Mwanamitindo mkongwe kutoka nchini tanzania TAUSI LIKOKOLA akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla yta chakula cha jioni iliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya kuchangisha fedha ziweze kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum ikiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi
Baada ya kukaa nje ya Tanzania kwa zaidi ya maika
kumi na hivi majuzi kurejea kwa kipindi kifupi nchini mwanamitindo maarufu na mkongwe TAUSI LIKOKOLA
usiku wa kamkia leo ameendesha shughuli ya kuchangia fedha kwa ajili ya
kuwasaidia watu wenye matatizo ya ulemavu wa ngozi pamoja na waathirika wa
ugonjwa wa ukimwi nchini ikiwa ni sehemu ya mwanamitindo huyo kurudisha
shukrani kwa watanzania kwa kumpokea tena nchini.
Shughuli hiyo ambayo imeendeshwa jijini Dar es
salaam imeshughudia watu mbalimbali kujitokeza kwa wingi kumpa saport ili
kufanikisha lengo lake hilo ambalo ni jambo ambalo limepongezwa na watanzania
wengi kwani kuna watu wengi wenye uhitaji na inahitajika watu kama TAUSI wengi
ili kuwasaidia watanzania.
Akizungumza na mtandao huu katika hafla hiyo ya
chakula cha jioni iliyokwenda sambamba na harambee hiyo mwanamitindo TAUSI
LIKOKOLA amesema kuwa ni miaka mingi amekuwa nje ya Tanzania na baada ya kurejea
kwake amesikitishwa sana baada ya kukuta tatizo ambalo limeanza kuwa sugu la
mauaji ya watu ambao wana ulemavu wa ngozi jambo ambalo amesema kuwa
limemsukuma kuanza kuwasaidia watu hao kwani kwa sasa wanaishi katika mazingira
yasiyo sala sana.
Mmoja kati ya waandishi nguli na wasomi nchini Tanzania GENERALI ULIMWENGU alikuwa ni mmoja kati wa wageni waalikwa katika shughuli nhiyo ambapo amempongeza TAUSI kwa wazo lake hilo la kuwasaidia watu wenye uhitaji kwani ni baraka hata kwa mwenyezi mungu
Amesema kuwa ni jambo la kutisha sana kuona au
kusikia mambo ambayo wanakutana nayo walemavu wa ngozi nchini Tanzania na hata
ukisikiliza story zao jinsi wanavyoishi bila amani lazima itakugusa ambapo
amesema kuwa ni wakati sasa wa watanzania kukemea kwa lugha moja tatizo hilo
ili likome na lisijirudie tena.
Alikuwepo pia,aliyekuwa miss Tanzania mwaka 2014 SITTI MTEMVU akiwa anashughudia hafla hiyo kwa ukaribu kabisa
Aidha katika hatua nyingine mwanamitindo TAUSI
LIKOKOLA ameitumia hafla hiyo kuzindua manukato yake mapya pamoja na vitabu
ambavyo ameviandika mwenyewe aambapo alitumia bidhaa hizo katika kupiga mnada
ili kupata fedha aweze kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum nchini tanzania.
Mbunifu wa mavazi maarufu nchini TANZANIA MUSTAFA HASANALI ambaye usiku huo ndiye aliyemvalisha TAUSI LIKOKOLA naye alikuwepo katika hafla hiyo
Tupige na sisi picha utotue kwenye blog--sawa nikawapiga ENDELEA KUANGALIA PICHA NYINGI ZA TUKIO HILO HAPO CHINI
MBUNGE wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba amefariki dunia jioni hii jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.
Mmoja wa watoto wa Komba ambaye aliyejitambulisha kwa jina la Herman amethibitisha kutokea kwa msiba huo na akasema, huku akilia, msiba wa baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu, Dar.
Habari zinasema asubuhi ya leo Komba alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi kama kawaida lakini baadaye akajisikia vibaya, hivyo akaamua kurudi nyumbani ambako alizidiwa ndipo familia yake ilipoamua kumkimbiza Hospitali ya TMJ lakini alipopimwa na madaktari ikathibitika kuwa alikuwa tayari ameaga dunia. habari zaidi zinasema kuwa hivi sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Kapteni Komba ambaye pia ni Mkurugugenzi wa Kikundi cha Maigizo cha Tanzania One Theatre (TOT), ambacho kina kikundi cha taarabu na bendi inayokwenda na mtindo wa Achimenengule, amekuwa akikisaidia sana chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni zake wakati wa uchaguzi kwa kutunga nyimbo za kuhamasisha wapiga kura na kushiriki kupiga live kwenye majukwaa ya kisiasa.
.
..alipokuwa bungeni
Enzi za uhai wake alitamani sana na kufanya juhudi kubwa ili mtindo wa Achimenengule uwe wa kitaifa lakini ikashindikana, na badala yake Watanzania sasa tuna muziki wa Mduara ambao umekuwa kama mtindo wa muziki wetu kwa sababu zifuatazo.
Kwanza, ni mtindo halisi wa Kitanzania uliochipuka kutoka mahadhi ya kimwambao ya Tanzania. Pili, ndiyo mtindo pekee uliowahi kutumiwa na bendi nyingi baada ya kuasisiwa na ‘mabingwa’ wa muziki wetu, wana Njenje, The Kilimanjaro Band.
Baada ya bendi hiyo kuuasisi, mtindo huo, tayari umepigwa na bendi kama TOT Plus, Chuchu Sound, Pamo Sound, Inafrika Band, wana mipasho kadhaa na mwanamuziki mahiri lakini asiyethamini kiwango chake kikubwa cha muziki, Bob Haisa.
Sababu ya tatu ni kwamba mtindo huo umekuwa wa kupigwa na bendi nyingi, vikundi vingi na wanamuziki wengi si kwa kulazimisha bali kwa mapenzi tu ya mashabiki wa muziki wa Tanzania.
Kapteni Komba awali alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kabla ya kuingia jeshini na kuwa kiongozi wa kikundi cha maonesho cha jeshi na baadaye Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akamshawishi aachane na jeshi na kujiunga na CCM wakati wa mfumo wa vyama mingi ulipoingizwa mwaka 1992.
“Mzee Mwinyi ndiye aliyenifanya niache jeshi wakati huo nikiwa na cheo cha ukapteni. Aliniomba nikisaidie chama kwa kuanzisha kikundi ambacho lengo lake lilikuwa kukipigia debe CCM,” aliwahi kusema hivyo Kapteni Komba.
Ameshiriki kampenzi za marais Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na aliye madarakani hivi sasa, Jakaya Mrisho Kikwete. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi hadi kifo kinamchukua.
Licha ya siasa Kapteni Komba alikuwa anamiliki shule na pia alikuwa na biashara kadhaa.
Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga.
Baada ya kurejea nchini alisema upasuaji huo ulichukua saa tano na ulifanyika katika Hospitali ya Apollo, India na alikanusha kuwa alikuwa na ugonjwa wa figo.Ugonjwa uliomuua ni shinikizo la damu ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
..marehemu Komba akiongea na wanahabari nyumbani kwake Mbezi tangi Bovu akielezea kuimarika kwa afya yake aliporejea kutoka India kwenye matibabu, Julai 27, 2012.
MALI ZAKE ZATISHIWA KUUZWA
Mapema mwezi uliyopita mwaka huu, mali za Kapteni John Komba zilitangazwa kupigwa mnada kutokana na kushindwa kulipa deni analodaiwa na Benki ya CRDB.
Mali hizo zilihusisha eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2,214 lililopo Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam, kiwanja namba 1030 kilichosajiliwa kwa jina la John Damiano Komba na Salome Komba.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari, Kampuni ya Uwakili ya Mpoki & Associates Advocates inayoiwakilisha CRDB ilitangaza kuuza eneo hilo la kibiashara lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta, maduka makubwa, benki, sehemu ya kufanyia mazoezi, hospitali na huduma nyingine za kijamii.
Marehemu Komba ameacha mjane, Bi Salome, ambaye ni mwalimu kitaalumu na watoto kadhaa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi- ameen!
Kazi inayofanyika katika Baraza la Maadili ni kazi nyeti sana ambayo inajenga 'misingi madhubuti ya uwajibikaji' ili kupambana na rushwa kwa viongozi wa umma. Iwapo Baraza hili lingekuwa limeanza kufanya kazi namna hii tangu mwaka 1995 sheria ya Maadili ilipotungwa, (Sheria hii ilitokana na Muswada binafsi wa Mbunge Jenerali Ulimwengu ), angalau tungekuwa tumeondosha 'impunity' iliyokita mizizi nchini kwetu.
Moja ya adhabu kwa mujibu wa Katiba kwa mtu aliyekiuka maadili ya Viongozi wa Umma ni kupoteza nafasi ya Uongozi aliyonayo. Wananchi tushinikize kwamba Tangazo la Mali na Madeni ya Viongozi wa Umma liwe wazi bila masharti ili kwanza kuwaumbua wanaodanganya mali zao na pili kuwaburuza kwenye Baraza la Maadili kueleza wamepataje Mali walizonazo na za wenza wao.
Taasisi za Uwajibikaji zipo, tatizo hazifanyi kazi inavyotakiwa. Sakata la Escrow limeibua taasisi hizi. Tusiishie hapa
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni Mkala Fundikira,Shafia Mpanja wa AM,Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na Khadija Kalili.
Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za
mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkurugenzi
Mkuu wa Takukuru, Dkt. Ewdard Hose, Mama Esther Gigwa, wakati wa
shughuli za maziko zilizofanyika nyumbani kwa Mkurugenzi huyo, Masaki
jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya marehemu Esther Gigwa, Mama mzazi wa
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki
kuaga mwili huo nyumbani kwa mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo
Feb 27, 2015. Picha na OMR
Wanafamilia wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya maziko
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimfariji, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika
kushiriki kuaga mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkuruenzi huyo nyumbani kwake,
Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Watu wenye ulemavu wa ngozi waendelea kuishi kwa hofu nchini Tanzania.
Mwanza, Jeshi la polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 14 kwa
tuhuma za kuhusika na tukio la utekaji nyara wa mtoto mwenye ulemavu wa
ngozi Pendo Emanuel wa kijiji cha ndami wilayani kwimba tukio
lililotokea Desemba 27 mwaka jana.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za
Misungwi, Kwimba na Sengerema Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa mulongo
amesema kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao wamo waliohusika kwenye
utekaji wa mtoto huyo pamoja na wale waliomuhifadhi kwenye hoteli moja
jijini Mwanza kabla ya kumsafirisha kwenda kusikojulikana.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Mwanza
Alfred Kapole pamoja na katibu wa chama hicho mkoani humo Enos Tuju
wameendelea kukemea ukatili dhidi watu wenye ulemavu wa ngozi Albino
pamoja na kuiomba serikali kudhibiti vitendo vya mauaji ya albino
yanayo endelea kutokea mkoani Mwanza.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida aliyekuwa
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa dare s salaam bwana JOHN GUNINITA leo
ametangaza kumpandisha mahakamani mkuu wa wilaya ya kinondoni DC PAUL MAKONDA kwa kila elichokiita kuwa ni
kudhalilishshwa na kutupiwa maneno ya kashfa.VIDEO IKIONYESHA SIKU MAKONDA ALIPOTOA MANENO HAYO
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dare s salaam
mh GUNINITA amesema kuwa kitendo alichokifanya DC MAKONDA cha kuitisha mkutano
wa wanahabari na kuwatukana viongozi wastaafu wa chama cha mapinduizi ni
kitendo ambacho hakivumiliki na mtu yoyote na kwa kuwa chama kimeshindwa
kumshughulikia sasa njia pekee anayoiona inafa kumwadhibu ni kwenda mahakani
ili haki ipatikane.
Amesema kuwa sio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo aliyewahi
kuwa kiongozi wa umoja wa vijana CCM kulalamikiwa kwa kitendo chake cha utomvu
wa nidhamu mbele ya viongozi wenzake wa ndani ya chama hivyo sasa ni wakati
muafaka wa kuhakikisha kuwa wanamfundisha adabu kwa kutumia sheria za Tanzania.
Ameongeza kuwa chama cha mapinduzi kina utaratibu
wake wa kuwaonya wanachama wake pale wanapokwenda kinyume na utaratibu wa chama
hicho lakini kitendo cha kijana huyo kutoka nje mbele ya wanahabari kuwatukana
viongozi wa chama hicho ambao mbali na uongozi ni baba zake ni kitendo ambacho
sio utaratibu wa chama na hakina wa kuvumilia kitendo hicho
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imethibitisha kushiriki michuano ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Baraza la vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano ya kombe la COSAFA inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya makundi inatarajiwa kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki moja kwa moja na kituo cha Luninga cha Supersport 4.
Taifa Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi nane zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali, nchi nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles, Swaziland.
Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.
Breaking News:Chidi Benzi atupwa jela Miaka miwili kwa makosa ya kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin wakati alipokuwa akienda kufanya tamasha la muziki Oktoba 24 Mwaka jana.
1. Mengi Athman (30), Machinga; mkazi wa Mburahati.
Ulituahidi kuondoa kero ya machinga kabla ya kupata kura yangu, leo hii tunaishi kama popo mitaani umefanya jitihada gani mpaka sasa?
Jibu: Nimetekeleza ahadi hii kwa namna mbalimbali mwaka 2011, 2012, 2013 na 2014. Nimefanya mkutano wa kikazi na Machinga na kupokea kero zilizopewa kipaumbele.
2. Omary Sebea (33), Fundi Seremala; mkazi wa Kimara King’ong’o
Miaka mitano imekwisha na kilio kikubwa cha maji bado hakijamalizika, ninanunua ndoo Sh500, kwa nini nikupe kura yangu 2015? Kwanini eneo la King’ong’o maji hayapatikani wakati kuanzia Kimara mpaka Msikitini na Matosa yanapatikana?
Jibu: Miaka mitano haijaisha na tayari kuna maeneo ambayo hakuna kilio cha maji. Nashukuru Omary Sebea ametambua kwamba maji yanafika Kimara mpaka Msikitini na Matosa. Juu ya eneo la King’ong’o na eneo lingine ambalo hajalitaja la Michungwani maji hayafiki na nilifuatilia Dawasa na Dawasco toka mwaka 2010 na 2011 na nikaelezwa kwamba kwa mwinuko uliopo hayawezi kufika kwa urahisi kutokana na mlima. Sikuridhika na majibu hayo hivyo nitaendelea kuisimamia Serikali.
3. Hamad Hussein (27), Dereva Bajaji; Mkazi wa Makoka
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Zambia Michael Sata aliyefariki mwaka jana katika eneo la maziko ya viongozi wa kitaifa jijini Lusaka Zambia leo.Rais Kikwete alitumia wasaa huo pia kuweka shada la maua katika marais wa Zambia waliofariki Marehemu Frederick Chiluba na Levy Mwanawasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya M-Pesa na Tigo kupitia huduma yake ya Tigopesa. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez.
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya Tigopesa na Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa. Anaeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto, aliyekaa) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia, aliyekaa), wakitia saini mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia huduma ya M-Pesa na Tigopesa. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (wa pili toka kushoto) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia huduma ya M-Pesa na Tigopesa, wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga.
Kocha Msaidizi wa Coastal Union,Jamhuri Kiwelu "Julio"kulia akisisitiza jambo mazoezini jana mara baada ya kuwasilia mkoani Tanga kuifundisha timu hiyo kushoto ni Kocha Mkuu James Nandwa ,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Coastal Union,Albert Peter,Katibu Mkuu Coastal Union,Kassim El Siagi na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.
Kocha Msaidizi wa Coastal Union ,Jamhuri Kiwelu "Julio"akizungumza na viongozi wa Coastal Union mara baada ya kuwasili mazoezini jana ,Picha kwa Hisani ya Coastal Union
Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi , Andrew Chenge akitoka kwenye Kamati ya Maadili leo Jiji Dar Es Salaa
MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Magharibi,AndrewChenge amesema anataka muongozo wa kujadiliwa yeye katika Tume ya Maadili kutokana na suala la Akaunti ya Tegeta Escrow liko Mahakamani hivyo shitaka lake haliko msingi wa kisheria ,Anaripoti KAROLI VINSENT ,Endelea nayo ..
Kugoma kwa chenge kwa shitaka lake kutosikilizwa na kutaka Tume ya Maadili itolee ufafanuzi juu ya kuwepo kwa Shauri kwenye Makama kuu ya Tanzania linalozuia kujadiliwa kesi nje ya Mahakama hivyo kuhusu sakata la Akaunt ya Tegeta Escrow kumetokea mda huu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anasomewa mashtaka yake kwenye tume hiyo ambapo---..
Chenge ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali anashatakiwa na tume ya maadili kutokana na kitendo chake che kupokea pesa ya zaidi Bilioni 1.6.8 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering bwana James Rugimalira wakati akiwa mtumisha wa umma na bila kuitangaza kama zinavyodai sheria za tume hiyo.
Mbunge huyo alipandishwa Mahakama ya Baraza la maadili mda huu Jijini Dar es Salaam mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo maadili Jaji Mstaafu Hamis Msumi -
Ambapo amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Baraza Maadili Hassan Mayunga alidaiwa Mbunge huyo wakati akiwa mwanasheria mkuu wa serikali mwaka 2006 alivunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuipa mkataba wa Miaka 20 kampuni ya kufua Umeme ya IPTL.
Wakili huyo amesema kitendo iko cha Chenge kuipa mkataba kampuni hiyo kinaonekana wazi alikuwa anamaslahi yake binafsi kwenye kampuni hiyo na kupelekea kuingiziwa pesa na Mbia wa Kampuni ya IPTL ambayo ni VIP Engineering na kupata mgao wa bilioni 1.6.8 kama zawadi ya kuingizia hasara serikali kwenye mataba hao.
Mbunge Chenge akimgomea mwandishi wa habari wa Itv na Radio One Ufoo asimuulize swali lolote
Mabishano ya Sheria yatokea
Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo na Wakili huyo wa Baraza hilo ndipo Chenge akaliomba Baraza hilo lisijadili kesi hiyo kutokana na kuwepo kwa kesi mahakama kuu linalokataza Vyombo vyovyote vya Serikali visijadili suala linalohusu Mihamala ya Akaunt ya Tegeta Escrow mpaka pale hukumu itakapotolewa.
Baada ya kusema hivyo Mwenyekiti wa Baraza hilo JajiHamis Msumi
Alimtaka Wakili wa Baraza hilo kuhakiki hati ya Staka ya mahakama kuu na Wakili huyo akajitetea na kusema hakuna kipengere kwenye kesi hiyo iliyoko mahakama kuu kinachozuia vyombo vingine kuzungumzia.
Baada ya kusema hivyo Jaji Hamis Msumi h akahahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili apate mda wa kusoma hati hiyo ya mahakama kuu kama kutakuwa na kipengele hicho kwenye kesi na endapo kitakuwepo basi Tume hiyo haiwezi kulizungumzia suala hilo