Monday, March 31, 2014
HABARI AMBAYO IMELISONONESHA TAIFA LEO--------AJALI MBAYA 14 WAFARIKI DUNIA, WAOKOAJI NAO WAZOLEWA WAFARIKI NA KUFIKIA WATU 21
Watu 21 wamefariki dunia katika ajali mbaya imetokea Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ikihusisha magari 3 na wengine 11 kujeruhiwa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alisema ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Lindi, eneo la Ikwiriri, wilayani humo.
Awali
ajali hiyo ilihusisha magari mawili, Toyota Hiace (T 948 CUX),
iliyokuwa ikitokea Ikwiriri kuelekea Rufiji ambalo lilikwenda
kukwaruzana na Lori(T 132 AFJ) kwa nyumba, ambalo lilikuwa limeharibika
na kusimama barbarani.
HEKA HEKA ZA UBUNGE HUKO CHALINZE---MWENYEKITI WA CCM AHAMIA CHADEMA
MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 26/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Machi 30 mwaka huu) Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam imeingiza sh. 26,455,000.
Watazamaji 4,741 walikata tiketi
kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawanyo kwa mapato ulikuwa Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47, gharama za kuchapa tiketi sh.
3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh. 5,460,687.63.
Uwanja sh. 2,776,620.83, gharama za
mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh. 1,665,972.50, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.
HELIOS TOWERS LAUNCHES IN BUILDING SOLUTIONS (IBS)
Some of invitees
exchanging views during the launching event. |
THE telecoms
Infrastructure Company in Tanzania, Helios Towers has inaugurate the In-Building
Solutions (IBS) to strength and magnifying telecommunication networking in
Tanzania.
Speaking during the
launching of the operation in Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es Salaam,
yesterday the Chief Executive Officer of Helios Towers Norman Moyo said, this
is new services in Tanzania that will ensure good and reliable telecoms
networking in big and tall building in the country as well as strong telecoms
road in the country.
PICHA TATU ZINAZOONYESHA JINSII POLISI LEO WALIVYOWAKUSANYA BODA BODA WALIOKUWA WANAINGIA KATIKATI YA JIJI
Sunday, March 30, 2014
BREAKING NEWZZ--DARAJA LA MTO RUVU MVUA YASABABISHA MAJANGA MUDA HUU
HABARUI AMBAZO TUMEPENYEZEWA HAPA NI KUWA MVUA KUBWA INAYONYESHA MAENEO MBALIMBALI YA TANZANIA IMESABABISHA DARAJA LA MTO RUVU LINALOUNGANISHA MSATA NA BAGAMOYO KUFUNIKWA NA MAJI KIASI CHA KUTAKA KUVUNJIKA MAGARI YOTE YANAYOTUMIA DARAJA HILO YAMETAKIWA KUPITA CHALINZE KWANI HALI YA DARAJA HILO NI MBAYA
HABARI AMBAYO INATIKISA NCHI----KARIAKOO YAHAMIA COCO BEACH KWA MUDA,YALE MAONYESHO MAKUBWA YA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO YANAENDELEA MUDA HUU.CHUKUA MUDA WAKO KUFAIDI KINACHOENDELEA HUKO
Bidhaa ambazo huwa unazipata ndani ya soko la kariakoo sasa zinapatikana ndani ya ufukwe wa coco beach kwa gharama nafuu sana na bidhaa nzuri kwa utulivu kabisa |
wauzaji wa bidhaa hizo wakiwa wanaweka mambo sawa asubuhi hii wakati wakijiandaa kuwahudumia mamia ya wateja wa dar es salaam watakaojaa muda sio mrefu ndani ya coco beach |
Saturday, March 29, 2014
KITUKO KUTOKA CHALINZE--BARA BARA MBOVU ZAKWAMISHA KAMPENI ZA CHADEMA KWA MASAA KADHAA,MGOMBEA UBUNGE MATHAYO TORONGEY AJITOSHA KUCHIMBA BARABARA MAMBO YAENDE,CHEKI HAPA
Panaitwa Kidung'hwe, Kata ya Msoga kwao mkulu...hakuna barabara kuna kile ambacho kinaitwa mapitio ya mifugo. |
Mathayo torongei kiwa kazini |
BAADA YA YULE MWANDISHI WA DAILY MAIL KUITWA TANZANIA,HATIMAYE AWAGEUKA WALIOMWITA,AANDIKA MAKALA NYINGINE YA KUKOSOA TENA JK NA NYALANDU JUU YA UJANGILI
Mwandishi huyo akitembelea hifadhi ya meno ya tembo |
NA KAROL VICENT
KILE kinachotafsriwa ni kugeukwa kwa
serikali ya Tanzania na Mwandishi wa Gazeti la Sunday Mail la Nchini uingereza
Martini Fletcher baada ya kuandika makala nyingine ikihishutumu tena
serikali ya Jakaya kikwete kwa kushindwa kuwachukilia hatua Majangili.
Kugeukwa kwa Serikali ya Tanzania
kumetokana na Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro
Nyalandu kutumia Garama kubwa ya kumuita Mwandishi huyo kile
kinachoonekana ni kujikosha kwa serikali baada ya mwandishi huyo kuandika
makala ikiituumu serikali ya Tanzania kushindwa kuwachukulia hatua Majangili.
HAYA SASA---DK SLAA NA MAKATIBU WA VYAMA VYA UPINZANI WAUNDA UKAWA NJE YA BUNGE,WATANGAZA KUFANYA MIKUTANO MIKUBWA NCHI NZIMA KUPINGA MCHAKATO WA KATIBA MPYA,KESHO WANAANZIA MWANZA,SOMA HAPA
Makatibu wakuu wa vyama vya CHADEMA,CUF,NA NCCR MAGEUZI wakizungumza na wanahabari jijini dar es salaam baada ya kutangaza muungano wao wa kupinga mambo ambayo yanaendelea bunge maalum la katiba |
Mungano
wa vyama vitatu vya upinzani vyenye wabu nge bungen ambao kwa sasa unajiita
umoja wa katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza kufanya mikutano ya hadhara
kiwa mikoa yote Tanzania kupinga kile ambacho wanakiita kuhujumiwa kwa mchakato
wa kupata katiba mpya ambao wanaituhumu moja kwa moja ccm kuwa wanataka
kuhujumu mchakakato wa kupata katiba mpya.
Akitangaza maamuzi hayo ambayo ni ya makatibu wakuu
wa vyama vya CUF,NCCR MAGEUZI NA CHADEMA,katibu mkuu wa CHEDEMA dk WILBROD SLAA
wakati wa mkutano na wanahabari katika katika makao makuu ya CHADEMA amesema
kuwa ukawa imekuwa ikifanya kazi ndani ya bunge na sasa wameunda UKAWA nje ya
bunge ili kuwasaidia wale waliopo bungeni kuwaletea watanzania katiba ya
wananchi na siyo ya ccm.
Dk SLAA anasema kuwa UKAWA NJE wameamua kuwafuata wananchi wa Tanzania kuwaunganisha
nguvu zao na kuwaeleza ukweli juu ya mchakato wa katiba mpya unavyotekwa na ccm
na kufanya wabunge wa bunge maalum la katiba wanaotaka katiba ya wananchi kuonewa
ndani ya bunge na kutokutendewa haki katika bunge hilo.
Anasema kuwa UKAWA NJE watafanya mikutano ya hadhara nje na ndani
kwa nchi nzima ambapo kampeni hiyo wametangaza kuizindua kesho mkoani mwanza na
baadae kufanyika kila mkoa wa Tanzania.
Katibu mkuu wa CHADEMA DK WILBROD SLAA akizungumza kwa niaba ya makatibu wakuu wenzake katika mkutano na wanahabari jijini dar es salaam muda mfupi uliopita |
TAARIFA KWA VIJANA WOTE DAR ES SALAAM NA TANZANIA
Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yenye jukumu la kusimamia sekta
ya Vijana nchini imeandaa Kongamano la Vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya
Juu kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano Wetu Miaka 50
tangu kuzaliwa kwake.
Friday, March 28, 2014
TAZAMA PICHA ZA ENEO LA JANGWANI BAADA YA MVUA KUNYESHA
PICHA HIZZI MBILI ZINAONYESHA MADHARA YA MVUA ILIYONYESHA USIKU WA LEO HADI ASUBUHI JIJINI DAR ES SALAAM NA KUFUNIKA NYUMBA ZOTE ZA MAENEO YA JANGWAANI |
TAZAMA MAFURIKO MAENEO YA JANGWANI BAADA YA MVUA YA LEO
TAZAMA MAFURIKO MAENEO YA JANGWANI BAADA YA MVUA YA LEO
EXCLUSIVE---JUKWAA LA KATIBA LATANGAZA NIA YAKE YA KWENDA DODOMA KULIFUNGA BUNGE MAALUM LA KATIBA IWAPO TU-----------
Mjumbe wa jukwaa la katiba tanzania bw izrael ilunde akizungumza katika kutano huo na wanahabari juu ya uamuzi wa jukwaa la katiba kuhusu bunge la katiba tanzania |
Jukwaa la katiba Tanzania JUKATA
leo limetangaza nia yake ya kutaka kuwashawishi wananchi kuandamana hadi mjini Dodoma
kulifunga bunge la katiba endepo kama hawataridhika na bunge hilo na kama
watagundua kuwa wabunge hao hawana nia ya dhati ya kuwapatia katiba bora
wananchi.
Hayo yamesemwa leo muda huu jijini dar
es salaam na kaimu mwenyekiti wa jukwaa hilo bw HEBRON MWAKAGENDA wakati akizungumza na vyombo
mbalombalo vya habari kuhusu mwenendo wa bunge hilo maalum la katiba
linaloendelea mjini Dodoma.
Kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania bw HEBRON MWAKAGENDA akizungumza na wananchi muda mfupi uliopita kuhusu bunge la katiba |
MWAKAGENDA anasema kuwa jukwaa
la katiba linaendelea kutathmini kile kinachoendelea bungeni na kama
wakijiridhisha kuwa kinachoendelea hakielekei kuwapatia watanzania katiba mpya
bali ni upotevu wa muda na rasimali za taifa basi JUKATA itatumia ibara ya nane
ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwaongoza wananchi kulifunga
bunge maalum la katiba na kuanza harakati za kuitafuta katiba mpya kwa utaratibu wenye
mantiki na tija kwa taifa.
Aidha jukwaa la katiba Tanzania limeipinga
vikali hotuba iliyotolewa na raisi wa Tanzania dk JAKAYA KIKWETE wakati
akifungua bunge hilo ambapo wamesema kuwa
hotuba ile ilifaa sana kutolewa na mwenyekiti wa chama cha siasa kwenye
mkutano wa chama husika na sio katika bunge kama lile.
Bw MWAKAGENDA anasema kuwa jukwaa
la katiba linapenda kuwataarifu watanzania wote kwa ujumla kuwa katiba
inayotengenezwa sio ya chama chochote cha siasa bali ni y watanzania wote hivyo
ni kosa kwa chama cha siasa kuuteka mchakato huo kama wao ndo wanatengeneza
katiba yao ambapo anasema kitendo cha wanasiasa kuwa na sauti kubwa katika
bunge la katiba kimeufanya mchakato wote kutekwa na kuonekana kama mchakato wa
kisiasa.
Mchakato
wa bunge la katiba unaendelea huku kukiwa na mabishano maengi ambayo watanzania
wengi wamekuwa wakishindwa kuelewa ni ya nini hadi kufikia matumizi ya matusi
na vijembe kutawala katika bunge hilo
Subscribe to:
Posts (Atom)