Monday, August 31, 2015
GLOBAL PEACE FOUNDATION, TAWI LA TANZANIA KUHAMASISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Viongozi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha amani nchini Tanzania katka kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda na kushoto ni Ofisa Utawala wa GPFTZ, Hilda Ngaja.
Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (kushoto) na Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda, wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
Ofisa Utawala wa Shirika hilo, Hilda Ngaja (kushoto) na Balozi wa Amani wa GPF, Dk.Ulimwengu (kulia), wakionesha kipeperushi kinacho hamasisha kushiriki uchaguzi kwa amani.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………
DR. MAGUFULI AITIKISA SONGEA, AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli amewaambia wananchi hao kuwa anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Amesema pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
Amesema ataongeza zaidi kasi yake katika utendaji tofauti na alipokuwa Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa akichaguliwa na watanzania kuwa rais yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
Dr John Pombe Magufuli pia alitembelea na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumba ni kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SONGEA)
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu John Damiano Komba katika kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni Mjumba wa Kamti kuu ya CCM Ndugu William Lukuvi.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John Komba huko Lituhi mkoani Ruvuma.
Picha 14--Tizama Lowasa alivyopeleka mafuriko yake Njombe leo,aweka historia mpya
STARS YAMALIZA KAMBI UTURUKI
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro chini ya Kocha wake Mkuu Charles Boniface Mkwasa imefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe – Kocaeli nchini Uturuki.
TASWA FC, TASWA QUEENS WAMALIZA ZIARA YAO YA MKOA WA ARUSHA NA TANGA BILA KUFUNGWA, TASWA QUEENS WAIBUKA MABINGWA WA BONANZA LA TASWA ARUSHA
Kikosi cha Taswa Fc |
Hussein Omari na Imman Makongoro wa Taswa Fc na Taswa Queens, wakifurahia baada ya kukamata Kuku katika mchezo wa kukimbiza kuku kwenye Bonanza la 10 la Taswa Arusha mwishoni mwa wiki jijini Arusha. |
Mchezaji wa Taswa Queens, Oliver Arbogasti, akimiliki mpira wakati wa mchezo wao na timu ya Chuo cha Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC. Katika mchezo huo Taswa Queens, ilishinda mabao 37 - 3. |
Sunday, August 30, 2015
AISEE--Umeona hii ya ukawa shinyanga mjini,unaweza kutizama sasa
Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako maelfu ya wakazi wa Shinyanga wamefurika katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mkuu ujao wilaya ya Shinyanga hususani jimbo la Shinyanga Mjini.Mkutano huo umeongozwa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema ndugu Patrobas Katambi maarufu kwa jina la "Mzimu wa Shelembi".
Viongozi wengine machachari waliohudhuria mkutano huo ni mgombea ubunge kupitia Chadema jimbo la Kahama mjini mheshimiwa James Lembeli,mgombea ubunge jimbo la Kishapu Fred Mpendazoe na mgombea ubunge jimbo la Msalala kupitia Chadema ndugu Paul Malaika.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog Kadama Malunde, alikuwepo eneo la tukio ametusogezea picha 38,Angalia hapa chini
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Ukawa/Chadema katika jimbo la Shinyanga
Lowasa aanza kazi-Tizama alichokifanya mkoani Iringa
Tizama jinsi wasanii hawa walivyojitokeza jana kwenye kampeni za UKAWA
Saturday, August 29, 2015
Soma kwa umakini Hotuba hii ya LOWASA aliyoitoa leo,
HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA
YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Sasa hapa yapo maneno yoote waliyotoa wazungumzaji waliozungumza leo pale jangwani,unaweza kuyasoma hapa
9:31 Mchana: Edward Lowassa akiwa na mgombea mwenza Haji Duni wanaingia kwenye viwanja vya Jangwani wakiwa kwenye gari la wazi.
9:43 Mchana: Lowassa amefika meza kuu na kuketi, meza kuu pia wamo Maalim Seif, Duni, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Salum Mwalim na wengineo.
9:48 Mchana: Sasa ni muda wa viongozi wa dini kuomba dua, Said Riko kwa niaba ya dini ya Kiislam anaomba dua na atafata mchungaji Gwajima kwa upande wa dini ya kikristo kuongoza sala kwa niaba ya wakristo.
9:56 Mchana: Baada ya dua, kilichopo kwa sasa ni wimbo wa taifa
Salum Mwalimu(9:59): Tunakutana hapa kwa sababu ya mambo mawili, jambo la kwanza kuzindua rasmi kampeni zetu. Jambo la pili ni kuzindua ilani yetu ya uchaguzi mkuu, japokuwa inazinduliwa na CHADEMA inaungwa mkono na vyama vyote vilivyo kwenye UKAWA.
U-15, MORO KOMBAINI ZATOKA SARE
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa 15 leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Moro Kids Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mchezo wa kirafiki.
VIJANA WATANO U-15 WAELEKEA AFRIKA KUSINI
Wachezaji watano kutoka katika kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) wanaondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea nchini Afrika Kusini katika klabu ya Orlando Pirates kwa ajili ya kufanya majaribio.
Tizama mabango niliyokutana nayo leo pale jangwani
Mafuriko ya Lowasa yazua makubwa jangwani,wengi wazimia kwa kukosa hewa
Friday, August 28, 2015
Tizama majumuisho ya ziara ya lowasa Dar es salaam leo
Msanii Juma Nature A.k.a Kibla akiongoza wasanii wenzake kuwasalimia viongozi wa UKAWA leo Ijumaa 28/08/2015 ikiwa ni majumuisho ya ziara ya Mgombea Urais Mhe. Lowassa kwa jiji la Dar es salaam |
Nimekuwekea mambo muhimu aliyoyazungumza ZITTO KABWE leo Jijini Dar es salaam
Chama cha ACT wazelendo
leo kimenza mafunzo ya siku mbili mfululizo kwa wagombea wake wa nafasi za
ubunge nchini mafunzo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo na kujiamini zaidi kuelekea
kufanya kampeni na kutafuta nafasi za uwakilishi wa katika majimbo mbalimbali
kikiwa ni chama pekee nchini Tanzania kulichoendesha mafunzo kama hayo kwa
sasa.
Kiongozi mkuu wa chama
hicho ZITTO ZUBER KABWE akizungumza na wanahabari wakati wa mafunzo hayo amesema
kuwa chama hicho ni chama pekee nchini Tanzania kilichodiriki kuwapa mafunzo ya
kuelekea katika uchaguzi ili kuwaweka katika mstaari mmoja wa kuhakikisha kuwa
wanakwenda na lugha moja kwa watanzania kueleza mipango na ilani ya chama
hicho.
ZITTO KABWE akiendelea kutoa mafunzo kwa wagombea ubunge zaidi ya 90 walioshiriki katika mafunzo hayo |
ZITTO KABWE anasema
kuwa chama cha ACT wazalendo ndio chama pekee nchini Tanzania ambacho kina
agenda maalum kwa watanzania tofauti na vyama vingine ambavyo amesema kuwa
vinatumia mbwembwe na ulaghai kwa watanzania bila kuweka wazi nini wanataka
kuwafanyia watanzania.
Kauli za Rais MKAPA sasa zaibua mengine,TACCEO waibuka na kusema haya
Ikiwa ni siku chache Tangu
Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh BENJAMIN MKAPA
kutoa kauli ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kuwa ni lugha
chafu, sakata hilo limeanza kuchukua sura mpya baada ya wadau mbalimbali kuanza
kujitokeza kulaani na kupinga matumizi ya lugha kama hizo katika kampeni za
uchaguzi wa mwaka huu.
Mtandao wa asasi za
kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO wamekuwa wa kwanza kuibuka
na kulaani vikali vitendo hivyo ambavyo wamedai kama tume ya uchaguzi na vyombo
husika vitafumbia macho vinaweza kusababisha machafuko na chuki kwa watanzania.
Akizngumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam HELLEN KIJO BISIMBA kwa niaba ya
nmwenyekiti wa TACCEO amesema kuwa matumizi ya lugha za kejeli,dharau,na
vijembe katika kampeni yataleta chuki na hatimaye kupelekea uvunjifu wa amani
jambo ambalo lazima wanasiasa wawe makini wanapokuwa majukwaani kuepuka
kuwagawa watanzania na kuwapandikiza chuki.
Baadhi ya wanabari wakichukua Taarifa hiyo |
Subscribe to:
Posts (Atom)