Wednesday, September 7, 2016

KUTOKA BUNGENI--Watumishi wameaswa kuwasilisha nyaraka zao mapema kabla ya muda wa kustaafu.

index
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Dodoma.
Serikali katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti 2016 imefanikiwa kulipa jumla ya sh. bilioni 511.86 ikiwa ni malimbikizo ya mwajiri kwa watumishi waliostaafu.

Kivutio cha Kimondo kuendela kuongeza mapato ya Serikali

kimondo 
Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.
……………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.
Serikali inaendelea kutangaza Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya ikiwa ni kivutio muhimu na adimu nchini na duniani kwa ujumla.

KUTOKA BUNGENI-Wanasiasa wameaswa kuzingatia na kutotumia masuala ya Muungano kwa maslahi yao binfsi.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4jbYzT0dGIe018FscqY9vFpou1V0o1vh_yklmep1479yT0TMVFrJrbXkPyAeohkg1KwtyYkbn2Yis5UaPlaLHusIkUlAEJN2UPceJp6tf3OacLGWG5MBJQu9LD-5O_XY3iSMRgoSFzrAW/s1600/Makamba.jpgNa Beatrice Lyimo – MAELEZO, Dodoma
Serikali imetoa wito kwa wanasiasa kutotumia masuala ya Muungano katika masuala yao ya kiasisa kwani watu wa pande mbili za Muungano hawawezi kufarakana kwa sababu ya umiliki wa eneo.

CUF MKUU SAWA UKUTA--MTATIRO ATANGAZA KUJIUNGA,AUKATAA UENYEKITI WA CUF

http://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2015/08/Julius-Mtatiro.jpgMwenyekiti wa muda wa Chama Cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amesema kuwa hatawania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi unaopangwa kufanyika hivi karibuni.

Mtatiro alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa muda wa chama hicho akikalia nafasi iliyoachwa na Profesa Ibrahim Lipumba aliyejiuzulu mwaka jana na baadae mwaka huu kuzua sintofahamu baada ya kutengua uamuzi wake na kutaka kurejeshewa nafasi hiyo.

“Sina mpango wa kuwania nafasi ya uenyekiti wa CUF hivi karibuni,” Mtatiro anakaririwa na Mwananchi. “Nitaendelea kuitumikia CUF kama mwanachama mtiifu,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa muda alisema kuwa anaunga mkono mpango wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuitisha maandamano nchi nzima Oktoba 1 mwaka huu baada ya kuahirisha kufanya hivyo Septemba 1 kupitia kile wanachokiita Oparesheni UKUTA.

“Ninawapongeza Chadema kwa kusogeza mbele maandamano hadi Oktoba 1 ili kupata muda zaidi wa ushauri,” alisema.
“Kwa niaba ya wanachama wa CUF na watu wanaotuunga mkono ninatangaza kuwa tutashiriki katika maandamano hayo,” Mtatiro anakaririwa.

Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku kufanyika kwa maandamano na mikutano ya kisiasa nchi nzima na tayari imewashikilia, kuwahoji na kuwafungulia mashtaka baadhi ya viongozi wa Chadema waliohusika kuandaa maandamano hayo.

Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa chama hicho pia walihojiwa na Jeshi la Polisi.

Tuesday, September 6, 2016

MSAADA KWA MGONJWA DANIEL MANOTA

Daniel Manota ni mhitimu wa mafunzo ya ualimu Ilonga Tc mwaka 2015.anasumbuliwa na maradhi ya FIGO tangu mwezi wa 10/2015,kwa sasa yuko Mhimbili hospital,hari yake inazidi kuwa mbaya kwa kukosa pesa za kununua dawa,hivyo kama ndugu ,jamaa na rafiki unaombwa kumchangia ili aweze kununua dawa zake zinazogharimu kiasi cha sh.milion 1 kwa wiki. 
Tunaomba tumuunge mkono kijana mwenzetu ambaye anapata maumivu makali .MUNGU HUMBARIKI ATOAYE KWA MOYO WA UKUNJUFU.
Tuma mchango kupitia namba hii ,tuunganishe nguvu zetu kwa lengo la kuokoa maisha yake.hii..............
0659656970. NEEMA URASA
076818874 .DANIEL MANOTA

MBEYA CITY FC WAANZA MAZOEZI MAKALI KUJIWINDA NA AZAM FC

IMG_20160906_133654BAADA ya mapumziko ya siku ya jana  yaliyotolwa na kocha Kinnah Phiri kufuatia  safari ndefu ya saa nyingi kutoka  kanda ya ziwa, kikosi cha Mbeya City fc  leo kimeanza mazoezi rasmi kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc  uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa  siku ya jumamosi.

Exclusive Video--ZITTO KABWE amfungulia Milango Lipumba,Akana habari za Jana lakini------------

Baada ya story myingi za jana zikimuhusisha Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF Mh LIPUMBA IBRAHIM kujiunga na ACT WAZALENDO hatimaye leo Kiongozi mkuu wa ACT WAZALENDO Mh ZITTO KABWE ameamua kufunguka juu ya sakata hilo huku akikana vikali habari hizo lakini akitanabaisha kuwa chama chake kinampokea mtu yeyote mwenye vigezo vya chama hicho.Nimekuwekea Video wakati alipoulizwa na wanahabari leo Juu ya Habari za Lipumba Kujiunga na chama chao  

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHASEMA UCHUMI WA NCHI KWA KIPINDI CHA MIEZI SITA UMEPUNGUA KWA ASILIMIA NNE

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kabwe Zitto (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa tamko la kamati kuu ya chama hicho baada ya kufanyika kikao chake cha kawaida jana. Kushoto ni Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho,  Juma Sanani na kulia ni Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Shaban Mambo.
Taswira meza kuu. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho,  Juma Sanani , Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Shaban Mambo, Makamu Mwenyekiti Tanzania Zanzibar, Ramadhan Ramadhan na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Msafiri Mtemelwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Millicom afanya ziara nchini Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Millicom ambayo ni kampuni Mama ya Tigo Tanzania Mauricio Ramos (Kushoto) akijibu maswali kutoka kwa wafanyakazi wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tigo jijini Dar es salaam. Ramos yuko nchini kutembelea kampuni ya Tigo na miradi yake.  Kushoto kwake ni Mjumbe wa bodi ya Millicom na Mkurugenzi wa uendelezaji vipaji  wa kampuni ya Tigo, Catherine Olak
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Millicom ambayo ni kampuni Mama ya Tigo Tanzania Mauricio Ramos (Kushoto) akijadiliana jambo na wafanyakazi wa Tigo mara baada ya mkutano pamoja nao mapema wa wiki iliyopita.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Millicom ambayo ni kampuni Mama ya Tigo Tanzania Mauricio Ramos (Kushoto) akijibu maswali kutoka kwa wafanyakazi wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tigo jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita. Ramos yuko nchini kutembelea kampuni ya Tigo na miradi yake.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII

http://africandevjobs.com/wp-content/uploads/2015/11/samia-suluhu.jpgOfisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.
Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.
Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam

Breaking news---ACT waibuka Baada ya kamati kuu Jana kukutana,waishukia serikali ya Magufuli

Tamko Rasmi la Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo kuhusu HALI YA NCHI 

1.Utangulizi

Jana Jumatatu, 5 Septemba 2016, Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo ilikutana katika kikao chake cha kawaida. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ilipokea, kujadili na kuidhinisha Taarifa kuhusu HALI YA NCHI. Taarifa hii sasa inatolewa rasmi kwa umma. Taarifa ipo katika maeneo makubwa manne: Hali ya kisiasa, hali ya kiuchumi, umoja wa kitaifa na hitimisho. 

Monday, September 5, 2016

TAARIFA MPYA KUTOKA ACT-WAZALENDO BAADA YA KAMATI KUU KUMALIZA KIKAO

ACT Wazalendo: TAARIFA KWA UMMA
Baada ya kumalizika kikao cha kamati kuu ya Chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika leo septemba 05/2016 jijini Dar esSalaam
Kesho Jumanne Septemba 06/2016,Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo watakutana na waandishi wa habari na kuelezea masuala mbali mbali muhimu yanayoendelea sasa ikiwemo:

• Hali ya Uchumi wa Taifa
• Hali ya Kisiasa ya Taifa
• Hatari ya Kuvunjika Kwa Umoja wa Kitaifa

Wapi:Makao Makuu ya ACT wazalendo yaliyopo Sayansi Kijitonyama jirani na Kanisa la KKKT
Muda:Saa tano kamili asubuhi (11:00am)
Kuhusu taaarifa zilizosambaa za Prof. Lipumba kujiunga na chama hicho, ACT- Wazalendo wamesema kuwa hawana taarifa yoyote ya Prof. Lipumba kujiunga na chama hicho na pia kikao cha leo hakihusiani na ajenda yoyote ya kupokea wanachama.
Muhimu kuzingatia muda
Abdallah Khamis

Afisa Habari
0655549154

TIZAMA PICHA CHADEMA WALIVYOKINUKISHA MAHAKAMANI SIMIYU,WAFUASI WAKE WAPEWA DHAMANA WOTE


Chadema imeibwaga serikali mahakamani baada ya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Simiyu kuzitupilia mbali hoja za upande wa mashitaka za kuzuia dhamana kwa viongozi na wanachama wa Chadema wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi.


Pia polisi walizuia msafara wa Mbowe wakati ukitoka mahakamani kwa muda wa Dk 45.Wote wamepatiwa dhamana.Tazama picha hapa kutoka kwa mwandishi wetu aliyeko Simiyu,Samwel Mwanga kilichojiri