Friday, August 28, 2015
Thursday, August 27, 2015
Kidoogo yatokee mafuriko--Tizama mkutano mzima wa lowasa na wanawake wa Dar es salaam leo


Wanawake kutoka kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika ukumbi wa Milenium Tower katika mkutano wa baraza la wanawake wa Chadema ambao mgeni rasm ni mgombea wa urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa ambaye amewataka wanawake kushiriki ipasavyo katika kuleta mabadiliko.
Mheshimiwa Lowassa aliyeambatana na viongozi wa juu wa chama hicho amesema wanawake wana mchango mkubwa wa kufanikisha ndoto za watanzania za kupata mabadiliko ya kweli.
WLAC yawapiga msasa wanawake wagombea katika uchaguzi ujao
| Mmoja kati ya wawezezaji wa warsha hiyo FORTUNATA MAKAFU kutoka Dodoma akiendelea na kutoa mada mbalimbali katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam |
| Wagombea mbalimbali waliojitokeza ambapo takribani wanawake 50 wameshiriki katika semina hiyo |
| Mgombea wa ubunge segerea kupitia chama cha mapinduzi CCM mama LUCY GEREMIA akizungumza na wanahabari waliotaka kujua manufaa ya mkutano huo kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu. |
Tizama wanawake wa UKAWA na LOWASA MUDA HUU
Wednesday, August 26, 2015
Magufuli Huko mbeya Usiseme--Tizama hii
![]() |
| Nyomi la Watu katika mkutano wa kampeni. |
![]() |
| Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu. |
![]() |
![]() |
| Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingin Tunduma mkoani Mbeya |
![]() |
| Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana kwa ajili ya mkutano wa kampeni. PICHA NA MICHUZI BLOG |
TIMU YA KAMATI YA AMANI YA VIONGOZI WA DINI MKOA WA DAR, YAENDELEA KUJIFUA UWANJA WA KARUME KUJIANDAA KUWASAMBARATISHA WENZAO WA ARUSHA MWEZI UJAO.
![]() |
| Kamanda Mpinga, akishiriki dua ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, baada ya mazoezi yao timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki na timu ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa Arusha unaotarajia kuchezwa mwezi ujao jijini Arusha na ule wa kirafiki kati yao na timu ya Mabalozi hivi karibuni. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao. |
![]() |
| Kamanda Mpiga akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya Mkoa wa Dar es Salaam,baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Kamanda Mpinga alifika kuwatembelea wachezaji hao kujionea maendeleo ya mazoezi yao. |
![]() |
| 5:- Kamanda Mpinga, akisalimiana na walimu wa timu hiyo, baada ya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. |
Breaking Newzz--Lowasa apigwa Stop jangwani jumamosi,Mbatia aibuka ,soma alichosema hapa
Umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA umesisitiza kuwa utazindua kampeni zake siku ya jumamosi ya
tarehe 29 mwezi huu katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam licha ya
mizengwe wanayowekewa na mansipaa ya ilala ya kuwanyima kutumia uwanja huo kwa
sababu ya kuwa na matumizi mengine siku hiyo.
Akizunzgumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa NCCR mageuzi ambaye
pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja huo JAMES MBATIA amesema kuwa uzinduzi huo
utafanyika siku ya jumamosi kama ilivyopangwa japo manispaa ya ilala
imewaandikia barua ya kuwa na matumizi
mengine siku hiyo.
Mbatia amesema kuwa
wamepeka maombi ya kutumia uwanja huo na wamejibiwa kuwa kuna watu
wameshauchukua kwa ajili ya kazi nyingine ambapo walipojaribu kuuliza ni mtu
gani ili wazungumze naye manispaa hiyo imegoma kumtaja na kusisitiza kuwa
uwanja huo utakuwa ukitumika siku hiyo ya jumamosi.
Mbatia amesema kuwa
kumekua na mbinu chafu ambazo zinatumiwa na serikali kupitia wakuu wa mikoa na
wakuu wa wilaya za kuhujumu harakati za kampeni za umoja huo lakini wamejipanga
kuhakikisha kuwa wanatetea haki yao na kuleta usawa katika kampeni hizo.
Akitolea mfano wa
mgombea EDWARD LOWASA leo kunyimwa kuendelea na ziara yake ambayo leo ilipangwa
kufanyika katika baadhi ya hospiytali kuzungumza na wagonjwa huku mgombea
mwenza wa chama cha mapinduzi SAMIA SULUHU akiendelea na zoezi kama hilo mkoani
kilimanjario jambo ambalo amesema kuwa ni rafu ya wazi ambayo kamwe hawawezi
kuivumilia.
Akizungumzia swala la
kampeni ya chama cha mapinduzi siku ya uzinduzi kufanyika hadi saa kumi na
mbili na nusu kinyume na sheria za uchaguzi mbatia amesema kuwa tume ya taifa
ya uchaguzi imekuwa ikikaa kimya kwa kuwa kitendo hicho kilifanywa na chama tawala
lakini kingefanyika na chama cha upinzani lazima wangepigwa mabomu jambo ambalo
amedai kuwa ni kuendelea kuwajaza hasira watanzania ambao wengi sasa wamekuwa
na kiu ya mabadiliko nchini.
Tuesday, August 25, 2015
WAZIRI WA FEDHA SAADA MKUYA SALUM AZINDUA BODI YA PPF NA MAFAO MAPYA YA MFUKO
![]() |
| Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja, mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Sara Haule ikiwa ni malipo ya fao la uzazi wakatinwa uzinduzi wa bodi mpya ya PPF, sambamba na uzinduzi wa fao hilo la uzazi, Jumanne Agosti 25, 2015. |
![]() |
| Waziri Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya uzinduzi |
![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akitoa hotuba ya ukaribisho na utambulisho nwakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Mfuko, sambamba na uzinduzi wa Fao la Uzazi, ambapo wanachama wawili wa Mfuko, Sara Haule na Caroline Kiswaga, walilipwa shilingi milioni 1 kila mmoja kama malipo ya fao hilo. |
KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAZINDUA KAMPENI YA 'CHAGUA TIGO PESA, INALIPA
Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa kampeni ya ya Chagua Tigo Pesa, Inalipa. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Tizama mizunguko yoote ya lowasa leo Tandale na Kwingine
![]() |
| "Uongozi usioyafahamu matatizo ya Watanzania kiundani hauna uhalali wa kuelezea suluhisho la matatizo hayo. Tumechoshwa na aina ya uongozi wa kuletewa ripoti maofisini, na Leo tumeendeleza ziara ya kuwatembelea wananchi na kusikia kero zao Za msingi. Tukutane Jangwani Jumamosi hii ya tarehe 28.8.2015 tuweze kuwaeleza namna tulivyojipanga kufanya ukombozi wa kiuchumi. Tuko Tayari kwa mabadiliko"-Edward Ngoyai Lowassa |
Tizama Taifa stars wakijifua nchini Uturuki
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro ambayo iliwasili jana nchini Uturuki, imeendelea na mazoezi leo asubuhi katika viwanja viliyopo kwenye viunga vya hoteli ya Green Park – Kartepe.
Mara baada ya kuwasili jana jioni katika eneo la Kartepe, timu ilifanya mazoezi jioni kwa takribani saa moja na nusu, kuanzia saa 1 jioni mpaka mida ya saa 3 kasoro usiku, ambapo leo na kesho itafanya mazoezi asubuhi na jioni.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema huduma na vifaa vilivyopo katika hoteli waliyofikia (viwanja, gym) wanavyotumia kwa ajili ya mazoezi ni vizuri, hivyo ratiba yake ya mazoezi inakwenda kama alivyopanga katika maandalizi ya wiki moja ya kuajiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa mazoezi na timu ya Taifa ya Libya siku ya ijumaa, ambapo kocha Mkwasa atatumia nafasi hiyo kupima kikosi chake baada ya kuwa wamefanya mazoezi kwa siku nne nchini Uturuki.
Kikosi cha wachezaji 21 chini ya kocha mkuu Charles Mkwasa, na msaidizi wake Hemed Morocco, kocha wa makipa Peter Manyika na mshauri wa benchi la ufundi Abdallah Kibadeni wanaendelea kuwanoa vijana vilivyo kwa ajili ya mchezo wa mwezi Septemba dhidi ya Nigeria.
|
Wachezaji waliopo kambini nchini Uturuki ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Abdi Banda, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub.
Lowasa abanwa tena na polisi Kuhusu ziara zake Jijini Dar.Soma kauli ya kova leo
Monday, August 24, 2015
TSUNAMI LA MAGUFULI LATIKISA NYUMBANI KWA PINDA-TIZAMA HII
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Chama hicho uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio mjini Mpanda mkoani Katavi leo ambapo amehutubia mikutano ya hadhara mitatu katika mkoa huo katika maeneo ya Mishamo, Katumba na Mpanda mjini.
Dr. Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ili ashinde na shughulika na matatizo ya wananchi kwakuwa anayaelewa matatizo na shida nyingi za watanzania, Dr. Magufuli ameahidi kukamilisha ujenzi wa barabara za Kasulu -Mpanda, Sumbawanga – Mpanda , Mpanda -Tabora ili zikamilike kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia wananchi katika shughuli mbalimbali za kiuchumi mkoani humo PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-KATAVI
Subscribe to:
Posts (Atom)












