Kampuni za simu nchini Tanzania zimeingia katika
ushirikiano na Tume ya Umoja wa Afrika (AU Commission) ili kuendeleza vita
dhidi ya ugonjwa wa Ebola unaoendelea kutishia amani nchi za Afrika Magharibi.
Ushirikiano huo unaojulikana kama ‘AfricaAgainstEbola’(AfrikaDhidiYaEbola)itatumia
mtindo wa ujumbe wa kiganjani (SMS) kuweza kuchangisha fedha kwa ajili ya
kuwawezesha watalaam wa afya kutoka Afrika kuweza kwenda na kuhudumia nchi
zilizo athirika.
Watu
zaidi ya 5,000 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola kutoka sehemu
mbali mbali Afrika Magharibi tangu ugonjwa huo kulipuka kwa mara ya kwanza
nchini Guinea mwezi Machi 2014. Kutokana na taarifa za Shirika la Afya Duniani
(WHO) huu ni mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika bara hili ambayo kwa
sasa ugonjwa huo umeshatapakaa katika nchi nne zikiwemo – Guniea, Liberia,
Sierra Leone na Mali.
Katika
mkutano wa kibiashara uliofanyika hivi karibuni chini ya AU, kampuni za simu
zilijitolea kuanzisha kampeni maalum ya bara nzima ijulikanayo kama “United Against Ebola” (Pamoja Dhidi ya
Ebola). Kampeni hii itakusanya michango kutoka kwa wateja wa kampuni mbali
mbali za simu, na fedha hizo zitakazo kusanywa katika muda wa miezi mitatu,
zitatumika katika mapambano dhidi ya kirusi hiki cha Ebola.















