YANAYOJIRI BUNGENI: NATAMANI KWENYE AMRI ZA MUNGU
IONGEZWE YA 11 ISEMAYO 'USIWE CCM' - KASEMA LEMA
Wabunge wanaendelea kuchangia taarifa za Kamati za Hesabu za Serikali PAC na
LAAC zinazoonesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma
Lema: Haiwezekani kila siku tukija humu tunazungumzia wizi tu, inatakiwa
tuzungumzie mipango ya maendeleo ya wananchi sio kila siku wizi wizi wizi
unaosababishwa na CCM.
Lema: Kama ningeweza kupendekeza pia kwenye Amri Kumi za Mungu, ningependekeza
iongezwe amri ya 11 inayosema 'USIWE CCM'
Lema: Katika mazingira kama haya, nathubutu kusema 'My Country is like a Getho'
mambo hayaendeshwi kwa utaratibu kabisa
Esther Bulaya: "Yani watu wanagawana posho Bilion 9, na wanafunzi wanasoma
kwa shida halafu mnataka tuwapigie makofi haiwezekani"
Esther Bulaya: "Hatuwezi kila siku tunakuja hapa majibu yaleyale kila siku
wizi wizi wizi, haiwezekani, hawa watu washughulikiwe"
Lissu: "Kinachotufikisha hapa ni Rais kushindwa kutimiza wajibu wake wa
kikatiba wa kuwawajibisha watendaji wake"
Lissu: "Tunachotakiwa kufanya hapa ni kuanza na hawa mawaziri tulionao
humu ndani, tukubaliane kuwawajibisha"