Thursday, April 30, 2015
HABARI NYINGINE KUTOKA HAI IKO HAPA
kaika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Ndg Antony Mtaka akizungumza katika uchaguzi wa wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe |
myenyekiti mpya wa bodi ya Maji ya Lyamungo Umbwe Michael Sitaki Mmasi |
Mhandisi wa maji wilaya ya Hai Eng. Nyakaraita Mwita akizungumza na wajumbe wa mkutano wa bodi ya Maji ya Lyamungo Umbwe. |
BODI YA AFYA WILAYA YA HAI YATOA RIPOTI YAKE OKTOBA 2010 HADI 2014 HAI
IMEELEZWA kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizopo katika hosipitali ya Wilaya ya Hai Bodi ya Afya wilayani hapo imeweza kufanya kazi ya kuziondoa changamoto hizo ili wananchi waweze kupokea humuda ya afya kwa njia stahiki.
Hayo yameelezwa hii leo na Mganga Mkuu Wa Hosipitali ya Wilaya Paul Chaote katika mkutano wa Bodi ya Afya ulio ambatana na uteuzi wa Mwenyekiti Mpya wa kuongoza Bodi hiyo kutokana na Mwenyekiti aliye kuwa madarakani kumaliza muda wake kutokana na utaratibu uliowekwa kumalizika.
Amesema kuwa Bodi ya afya ya Wilaya inayomaliza kipindi chake ilisimikwa na kuanza kazi rasmi mwezi oktoba mwaka 2010 lengo ikiwa ni kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu lakini kutokana na kuchelewa mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wapya,Bodi hii iliendelea kuwapo madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi.
Aliongeza kuwa Katika kipindi cha miaka minne bodi kwa kushirikiana na timu ya uendeshaji shughuli za afya pamoja na Menejimenti ya Halmashauri ilifanya mambo mbalimbali ikiwamo Kuongeza wigo wa huduma katika hosipitali ya wilaya kwa kufanya upanuzi kutoka majengo 7 mwaka 2010 hadi majengo 11 mwaka 2014.
Chaote aliongeza kuwa mambo mengine ni pamoja na Kufanya ukarabati katika vituo vya Afya na Zahanati,Kuongeza vituo vya hiduma toka 60hadi 62,Kufanya ziara elekezi za usimamizi katika hosipitali ya Wilaya nay a Machame,Vituo vya Afya na Zahanati na Kuingia mikataba 3 ya kiushirikiano kuendesha vituo vya makanisa ikiwa ni pamoja na hosipitali teule ya Machame.
Pia tumeweza ku Kufanya uhamasishaji wa mfuko wa afya ya jamii katika mikutano ya wananchi,mikusanyiko ya watu kama masokoni,makanisani na misikitini,katika shule za sekondari na kuongeza wanachama kutoka kaya 854 mwaka 2010 hadi kaya 5,028 mwaka 2014,Kufungua akaunti katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali.
"Ni jambo la kunivunia kuona kuwa licha ya changamoto nyingi zinazo jitokeza ndani ya hosipitali yetu na vituo vingine fya Afya bado Bodi ya Afya imeweza kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kuwaelimisha kuhusu bima za afya ili kila kaya iweze kupokea matibabu yaliyo bora kpitia bima ya Afya."Alisema Chaote.
Alisema kuwa mbali na mafanikio hayo yote pia wameweza kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchangiaji mdogo wa wananchi katika masuala ya mfuko wa afya ya Jamii ambapo lengo la kitaifa ifikapo disemba 2015 ni 30% wakati wilayaya Hai bado ni 10%tu,uchakavu wa majengo katika baadhi ya vituo,ukosefu wa huduma za maabara katika zahanati za Serikali ukosefu wa baadhi ya huduma muhimu katika Hosipitali ya Wilaya kama nishati mbadala wakati umeme wa Tanesco unapo katika.
"Tunaamini kwamba Bodi hii iliyo undwa itasimamia kamati zote zilizoko chini yake na itahakikisha kuwa huduma za Afya katika Wilaya yetu zitaboreshwa katika viwango vinavyopendekezwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Nina kuomba sasa uzindue rasmi Bodi hii ambayo itafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu."alisema Chaote.
HABARI KATIKA PICHA WAKATI WA UPIGAJI KURA WA KUCHAGUA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI MPYA YA MAJI HAI.
Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya ya hai Paul Chaote aliye simama akizungumza jambo wakati wa kikao cha kuchagua wajumbe wa Bodi ya Afya Wilaya. |
Wajumbe wa Bodi ya Afya Wilaya wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya Hai |
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Afya Wilaya katikati Bw Inocavity Swai akisikiliza maelezo mara baada ya upigaji kura kumalizika. |
KIMEELEWEKA--UKAWA WATOKA CHIMBO MUDA HUU,SOMA WALICHOAMUA SASA
Viongozi wakuu wa vyama vikuu vya upinzani UKAWA wakiwasili makao makuu ya CUF kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari leo |
Hatimaye viongozi wa vyama
vikuu vya upinzani vinavyounda UKAWA wameibuka
upya na kutangaza rasmi kutokuwa na kutokuwa na imani na tume ya taifa ya uchaguzi
nchini kwa kudai kuwa serikali ya chama cha mapinduzi inaitumia tume hiyo
kutaka kusogeza uchaguzi mbele kwa lengo la kujiongezea muda wa kutawala.
Akisoma maadhimio ya
umoja huo baada ya kukutana ndani ya siku mbli jijini Dar es salaam mwenyekiti
mwenza wa umoja huo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi mh JAMES
MBATIA amesema kuwa kutokana na hali ya hewa inayoendelea kuhusu sintofahamu ya
daftari la kupiga kura ni wazi kuwa sasa umoja wao hauna inami hata kidogo na tume
ya uchaguzi kwani imeonyesha wazi kuwa inashirikiana na serikali ya chama cha
mapinduzi kutaka kuhujumu uchaguzi ujao na kisha kuongeza muda wa uongozi wa
serikali hiyo kwa kisingizio cha kutokumalizika kwa uandikishwaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura.
Amesema kuwa tume ya
taifa ya uchaguzi hadi sasa ikiwa imesalia takribani miezi mitatu pekee kuanza
kwa kampeni rasmi za uchaguzi haijaanza wala hakuna dalili za maandalizi yoyote
ya kufanyika kwa uchaguzi huo jambo ambalo linazidi kuleta wasiwasi kwa
watanzania na kuamini kuwa kuna njama za kuahirisha uchaguzi huo kama ilivyofanyika
kwa daftari la kudumu la wapiga kura.
“kuna jambo
linashangaza sana,hadi sasa hakuna maandalizi yoyote yanayoashiria kuwepo kwa
uchaguzi huo ilihali imebaki miezi sita tu kufanyika kwa uchaguzi huo,hakuna
utaratibu wa vifaa vya uchaguzi huo,ambapo miaka iliyopita imekuwa ikifanyika
maadalizi mwaka mmoja kabla lakini uchaguzi huu hadi leo hakuna maandalizi ya
kuonyesha kuwa uchaguzi huo upo japo kuwa mwenyekiti wa tume hiyo anazidi
kuwdanganya watanzania kuwa uchaguzi huo upo”.aliseama mh MBATIA.
Naye mwenyekiti wa
CHADEMA mh FREMAN MBOWE amesema kuwa hakuna njia yoyote ya kuzia mabadiliko
ambayo yanataka kufanywa na ukawa kwa sasa hivyo tume hiyo isikubali kutumika
na serikali na badala yake ni lazima uchaguzi ufanyike mwaka huu kwa njiia
yoyote.
MGOGORO KUHUSU MAJIMBO
Wednesday, April 29, 2015
TIZAMA ALICHOKIFANYA DC MAKONDA LEO JIJINI DAR ES SALAAM
DK.SHEIN AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOA WA RUVUMA APRIL 29, 2015.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwasha mwenge wa Uhuru Kitaifa katika uwanja wa Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma leo(kushoto) Waziri wa Vijana Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara na Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa jamii vijana wanawwake na watoto Bi Zainab Mohammed.
UMESKIA NCCR KUJITOA UKAWA--TAARIFA MPYA HII HAPA
VIONGOZI wa Vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda (UKAWA) Vimekanusha Uvumi unaoenezwa na Vyombo vya Habari kuwa Miongoni mwa Chama cha siasa kinachounda umoja huo ambacho ni NCCR Mageuzi kwamba kimetoa hoja ya kujitoa kwenye umoja Huo, na kusema huo ni upotoshaji Wa Vyombo vya Habari ambavyo vinatumiwa na Chama cha Mapinduzi CCM.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kauli hiyo ya (UKAWA) inakuja ikiwa ,Gazeti la moja linalotoka kila siku Gazeti la Mtanzania toreo la leo Tarehe 29-mwezi wa nne mwaka huu bila ya kutaja chanzo cha uhakika kimeripoti Habari kwamba Vyama hivyo vikuu vya Upinzania vimeshindwa kufikia muhafaka kwenye ugawaji wa Majimbo na kudai kwamba Chama cha NCCR mageuzi kimepeleka hoja ya kujitoa kwenye Umoja huo.
WAZIRI WA MEMBE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON JIJINI DAR ES SALAAM
LHRC-SERIKALI IACHE MARA MOJA KUIPIGIA KAMPENI KATIBA PENDEKEZWA
Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA Akizngumza na wanahabri leo jijini Dar es salaam kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mchakato wa kura y7a maoni juu ya katiba pendekezwa |
Kituo cha sheria na
haki za binadamu nchini LHRC kimesema kuwa kitendo cha serikali kuanza kupiga
kampeni na kuwashawishi wananchi kuipigia katiba pendekezwa kura ua ndio ni ukiukwaji
mkubwa wa sheria na na kitendo ambacho kina
lengo la kiuvuruga mchakato mzima kwani serikali haina mamlaka ya kufanya hivyo
kisheria.
Mratibu wa katiba kutoka kituo hicho Bi ANNA HENGA akizngumzia mambo kadhaa ambayo wamekutana nayo walipokuwa nawazunguka katika mikoa mbalimbali kutoa elimu juu ya katiba pendekezwa |
Akizungumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es
salaam Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kituo
hicho kimekuwa kikifwatilia kwa ukaribu
kauli mbalimbali za viongozi wa serikali kuanzia kwa Mh Rais KIKWETE pamoja na
mawaziri mbalimbali ambapo wamekuwa wakiendelea kupiga kampeni ya kuwahimiza
wananchi kupiga kura ya ndio katika katiba inayopendekezwa.
WAISLAM WACHARUKA TENA,SOMA WALICHOKISEMA LEO JUU YA KAMATA KAMATA YA WAISLAM INAYOENDELEA NCHINI
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo SHEKH MUSSA KUNDECHA akizngumza wakati wa akitoa tamko hilo leo jijini Dar es salaam |
Wakati matukio
mbalimbali ya kukamatwa kwa viongozi na waislam nchini kwa sababu za
kujihusisha na ugaidi yakizidi kutokea Jumuiya ya taasisi za kiislam nchini Tanzania
wameibuka na kulaani vitendo hivyo vinavyofanywa na serikali kupitia jeshi la
polisi huku wakiitaka serikali kuwaomba
radhi waislaam kwa vitendo hivyo ambavyo wameviita ni vya uonevu na
udhalilishaji kwa waislam wote nchini.
Mapema leo akizungumza
na wanahabari mwenyekiti wa jumuiya hiyo SHEKH MUSSA KUNDECHA amesema kuwa
kumekuwa na matukio ya kamata kamata ambayo kwa viongozi wa kiislam,walimu wa
madrasa pamoja na watoto ambao wanasoma katika madrasa hizo vitendo ambavyo
amesema kuwa vinakiuka haki za binadamu,haki ya kikatiba,kisheria,na utu wa
mwislam huku amesema vitendo hivyo vinazidi kuchochea hasira kwa waialam hao na
kuhisi kwamba serikali ina mpango wa kuangamiza uislam nchini.
Amesema kuwa vitendo
hivyo vinavyoendelea katika mikoa mingi sasa nchini vinazidi kuwagawa
watanzania kwa misingi ya dini,na imani zao jambo ambalo amesema kuwa linaweza
kusababisha matatizo makubwa kama halitadhibitiwa huku awali.
Akitaja maeneo ambayo
kamata kamata hiyo imewathiri waislam wengi ni pamoja na mkoa wa Kilimanjaro ambapo
watoto na walimu wa madrasa wamekamatwa,mtwara,kilombero mkoani morogoro ambapo
watu waliingia msikitini saa tisa usiku na baada ya muda mchache polisi
wakaingia na kuwakamata jambo ambalo amesema bado linawapa shaka kuwa ulikuwa
ni mpango uliosukwa.
Naibu katibu mkuu wa Jumuiya na taasisi ya kiislam Tanzania, Rajab Katimba (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo |
Amesema kuwa hoja
inayoenezwa na serilakali kuwa wanazivamia madrasa kwa kuwa zipo kwenye hali duni
na hazina usajili haina maana kwa kuwa
hakuna sheria inayoonyesha jinsi na
vigezo vya kuzisajili huku akisema uduni wa madrasa hizo sio hoja kwani zipo
shule hadi wanafunzi wanakalia mawe lakini zimekuwa hazifungi wala kuvamiwa na
polisi.
Aidha amesema kuwa
kumekuwa na ugumu wa viongozi wao pindi wanapokamatwa na polisi kwa makosa kama
hayo ambayo ameita ya kusingiziwa ambapo swala la kuwapatia dhamana limekuwa ni
gumu sana na kinachofanyika ni kuwahamisha kutoka kituo kimoja kwenda kingine
huku wakiendelea kupatiwa mateso bila makosa ya msingi kutajwa.
Katika hatua nyingine
jumuiya hiyo imemtaka mkuu wa polisi nchini IGP,DPP,na kila kiongozi
anayehusika na utekelezaji wa matendo hayo kuchukua hatua za kujirekebisha na
kuacha kutekeleza uonevu huo dhidi ya waislaam.
Aidha amesema kuwa wao
kama waislaam wanaotetea waumini wao wamedhamiria kama ifikapo tarehe 15 mwezi ujao bila majibu sahihi ya
tamkio lao wamedhamiria kufanya maandamano ya amani kuishinikiza serikali
kuacha mara moja mpango huo ambao hauna tija kwa waislaam wala taifa kwa
ujumla.
Tuesday, April 28, 2015
VIDEO--HEBU TIZAMA ALICHOSEMA MBOWE KUHUSU HAWA RED BRIGADE NA MALENGO YAO
Kumekuwa na story inaendelea juu ya kikosi ambacho kinapewa mafunzo na chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA,maaarufu kama “Red Brigade” ambapo wadau mbalimbali wamekuwa wakikosoa kikosi hicho wengi wakidai kuwa ni kikundi ambacho kiinaandaliwa kufanya uhalifu wakati wa uchaguzi na mauaji wakati huo.,moja kati ya wada ambao wamekuwa wakilalamikia swala hilo ni msajili wa vyama vya siasa ambapo amekuwa akitishia hata kuwaadhibu CHADEMA kama hawatasitisha mpango huo.sasa hapa nimekuwekea video ya mwenyekiti MBOWE akizngumzia mafunzo hayo na lengo lake huku akipiga mkwara kwa wale ambao wanaulalamikia mpango huo |
WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA TAFFA OFISINI KWAKE,AWAAHIDI KUWAKUTANISHA KWA PAMOJA HIVI KARIBUNI
Waziri wa ushirikiano
wa Africa mashariki mh HARISON MWAKYEMBE amekutana Uongozi wa
wakala wa forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA),kwa
lengo la kukaa kwa pamoja na kujadili chamgamoto mbalimbali ambazo zinaikabili secta
hiyo katika nchi za Africa mashariki.
Akizungumza katika
,mkutano huo waziri mwakyembe amesema kuwa ameamua kukutana na wakala hao kutokana na mchango mkubwa walionao katika
kuinua uchumi wa nchi na amekuwa na mahusiano ya karibu na wakala hao tangu
akiwa waziri wa uchukuzi hadi sasa wizara ya Africa mashariki.
Waziri mwakyembe
amesema kuwa amekuwa akipokea kero nyingi za maswala ya uondoshwaji wa shehena
kutoka katika nchi za Africa mashariki na kuzitatua lakini ameshangaa kwanini Tanzania
wamekuwa wagumu kupeleka kero zao kwa waziri huyo jambo ambalo limemsukuma
kukutana na wadau kama hao ili kujua ni changamoto gani zinawakabili na jinsi
gani wanaweza kuzitatua kwa pamoja.
Waziri wa ushirikiano wa africa mashariki mh HARSON MWAKYEMBE akizngumza na Uongozi wa wakala wa forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA) alipokutana nao ofisini kwake jana kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika shughuli zao |
Wakizungumza na waziri
huyo viongozi wa TAFFA wameonyesha kutokuwa na imani na mamlaka ya mapato Tanzania
TRA kwa kile walichokiita ukiritimba uliokithiri juu yao wanaofanyiwa na mamlaka
hayo ikiwemo dharau pamoja na
kutosikilizwa keri zao jambo ambalo waziri MWAKYEMBE amesikitishwa nalo na kuahidi
kulifanyia kazi mara moja
Aidha wakala hao
wamelalamikia mfumo mbovu wa utoaji wa leseni kwa ajili ya kufanya kazi zao
ambao kwa sasa leseni kwa wakala hao zimekuwa zikitolewa kwa mwaka mmoja jambo
ambalo wamedai ni kero kwao kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi sana katika
kufwatilia leseni kuliko kufanya kazi za kampuni zao jambo ambalo pia waziri
mwakyembe ameahidi kulisimamia kwa kina kuhakikishakuwa miaka ya leseni ya kazi
zao inaongezwa ili kuwapa unafuu wao katika kufanya kazi zao.
Katika mkutano huo
baada ya kuonekana wazi kuwa wakala hao wana changamoto nyingi za kuzungumza
waziri MWAKYEMBE aliahirisha mkutano huo na kuahidi kuwakutanisha tena siku za
karibuni kujadili kwa kina changamoto zinazowakabili ambapo mkutano huo unatarajiwa
kujumuisha wadau wengine wengi akiwemo waziri wa fedha pamoja na wadau kutoka
mamlaka ya mapato Tanzania TRA.
NYALANDU -AKUKAGUA VIFAA MBALIMBALI VILIVYONUNULIWA NA TAASISI YA BUFFET FOUNDATION
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikagua gwaride la heshima jana alipowasili Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya kompyuta maalum zinazotumiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
WAZIRI KIVULI WA FEDHA, JAMES MBATIA AZUNGUMZIA KUPOROMOKA KWA THAMANI YA SHILINGI TANZANIA
Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia.
Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
SOMA ORODHA YA VILABU VILIVYOLIMWA FAINI NA TFF LEO,NA WAMUZI WALIOFRUNGIWA HAPA
VILABU VPL VYAPIGWA FAINI, WAAMUZI WAFUNGIWA
Ruvu Shooting imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kuzingatia Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo (changing room) katika mechi namba 149 dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga
Pia Ruvu Shooting imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.
Stand United imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya washabiki wake kuwatupia chupa za maji wachezaji wa akiba wa timu ya Polisi Morogoro katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu.
MALINZI AWAPONGEZA YANGA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Yusuf Manji kufuatia timu yake kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Katika salamu zake za pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo muhimu na sasa wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya kimataifa barani Afrika mwakani.
Monday, April 27, 2015
VIDEO--KIMENUKA TENA--ZITTO YALE YALEE YA KULE,ATUHUMIWA KUPORA CHAMA NA KUJIMILIKISHA MWENYEWE.MSIKILIZE HUYU
Katika hali ambayo sio ya kawaida na ya kushangaza mwenyekiti za zamani wa chama cha ACT TANZANIA ameibuka na kusema kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho kwa sasa mh ZITTO kabwe amekipora chama hicho mikononi mwake kinyume na sheria na hastahili hata kuwa kiongozi wa chama hicho.mwenyekiti huyo anadai kuwa kitendo cha ZITTO KABWE kubadili jina la chama hicho pamoja na nembo
MABADILIKO HAYO YANAYOLALAMIKIWA YAKO HIVI-----
Wadau kama mnakumbuka Chama cha ACT-Tz kilibadilisha jina na kuwa ACT wazalendo mabadiliko yaliyofanyika machi 28 kwa kupitishwa na mkutano mkuu wa kwanza
Kamati ya mabadiliko ya katiba ilitoa maelezo juu ya taratibu zilizo tumika kufikia mabadiliko na maboresho ya katiba ya cham ikiwa ni pamoja na ufafanuzi ya juu ya mabadiliko yalifanywa kwenye katiba inayopendekezwa kama ifuatavyo
1 Jina la chama litakuwa ACT-WAZALENDO Badala ya ACT-TANZANIA
2 Herufi T katika neno ACT liwe na nembo ya taifa bendera ya Tanzania
3 Alama ya mkono iashirie uwazi na ukweli
4. Makao makuuu ya chama yawe dareesalaam na ofisi ndoga za makao makuuu ziwe mwanza na Zanzibar
5 Kuwepo na misingi kumi ya chama ambayo imeanishwa katiba katiba ya chama
KAMATA KAMATA DAR-WAZUNGU WAWILI WADAKWA KWA UTAPELI.SOMA HII
RAIA
WATATU WA KIGENI WAKAMATWA KWA MAKOSA YA WIZI WA MTANDAO KATIKA MABENKI JIJINI
DAR ES SALAAM.
Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu raia wa kigeni kwa makosa
yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa lengo la kuiba katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka
ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha
zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi.
Polisi wa kikosi Maalum
cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime) walipata taarifa za kuaminika
kwamba watu hao watatu walikuwa katika mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo
Polisi walienda Mtaa wa Mindu eneo la Upanga na kuwakamata. Watu hao walikutwa
katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa
majina yafuatayo:
1. FOTIOS
S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini
UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.
2. ATHANASIOS
S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki
mwenye Passport namba AK3049876.
3. PANAGIOTIS
S/O ANGELIDIS, Miaka 25, Mkazi
wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.
Watu hao watatu ambao
ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba wamekuwa wakiingia
na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya katika
namna ambayo inaonyesha kuwa ni wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.
Katika upekuzi watu hao
wamekamatwa na vielelezo mbalimbali vinavyopashiria njama zao kama ifuatavyo:
1.
Muhuri mmoja wa kughushi ulioandikwa
“Inspector General of Police DSM”
MALINZI AFUNGUA KOZI YA WAKUFUNZI
Picha na maktaba |
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi leo amefungua kozi ya walimu wakufunzi wa mpira wa miguu chini inayofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Malinzi amesema kozi hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa soka la Tanzania, walimu wakufunzi watasaidia kuwafundisha walimu wengine wa mpira, ili kuweza kufundisha mpira kwa watoto wadogo ambao ndio hazina ya baadae.
Sunday, April 26, 2015
DC MAKONDA AENDELEA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA WILAYA YAKE SAFARI HII NI KATA YA WAZO
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwahutubia wakazi wa Mtaa wa Kilimahewa Juu iliyopo uliopo Kata ya Wazo Dar es Salaam jana, alipofika kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu muda mrefu.
DC Makonda akizungumza na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni na wakata ya Wazo kuhusu mgogoro huo.
PICHA --YALIYOJIRI SHEREHE ZA MUUNGANO LEO DAR ES SALAAM
TIZAMA MBUNGE NASSARI NA SALUM MWALIM WAKIWA MAKAMBAKO WALICHOKIFANYA
Saturday, April 25, 2015
MBOWE HUKO UKEREWE NI HISTORIA NYINGINE--PICHA ZIKO HAPA
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mongella mjini Nansio wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. |
Mbowe akisalimiana na mlemavu wa viungo alipowasili kwa chopa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mongella mjini Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)