CHA UBORA NA TBS LEO
KATIKA kuonyesha ubora kwa Watanzania
mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imetakiwa kuongeza juhudi katika
kuboreshaji sekta hiyo, baada ya kukabidhiwa cheti cha kiwango cha
kimataifa na Shirika la Viwango Duniani.
Cheti hicho kilikabidhiwa jijini
Dar es Salaam leo, mbele ya wafanyakazi wote wa TCRA na Mkaguzi wa kimataifa
kutoka Uingereza Andrew Rowe na kumpa Mkurugenzi wa TCRA Prof. John Mkoma.
Akipokea cheti hicho, Profesa Nkoma,
alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika kudhibiti
mawasiliano nchini, ndio sababu iliyopelekea kupata cheti hicho kinachoipa
heshima Tanzania.
Sunday, June 29, 2014
Saturday, June 28, 2014
KAULI YA ADEN RAGE KUELEKEA UCHAGUZI WA SIMBA SC HII HAPA!
SIMBA SC inatarajia kufanya mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu Kesho Jumapili (Juni 29 mwaka huu), katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kuelekea katika mkutano huo utapata Rais mpya, makamu wa Rais na wajumbe wapya wa kamati ya utendaji kwa mujibu wa katiba mpya Simba, mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage awewatakia kila la heri wanachama wote katika uchaguzi huo.
Akizungumza na Mtandao huu mchana huu, Rage amesema ana imani uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu ili klabu ipige hatua.
KAMPENI SIMBA ZAKAMILIKA KWA AINA YAKE,WAMBURA AJITKEZA KUMPIGIA KAMPENI TUPA,AVEVA NAYE AAHIDI MAKUBWA SIMBA.PICHA ZOTE HAPA
TIGO YAWEZESHA MAFUNZO YA TECHNOHAMA KWA WASICHANA JIJINI DAR ES SALAAM
Badhi ya wasichana kutoka shule mbalimbali jijini dar es salaam wakiwa katika mafunzo hayo |
Wasichana nchini Tanzania wamepewa changamoto ya
kujiendeleza katika masomo ya technohama ili kuweza kuongeza upeo wao katika
matumizi ya computer na kuweza kuchangia katika maendeleo ya kijamii kwa ujumla
nchini Tanzania.
Changamoto hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na meneja
wa uwajibikaji kwa jamii kutoka kampuni ya tigo Tanzania Bi WOINDE SHISAEL
wakati akizungumza na wanafunzi wa kike wapatao 100 kutoka shule za secondary
mbalimbali waliokuwa katika mafunzo maalum ya technohama yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali
linalijihusisha na technohama APPS AND GIRLS ambao pia ni mmoja wa washindi wa
program maalum ya wajasiriamali wa kijamii TIGO REACH FOR CHANGE
Bi WOINDE amesema kuwa “mkakati wa huduma ya
uwajibikaji walionao tigo ni kuwezesha jamii kupitia matumizi ya vyombo vya
kidigital” ambapo ametoa rai kwa wanawake na wasichana wote kujitokeza zaidi
kujiendeleza kidigital kupitia technohama huku akiongeza kuwa ni dhana potofu
kuwa wasichana hawawezi kufanya vizuri katika technohama wakati wana nafasi
kubwa sana.
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wasichana
tu kwa sababu wanawake wengi wameonekana kuwa nyuma sana katika kujihusisha
katika technohama.
Meneja wa uwajibikaji kwa jamii kutoka kampuni ya tigo Tanzania Bi WOINDE SHISAEL |
Muasisi wa APPS AND GIRLS bi CAROLYNE EKYARISIIMA |
Naye muasisi wa APPS AND GIRLS bi CAROLYNE EKYARISIIMA ampaye pia ni mmoja wa washindi wa
dola 25,000 za kimarekani kutoka tigo reach for change kwa mwaka huu amesema
kuwa mafunzo haya yanazingatia kwapatia wasichana utaalam katika kutengeneza
tovuti kama njia moja wapo ya kuwahamasisha katika maswala ya technohama.
Shule zilizohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na
kisutu,jangwani,na kibasila ambapo mafunzo hayo ni ya simku moja.
Friday, June 27, 2014
EXCLUSIVE--HUYU NDIYE MCHEZAJI WA YANGA TOKA BRAZIL (COUNTINYO) AWASILI DAR KWA MBWEMBWE
Afisa Haari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto (kushoto) akiwa pamoja na mshambuliaji mpya Andrey Coutinho mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa JK Nyerer leo |
Kiungo mshambuliaji mpya wa timu ya Young Africans SC Andrey Marcel Ferreira Coutinho amewasili mchana wa leo jijini Dar es salaam akitokea kwao nchini Brazil tayari kabisa kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wana Wanajangwani katika msimu wa 2014/2015.
Countinho amewasili mchana kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways) akitoka jijini Sao Paul ambapo safari ya kuja Tanzania imemkchukua takribani masaa 20 tokea katika Mji wa Berem ambapo ndipo anapoishi.
Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere, Coutinho alipokelewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw. Mohamed Bhinda ambaye alimuongoza kuwasilimia washabiki na waaandishi wa habari walijitokeza kumlaki.
TIZAMA VIDEO HII--KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AWASHAMBULIA KAFULILA NA ZITTO,ASISITIZA KAFULILA NI TUMBILI TU
SAKATA linalohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), limechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuwashambulia kwa maneno makali, wabunge wawili Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi).
HABARI24 likuwapo wakati Maswi akitumia maneno makali kwa kuyarudia, akikejeli nyaraka zinazotajwa kuwa ni ushahidi wa jinsi IPTL ilivyouza hisa zake na fedha kutolewa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti maalumu ya pamoja (Escrow), akisema nyaraka hizo ni karatasi za kufungia vitumbua zinazosambazwa na wabunge hao aliowaita “washenzi”.
Kauli hiyo ya Maswi imekuja siku mbili tu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kushambuliana na Kafulila kwa maneno makali malumbano yao yakianzia ndani ya Bunge na kuendelea walipotoka, kila mmoja akiamini kauli aliyoitoa ilikuwa ni sahihi.
Werema alimfananisha Kafulila na tumbili na yeye kumuita mwanasheria huyo mwizi. Tumbili ni mnyama wa porini wakati mwizi ni mtu anayetenda uhalifu kwa kuchukua kitu au mali isiyo yako.
PATA NAFASI YA KUSOMA KAULI TANO KALI ALIZOZUNGUMZA KOCHA MPYA WA YANGA MAXIMO MBELE YA WANAHABARI LEO
Kocha MAXIMO akizungumza na wanahabari makao makuu ya timu hiyo jijini Dar es salaam |
Kocha mpya wa timu ya yanga ya dar es salaam mbarazili MARCIO MAXIMO leo amezungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza jijini dar es salaam ambapo katika mambo mengi aliyoyazungumza ameonekana kuwaahidi mambo makubwa mashabiki wa timu ta yanga.
Naomba ninukuu kauli zake tano ambazo amezitoa na zikaonekana kuwafurahisha wapenzi wa timu ya yanga na viongozi wake
1-Nimekuja kuifanya timu ya yanga kuwa kama timu ta TP MAZEMBE ya congo,nadhani nina uwezo huo na nadhani kwa kushirikiana na viongozi wa timu hii tutaweza.
2-Nataka kuipeleka yanga level za kimataifa zaidi tofauti na sasa
3-Nataka kutengeneza timu ya yanga kuwa timu yenye upinzani mkubwa tanzania na barani africa kwa ujumla
4-Nataka kuifanya yanga iwe timu yenye mvuto na ifike kipindi timu hii wazungu na wachezaji wa kutoka ulaya kuja kucheza hapa yanga na kwa kuanza hilo naanza kwa kumleta mchezaji mzuri toka Brazil anaitwa ANDERY CONTINYO ambaye atawasili leo jioni.
5-Swala la kaseja ni kwamba sina bifu na kipa wa yanga JUMA KASEJA nampenda sana yaliyopita yamepita sasa tugange yajayo tuwaze kuijenga timu yetu.
MAXIMO ATAKUWA AKIJIZOLEA KITITA CHA MILION 19 KWA MWEZI AKIWA YANGA
Thursday, June 26, 2014
MAJONZI: MWILI WA SISTA ALIYEPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI UBUNGO WAAGWA JIJINI DAR-R,I,P
PICHA ZOTE KWA UDHAMINI WA GLOBAL PUPLISHER
MICHEZO--FAIDI PICHA ZA MAXIMO ALIVYOTUA YANGA LEO--ZIKO HAPA
Kocha mpya wa timu ya yanga ya Dar es salaam leo ametua jijini dar es salaam kwa ajili ya kuanza kibarua chake cha kuinoa club hiyo ya Jangwani |
breaking newzz---TUNDU LISSU AVUNJA UKIMYA WA CHADEMA KWA MARA YA KWANZA ATOA YA MOYONI KUHUSU KINACHOENDELEA CHADEMA,APANGUA HOJA ZA WAKINA YONA--USIKOSE IPO HAPA PEKEE
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita Baada
ya watu, wanaojiita Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA,kuandamana mpaka kwenda kwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali “CAG”
pamoja na kwa Masajili wa vyama vya kisiasa nchini,kuwashtaki viongozi wa Juu
wa chama hicho kwa madai ya matumizi mabaya ya Fedha.
Nae,mwanasheria mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu,ameibuka na kuwataka wanachama wa
chama hicho kuwapuuza watu hao,kwa madai kuwa chadema iliwafukuza uanachama na sasa
hivi wanatumiwa na Viongozi wa kutoka
chama cha Mapinduzi ili kukidhofisha chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
BARAKA ZASHUKA PALESTINA HOSPITALI --FARIDA FOUNDATION YATOA MISAADA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA NA KWA WALEMAVU ENEO LA UBUNGO DARAJANI
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle akipoke Ndoo zitakazotumika kwa ajili ya kuhifadhia uchafu katika Hospitali hiyo,ambazo zilitolewa kama Msaada na Farida Foundation |
Mkurugenzi wa Farida Foundation akikabidhi moja ya msaada kwa kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle,Huku wafanyakazi wengine wa Hospitali hiyo wakishuhudia.
Bi Farida Abdul Akikabidhi bandeji kwa ajili ya kufungia wagonjwa kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle
Bi Farida Abdul akimuonyesha kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Palestina Dk Hugoline Mselle Vifaa ambavyo vimeletwa kama msaada kwenye Hospitali hiyo.Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti vya magurudumu vitatu ambavyo vitasaidia kubebea wagonjwa,Bandeji za kufungia vidonda,Ndoo za kuwekea taka,na vinginevyo.
TIGO NA HUAWEI WAFANYA MAAJABU MENGINE MUDA HUU,SASA "SMARTPHONES" BEI SAWA NA BURE,NUNUA URUDISHIWE HELA YAKO
Mkuu wa kitengo cha internent wa TIGO bw DAVID ZACHARIA akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita |
Kampuni ya mawasiliano ya TIGO Tanzania leo
imetangaza kuingia katika ushirikiano na kampuni ya technologia ya HUAWEI ili
kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo ya simu nchini kuweza kupata simu za kisasa "SMARTPHONES " kwa bei nafuu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam muda
mchache uliopita mkuu wa kitengo cha internent wa tigo bw DAVID ZACHARIA
amesema kuwa ushirikiano huo unawapa wateja fursa ya kuweza kumiliki simu aina ya
HUAWEI Y330 kwa bei ya punguzo ya
shilingi 130,000 na HUAWEI Y530 kwa shilingi 195,000 tu.
Ndio aina ya simu ambazo zitakuwa zinauzwa |
Kwa mujibu wa Bw ZACHARIA wanunuzi wa simu hizi
mbili watapata kifurushi cha bure cha thamani ya shilingi 30,000 katika mwezi
wa kwanza baada ya kununua ambapo kifurushi hicho kinajumuisha dakika 600 za
muda wa maongezi,sms 8000,za bure na 1.5 GB za
data za internent.na katika miezi sita inayofuata mteja atakayenunua
kifurushi cha mwezi cha shilingi 15,000 atarudishiwa kiwango sawa na alichonunulia,ambapo
amesema inamaanisha kuwa baada ya baada ya miezi sita
mteja atakuwa amerudishiwa zaidi ya shilingi 120,000.
Akizungumza katika mkutano huo wa waandhishi wa
habari meneja chapa wa kanda ya Africa mashariki na kusini toka HUAWEI AZALEA DU amesema kuwa HUAWEI Y 330 ni simu za kisasa zinazolenga vijana
ambapo kampuni yake inafarijika sana kuwapatia wateja wa tigo fursa ya
kuitumia.
Mwakilishi kutoka HUAWEI akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya TIGO TANZANIA |
Ofa hii inakuja ikiwa ni miezi michache tangu
kampuni ya tigo kutangaza kuwapa wateja wake uwezo wa kutumia FACEBOOK buree
kabisa kwa lugha ya Kiswahili ambapo wateja wake wameonekana kuifurahia sana .
Wednesday, June 25, 2014
HII NDIO TAARIFA RASMI KUHUSU HABARI YA KIFO CHA MH SHUKURU KAWAMBWA
Kutokana na baadhi ya mitandao ya kuijamii muda mchache uliopita kuandika habatri juu ya kumuhusisha na kifo mbunge Shukuru kawambwa mtandao huu umezungumza na watu wa karibu wa waziri huyo na kudai kuwa shukuru kawambwa ni mzima wa afya na habari zinazoenea ni uzushi mkubwa na hazina ukweli wowote.
Na hii ndio mesege kutoka Kwa mbunge RIDHIWAN KIKWETE juu ya uvumi huo.
Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.
UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.
Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze
Mbunge -Chalinze
BREAKING NEWZZ--UCHAGUZI CUF WAMALIZIKA LIPUMBA NA SEIF WAFUNIKA TENA WAPITISHWA KWA KURA ZAIDI YA ASLIMIA 90,CUF WASEMA BADO WANAWAAMINI SANA,FAIDI PICHA HAPA
Profesa LIPUMBA akipongezwa na aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi huo baada ya matokeo kutangazwa muda huu hapa katika ukumbi wa ubungo plaza jijini Dar es salaam |
Uchaguzi mkuu wa cjhama cha wananchi CUF umemalizika hapa jijini dar es salaam ambapo aliyekuwa mwenyekiti profesa IBRAHIM HARUNA LIPUMBA amechaguliwa tena kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano baada ya kupata kura 659 kati yakura 689 zilizopigwa ambapo ni ushindi wa zaidi ya 95% ya kura zote ambapo aliyekuwa mpinzani wake pekee katika uchaguzi huo mh CHIEF YEMBA amepata kura 30 sawa na aslimia 4.3% ya kura zote zilizopigwa.
Katika nafasi ya makamu mwenyekiti mgombea alikuwa mmoja ambaye ni JUMA DUNI HAJI ambaye katika kura 667 zilizopigwa amepata 662 sawa na aslimia 99.25 ya kura zote na kutangazwa rasmi kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho.
Aidha katika nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho kama kawaida mgombea alikuwa mmoja ambaye ni MH SEIF SHARIF HAMAD ambaye katika kura 678 zilizopigwa amejinyakulia kura 675 sawa na aslimia 99.5% ya kura zote zilizopigwa hivyo kutangazwa rasmi kuwa katibu mkuu wa chama hicho akiendelea kushika nafasi aliyokuwa anaiongoza.
Sura za furaha baada ya kurudi tena katika madaraka yao waliyokuwa nayo hapo awali kabla ya mchakato wa uchaguzi |
BREAKING NEWZZ--KINACHOENDELEA KATIKA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA CUF-PICHA NNE MUHIMU ZIPO HAPA
Chama cha wananchi CUF muda huu kinanfanya uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama chao ambapo wagombea mbalimbali wamejitokeza kugombea nafasi hizo.
Katika nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa wagombea watatu wamejitokeza kugombea nafasi hiyo ambao kwa majina ni aliyekuwa mwenyekiti wake pr LIPUMBA,MH CHIEF LUTAYOSA YEMBA,pamoja na mh MBEZI ADAM BALARI,huku nafasi ya makamu mwenyekiti na katibu wakijitokeza wagombea mmoja mmoja ambao ni katika umakamu wa mwenyekiti amejitokeza mh JUM,A DUNI HAJI,na katika nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho amejitokeza mh SEIF SHARIF HAMAD ambaye alikuwa ameshikilia nafasi hiyo.
Matokeo ya uchaguzi huu yatakujia baadae hapa hapa katika mtandao wenu
Wagombea wa uenyekiti wa chama hicho PROFESA IBRAHIMU LIPUMBA akiwa anajadili jambo na mgombea mwezake kabla ya wajumbe kuamua nani wampe tena uenyekiti wa chama hicho cha CUF leo muda huu |
EXCLUSIVE--WALIOMKASHFU MBOWE NA VIONGOZI WA CHADEMA JUU YA UFISADI WAJIBIWA--SOMA TAMKO LOTE HAPA
Ndugu wanahabari,wanachama na wapenzi wa chama cha Demokrasia na maendeleo
kanda ya magharibi na nchini kwa ujumla.
Tumewaalika leo hii ili kuja kuweka sawa kwa kile kinachoendelea
kwa baadhi ya wanachama wa CHADEMA ambao hawana mapenzi mema na chama kwa kile
walichokitoa mbele ya wanahabari huku wakiwa wamejivika vyeo ambavyo ama havipo
au wamekaimishwa au wamekwishavuliwa hapo awali. Taarifa iliyopewa kichwa
”TAARIFA YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WA CHADEMA KWA UMMA”
iliyotolewa tarehe 23/06/2014 katika Hoteli ya Lamada iliyopo jijini Dar es
Salaam.
Ndugu wanahabari.
Mtindo huu umezuka sana hivi karibuni ambao kwa namna moja ama
nyingine unaratibiwa na viongozi wa CCM kwa mgongo wa waliokuwa viongozi wa
CHADEMA ambao kwa sasa ni viongozi wa chama kipya cha Alliance for Change and
Transparence – Tanzania (ACT - Tanzania). Tunasema ni viongozi wa ACT - Tanzania
kwa sababu ushahidi wa kimazingira, wa kimuonekano, wa kimwenendo na
vidhibitisho visivyokuwa na shaka vipo!
Subscribe to:
Posts (Atom)