Friday, December 5, 2014

MICHUANO YA WANAWAKE TAIFA CUP KUANZA DESEMBA 28

Michuano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Proin Women Taifa Cup inaanza rasmi Desemba 28 mwaka huu kwa mechi ya ufunguzi kati ya timu za mikoa ya Mara na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kombaini za mpira wa miguu za mikoa yote ya Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo yatakayochezwa kwa raundi mbili mwanzoni, na baadaye hatua ya robo fainali hadi fainali.

Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin Promotions Limited, kuanzia hatua ya robo fainali, mechi zote zitafanyika jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MWAKYEMBE AWAPONGEZA FASTJET KWA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakzi wa kampuni ya ndege ya FastJet wakati wa maadhimisho ya siku yaanga duniani ambapo aliipongeza kampuni hiyo kwa kutoa huduma kwa bei rahisi kwa wasafiri pembeni yake ni Mwenyekiti wa Bunge ya Miundombinu,  Peter Serukamba.
Ofisa wa Mahusiano na Masoko wa kampuni ya ndege ya FastJet Lucy Mbogoro akitoamaelezo kwa ujumbe kwa Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe na ujumbe wake wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bunge ya Miundombinu,  Peter Serukamba.

TIGO,VODACOM,NA AIRTEL ZASHIRIKIANA NA "AU" KUTOKOMEZA EBOLA AFRICA

Kutoka kushoto: Mkuu wa Mawasliano na Mahusiano ya Umma kutoka Vodacom Bi. Rosalynn Mworia, Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael na Meneja wa Huduma za Kijamii kutoka Airtel Bi. Hawa Bayumi wakionesha ujumbe wa simu kudhibitisha mchango wao katika kampeni maalum ya kampuni za simu nchini 'Tokomeza Ebola'. Kuchangia vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola mteja yeyote wa kampuni hizo tatu anaweza akatuma neno 'Tokomeza Ebola' kwenda 7979.
Kampuni za simu nchini Tanzania zimeingia katika ushirikiano na Tume ya Umoja wa Afrika (AU Commission) ili kuendeleza vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola unaoendelea kutishia amani nchi za Afrika Magharibi. Ushirikiano huo unaojulikana kama ‘AfricaAgainstEbola’(AfrikaDhidiYaEbola)itatumia mtindo wa ujumbe wa kiganjani (SMS) kuweza kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwawezesha watalaam wa afya kutoka Afrika kuweza kwenda na kuhudumia nchi zilizo athirika. 

Watu zaidi ya 5,000 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola kutoka sehemu mbali mbali Afrika Magharibi tangu ugonjwa huo kulipuka kwa mara ya kwanza nchini Guinea mwezi Machi 2014. Kutokana na taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) huu ni mlipuko mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika bara hili ambayo kwa sasa ugonjwa huo umeshatapakaa katika nchi nne zikiwemo – Guniea, Liberia, Sierra Leone na Mali.

Katika mkutano wa kibiashara uliofanyika hivi karibuni chini ya AU, kampuni za simu zilijitolea kuanzisha kampeni maalum ya bara nzima ijulikanayo kama “United Against Ebola” (Pamoja Dhidi ya Ebola). Kampeni hii itakusanya michango kutoka kwa wateja wa kampuni mbali mbali za simu, na fedha hizo zitakazo kusanywa katika muda wa miezi mitatu, zitatumika katika mapambano dhidi ya kirusi hiki cha Ebola.

Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni maalum ya kampuni za simu tatu nchini zilizoungana kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia kutokomeza ugonjwa wa Ebola Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Mawasliano na Mahusiano ya Umma kutoka Vodacom Bi. Rosalynn Mworia, na Meneja wa Huduma za Kijamii kutoka Airtel Bi. Hawa Bayumi (kulia). Kuchangia mteja yeyote wa kampuni hizo tatu tajwa anaweza akatuma neno 'Tokomeza Ebola' kwenda 7979.

ZITTO ATOA SHARTI MOJA ILI AREJEE CHADEMA,SOMA HAPA

Harufu ya kuisha kwa mgogoro baina ya Zitto Kabwe na chama chake cha Chadema inanukia, lakini mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini anataka kuwapo na mazungumzo kubaini tatizo ili atakayebainika kuwa alifanya makosa awe tayari kuomba radhi hadharani.
Zitto alikiri bungeni kuwa amekuwa “akimiss” harakati zilizokuwa zikifanywa na vyama vya upinzani wakati wa Bunge Maalumu la Katiba, harakati zilizozaa Umoja wa Katiba ya Wananchi na kufurahia kuhudhuria kwa mara ya kwanza vikao vya umoja huo.
Zitto, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alipata fursa ya kuingia vikao vya Ukawa wakati wapinzani walipoungana tena kupambana dhidi ya wizi wa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, sakata ambalo liliwekwa bayana na kamati yake baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kulifikisha bungeni, lakini hakudokeza lolote kuhusu Chadema.

ESCROW UPYAAA--KAFULILA ALIPUKA TENA,SASA NI IKULU LAWAMANI,SOMA ALICHOKISEMA MUDA HUU

Na Karoli Vinsent
     WAKATI Rais Jakaya Kikwete akisuasua kuwachukulia hatua viongozi waliotajwa na Bunge kuhusika Katika Wizi wa zaidi ya Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Tegeta Esrcow ,naye Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila Ameibuka upya na Ameivaa Ikulu
       Baada ya kusema Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete inamedhamilia kuwalinda wezi waliohusika katika kuiba pesa hizo,baada ya kumzuia Mkurugenzi wa ofisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa PCCB Dk Edward Hosea kutoiwasilisha Taarifa ya uchunguzi juu ya sakata hilo la Esrcow  kwa Umma kutokana na Ripoti ya PCCB kuwataja vigogo wa Ikulu kuhusika katika kuchota pesa kwenye Benk ya Stabink.
    Hayo yamebuliwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kafulila  huku akizungumza kwa uchungu alisema Inasikitisha kuona jinsi Ikulu inavyotumia ubabe wake kumzuia Dk Hosema kutoiweka wazi ripoti yake ya uchunguzi.

HABARI PICHA--TESEMA FC YA KINONDONI YAJIPIMA UBAVU NA MTIBWA SUGAR KARUME

Timu ya mpira wa miguu jijini Dar es salaam ambayo inamilikiwa na halmashauri ya manispaa ya kinondoni TESEMA FC  ikiwa katika harakati za kujiandaa kuendelea kushiriki na mashindano ya ligi daraja la kwanza jijini Dar es salaam,imejipima nguvu na vinara wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu MTIBWA sugar ya mkoani morogoro,mchezo uliofanyika katika uwanja wa karume jijini Dar es salaam,timu hiyo ambayo ni ya kwanza kumilikiwa na manispaa zinazopatikana jijini Dar es salaam jana ilikuwa katika kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa michuano ya ligi daraja la kwanza ambapo ilishughudia timu hiyo ikimenyena vikali na timu hiyo na kuonyesha uwezo mkubwa mbele ya wababe wa soka hadi sasa wa ligi ya Tanzania MTIBWA SUGAR huku ikishughudia mtibwa ikiibuka mshindi kwa mabao mawili kwa bila .Picha zote za mchezo huo ziko chini,mtibwa sugar ni hao waliovaa blue

Thursday, December 4, 2014

TASWA YAPITIA MAJINA YA WATU WALIOTANGAZWA KUWANIA TUZO,YOTE YAKO HAPA

Mkurugenzi wa Times Fm, Rehure Nyaulawa akisisitiza jambo
KAMATI ya Kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kupitia majina ya wanamichezo waliopendekezwa kuwania tuzo hizo.
Tuzo itafanyika Desemba 12 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee (VIP), Dar es Salaam, ambapo wanamichezo mbalimbali waliofanya vizuri kati ya Juni 2013 hadi Juni 2014 watakabidhiwa tuzo zao.
Ni imani yetu kwamba zaidi ya wanamichezo 40 watakabidhiwa tuzo zao siku hiyo, ambapo kamati imejiridhisha kwamba wanaowania tuzo hiyo wanastahili kulingana na mapendekezo ya vyama vya michezo kupitia Kamati zao za Ufundi.
Mshindi wa kila tuzo ataingia katika mchakato wa kumpata Mwanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2013/2014, ambapo pia siku hiyo ya sherehe za tuzo itatangazwa zawadi ya Tuzo ya Heshima kwa yule ambaye itaonekana alikuwa na mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya kimichezo hapa nchini. Tuzo hizo ni kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014.
ORODHA KAMILI YA WANAOWANIA TUZO ZA TASWA 2013/2014

KAMISHNA KOVA AWATAKA ASKARI WALIOMALIZA MAFUNZO YA UONGOZI MDOGO WA JESHI LA POLISI KUTUMIA UJUZI NA MAARIFA WALIYOYAPATA KUONDOA KERO NA KUDUMISHA AMANI KATIKA MITAA YOTE YA JIJI LA DAR


 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akifurahi jambo wakati akizungumza na Askari Polisi waliomaliza Mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika vyuo vya Polisi vya Moshi na Zanzibar,wakati alipowapokea leo Desemba 4,2014 katika Kituo cha Kati cha Polisi,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Askari Polisi waliomaliza Mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika vyuo vya Polisi vya Moshi na Zanzibar wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova,wakati akiwaasa maswala mbali mbali yahusuyo Jeshi hilo.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam amewapokea askari waliomaliza mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika vyuo vya Polisi vya Moshi na Zanzibar ambao ni utaratibu wa kawaida na kuwaasa mambo yafuatayo:

KUELEKEA SIKUKUU HIINDIO KAULI YA SUMATRA JUU YA USAFIRI WA MIKOANI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Dk Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es salaam jana juu ya hali ya usafiri kipindi cha siku kuu za Krismas na mwaka mpya ambapo ametahadharishja abiria kuto kukubali kutozwa nauri za juu na pindi ikitokea hivyo Sumatra ipewe taarifa haraka.
 BARAZA  la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA Limewakumbusha wamiliki wa Mabasi yaendayo  Mikoani na Madereva  kufuata  Masharti ya Leseni zao kwa  kutotoza nauli kubwa katika kipindi hiki cha Sikuku za mwezi Desemba na endapo mtu akikiuka sheria basi Mamlaka hiyo haitosita kumfutia Leseni  ya Basi litakalokwenda kinyume.
        

TIZAMA WALICHOKIFANYA CHADEMA KWENYE BUNGE LA ULAYA

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Safari Abdalla akisalimiana na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP) Rainer Wieland wakati ujumbe wa CHADEMA ulioko nchini Ubelgiji, ulipofika ofisi za bunge hilo mjini Brussels kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa BAWACHA, Grace Tendega na Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri John Mrema.
Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Patrobas Katambi. Ujumbe wa CHADEMA ukiongozwa na mwanadiplomasia mahiri Profesa Abdalla Safari, uko nchini Ubelgiji kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demoikrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Safari na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu wakiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, wakati ujumbe wa CHADEMA ulipofika Ofisi za EP kuanza ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa bunge hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Profesa Abdalla Jumbe Safari akiwa na Makamu wa Rais wa Bunge la Ulaya (EP), Rainer Wieland, walipokutana jana mjini Brussels, Ubelgiji kwa mazungumzo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya ujumbe wa CHADEMA kufuatia mwaliko wa bunge hilo.

fastjet kwenye maadimisho ya miaka 70 ya kimataifa ya safari za anga duniani

unnamed2
unnamed1

TAARIFA MAALUM KWA WATEJA WA NBC KUHUSU PESA ZAO

Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo akitoa ufafanuzi wa tatizo la huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo alisema licha ya tatizo hilo hakuna hata senti moja ya mteja wao iliyopotea. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rukia Mtingwa.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu tatizo lililojitokeza jana katika huduma zao za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo alisema licha ya wateja kutoona salio katika akaunti zao hakuna hata senti moja iliyopotea. Kushoto ni Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Jimmy Myalize.
Baadhi ya wanahabari wakiwa kazini kurekodi mkutano wa menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) jijini Dar es Salaam leo walipokuwa wakitoa ufafanuzi juu ya tatizo lililojitokeza jana Desemba 3, 2014 ambapo wateja wa benki hiyo walishindwa kutumia huduma za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi (Mobile Banking).

Wednesday, December 3, 2014

CHADEMA WAPATA MWALIKO BUNGE LA ULAYA,SOMA HAPA

CHADEMA Waalikwa Bunge La Ulaya
Baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wamepata  mwaliko wa kuhudhuria Bunge la ulaya nchini Ubelgiji, na kukutana na viongozi wa bunge hilo, pamoja na kuhudhuria mkutano Mkuu wa 27 wa  chama cha CDU nchini Ujerumani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar,  Salum Mwalim amesema, ujumbe huo wa CHADEMA utafanya mazungumzo na viongozi wa bunge hilo, juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini.

Amesema  kama chama kikuu cha upinzani,  watakaowakilisha ni ujumbe wa viongozi wakuu wa Chadema na wamejipanga kufanya mazungumzo, maalumu kwa mustakabali wa taifa la Tanzania.

Aidha mwalimu amesema wakiwa  nchini ujerumani  viongozi hao watazungumzia changamoto  mbalimbali  zinazolikabili taifa
Ujumbe huo wa CHADEMA tayari umeshaanza safari yake, na utakuwa kwenye ziara hiyo kwa muda wa siku kum