Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi wa kambi ya JKT Ruvu baada ya kupanda miti. Picha na OMR |
Saturday, May 31, 2014
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI KATIKA KAMBI YA KIKOSI CHA JESHI LA KUJENGA TAIFA RUVU.
HABARI ILIYOTIKISA JIJI---RAIS KIKWETE ATAJWA KUHUJUMU MCHAKATO WA KATIBA MPYA,WANANCHI WASEMA AMEWASALITI.SOMA KIUNDANI HAPA
Wachokoza mada katika mdahalo huo ambao umemalizika muda mchache uliopita,mwanzo ni awadhi ally,Ayubu Rioba,Onesmo olenguruma,na Mwesiga baregu |
Na Karoli Vinsent
WANANCHI mbalimbali wamtaja Rais Jakaya
kikwete kuwa ni kikwazo kikubwa cha upatikanaji wa Katiba Mpya ,kutokana na
kushindwa kusimammia misimamo yake mwanzo ambayo ilikuwa inamalengo ya
kupatikana katiba mpya ya Wananchi.
Hayo,yamegundulika mda huu kwenye
Mdahalo wakujadili Katiba mpya,uliondaliwa na Umoja wa Asasi za kirai
(AZAKI)uliofanyika jijini Dar es Salaam,mdahalo huo ambao uliwahusisha Wananchi
wa Kawaida pamoja na Wasomi Mbalimbali.
Katika Mdahalo huo wananchi wameonekana
Dhahiri kumshutumu Rais jakaya Kikwete kwakushindwa kusimamia misimamo yake ya
mwanzo ambayo ilikuwa inalengo la kupatikana Katiba mpya ya
Wananchi bila Upendeleo,ambapo sasa ameonekana kubadilika na kuanza
kushikilia Misimamo yake ya Chama cha Mapinduzi CCM, ambayo inakuwa
kinyume na sasa.
Watanzania waliojitokeza katika mdahalo huo |
Kwa upande wake Msomi na mchambuzi wa
Masuala ya kisiasa Nchini kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Profesa
Mwisiga Baregu.alisema Rais kikwete amefanya usaliti mkubwa sana kwa wananchi
kwa kitendo chake kuanza kufuata maoni ya chama chake.
“Kiukweli mimi
sikutegemea Rais kikwete angefanya usaliti namna hii kwenye mchakato huu
wakatiba, wakati mimi sikutegemea .Kwanza wakati kila hatua tuliyokuwa
tunaifanya kwenye mchakato huu wakatiba tulikuwa tunamjulisha halafu na yeye
alikuwa anaungana na sisi kwa kazi tuliokuwa tuanafanya”
“Lakini tunashangaa yeye amebadilika na
kuanza kufuata misimamo ya chama chake,na huku ndiko alipoanza kuharibu
mchakato mzima wa ujio wa Katiba mpya.Alisema Baregu.
Baregu,ambaye ni Kada
kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,alizidi kusema kitendo cha
wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Chama cha Mapinduzi CCM.
Kuendelea kujadili
Rasimu ya Muundo wa Serikali mbili ni kuvunja kanuni ya mabadiliko ya katiba
kifungu cha 25,ambacho kinataka wajumbe wa Bunge hilo kutojadili Rasimu ya
Kwao.
Kwa Upande wake
Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Nchini,Deus Kibamba,aliwataka wananchi
kushirikiana na AZAKI ,kutetea katiba yao na kutowaacha wanasiasa kuhodhi
mchakato mzima wa Katiba.
Vilevile Mwanasheria
na mwenyekiti wa chama cha Wanasheria Zanzibar Hawadhi Ally, ambapo yeye
alikuwa miongoni mwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,alisema
Rais Jakaya Kikwete ndio mtu wa kulaumiwa kwa wananchi kwa kitendo chake cha
kuanza kufuata matakwa ya Chama chake ambao wamekuwa kinara wakubwa wakipinga
maoni ya tume ya Jaji warioba.
Mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania Deus Kibamba akitoa maoni yake kama mwananchi katika mdahalo huo uliomalizika muda mfupi uliopita |
Naye Mwenyekiti wa
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali,inasimamia Muenendo wa Shuguli za Bunge
nchini,Marcus Albanile,aliwataka wananchi kuacha upole wa kuigopo Serikali ya
Rais Kikwete, ambayo imekuwa hikihalibu mchakato wa katiba mpya na
akawataka wananchi kuandamana na kulala barabarani na kudai katiba mpya.
Ikumbukwe, Midahalo
hii ya kuwapa wananchi fursa ya kujadili katiba mpya imeandaliwa na Umoja Asasi
zisizokuwa za Kiserikali AZAKI,ambao umoja huo unawakilisha Asasi hizo
zaidi ya mia tano.
Friday, May 30, 2014
KITUO CHA DALADALA MWENGE KUFUNGWA RASMI JUMAPILI HII YANI KESHO
Wamiliki, madereva na abiria wote mnatangaziwa kuwa kituo cha daladala Mwenge kitafungwa rasmi siku ya Jumapili jioni tarehe 01.06.2014. Kuanzia siku ya jumatatu asubuhi tarehe 02.06.2014 kituo kitakachokuwa kinatumika ni Makumbusho tu.
BREAKING NEWZZ : GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI MKOANI MOROGORO--TZAMA PICHA ZA GARI LAO NA PICHA ZAO KABLA YA AJALI--R.I.P TYSON
Muongozaji mkongwe wa filamu nchini Tanzania mwenye asili ya Kenya, George Tyson amefariki Dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari wakati wakitokea kwenye hafla ya kuadhimisha miaka miwili ya kipindi cha luninga cha The Mboni Show mkoani Dodoma kufuatia gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Noah kupasuka matairi na kuangukaeneo la Gairo mkoani Morogoro majira ya saa moja jioni.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kurudi Dar es Salaam
Awali Tyson aliwahi kuwa mume wa muigizaji nyota wa kike wa Bongo Movie, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ aliyeza nae mtoto mmoja wa kike anayeitwa Sonia.
Atakumbukwa kwa ucheshi, ukarimu na busara zake, Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema peponi Ameen.
Gari alilopata nalo ajali Director George Tyson na picha za saa 4 kabla ya tukio
KAMA ULISKIA ILE STORY YA KATIBU MKUU WA CCM KINANA KUGOMBEA URAIS MWAKANI--UNDANI WAKE HUU HAPA
Na Karoli Vinsent
KATIBU
wa chama cha Mapinduzi CCM,Abdulrahman
Kinana,anatarajiwa Kugombea Urais kwenye Uchaguzi mkuu mwakani 2015.
Taarifa hizo
ambazo Mtandao huu umedokezwa,zinasema kitendo cha Katibu mkuu huyo
kuingia kwenye Kinyanganyiro hicho zinalenga Kuwanyamazisha Makada mbalimbali
ndani ya Chama hicho ambao wamekuwa wakitumia kila Njia kuhakikisha wanashika
nafasi hiyo ya Urais kwenye uchaguzi mkuu mwakani.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA CHI ZA NJE WA UTURUKI
HALFA YA KUKABIDHI MTAMBO WA MFUMO WA MAWASILIANO WA MASAFA MAREFU KWA JESHI LA MAJI YAFANYIKA
Balozi wa Marekani Nchini Lt.Kevin Balisky akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima wakati wa halfa ya kukabidhi mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa jeshi la maji, masaada huo umetolewa na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa AFRICO,leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Silima (kulia) akizindua mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa kikosi cha askari wa maji katika halfa iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Balozi wa Marekani nchini, Lt. Kevin Balisky,mtambo huo umetolewa na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa AFRICO kwa ajili ya kusaidia kudhibiti uhalifu wa majini na kuweza kutambua vyombo na shughuli zote zitakazofanyika katika maji.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Silima (kulia) akizindua mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa kikosi cha askari wa maji katika halfa iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Balozi wa Marekani nchini, Lt. Kevin Balisky,mtambo huo umetolewa na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa AFRICO kwa ajili ya kusaidia kudhibiti uhalifu wa majini na kuweza kutambua vyombo na shughuli zote zitakazofanyika katika maji.
KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA NCHI WASHIRIKA WA MAENDELEO JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akibadilishana mawazo na mabalozi na wawakilishi wa nchi washirika wa maendeleo kabla ya mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika mazungumzo na mabalozi na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo katika mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika mazungumzo na mabalozi na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo katika mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
PICHA NA IKULU
BANK YA POST YAINGIA MAKUBALIANO NA SIMBA NA YANGA MCHANA HUU,CHEKI PICHA HAPA--RAGE AONEKANA
Tutashirikiana |
JUKATA WATOA TATHMIN YAO JUU YA UCHAGUZI WA MALAWI NA AFRICA YA KUSINI.SOMA HAPA
Mwenyekiti wa JUKATA DEUS KIBAMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam |
Jukwaa
la katiba Tanzania JUKATA leo limetoa tathmini yake juu ya chaguzi mbili zilizofanyika katika
nchi za Malawi na Africa ya kusini mwezi uliopita huku wakionyesha kuipongeza
sana nchi ya Africa ya kusini kwa kufanya uchaguzi wa haki na huru tofauti na
nchi ya Malawi
Akizungumza
leo jijini dare s salaam mwenyekiti wa jukwaa
hilo DEUS KIBAMBA amesema kuwa wao kama jukwaa waliweka kambi katika
nchi hizo mbili,kwa lengo la kuangalia uchaguzi huo
Kaimu mwenyekiti wa jukata HEBRON MWAKAGENDA |
KIBAMBA
anasema kuwa ni wazi kuwa hali ya nchi hizo mbili kiuchumi ni tofauti sana
jambo ambalo pia limechangia kufanya chaguzi zao pia kutofautiana sana,ikiwa ni
pamoja na tume ya uchaguzi ya Malawi kuonyesha kuwa haikuwezeshwa kiswasawa
katika kusimamia uchaguzi huo jambo ambalo nchini Africa ya kusini halikuwa
hivyo.
“Tume
ya uchaguzi ya Africa ya kusini imeonyesha kuwajali sana wapiga kura hadi
kufikia hatua ya kuwajali walemavu ambao wasingeweza kufika vituoni na
kuwafwata walipo ili wapige kura.”amesema KIBAMBA
Kuhusu hamasa ya wananchi ya kupiga kura
JUKATA wamesema kuwa wananchi wa Africa ya kusini walikuwa na hamasa sana
tofauti na wale wa Malawi jambo ambalo limechangiwa na hamasa pia iliyofanywa
na serikali kwa ujumla.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini |
Akizungumzia
swala la rais wa Malawi kufuta matokeo
na kutangaza uchaguzi kurudiwa JUKATA
wamesema kuwa wameshangazwa sana na hali hiyo ambapo wameipongeza sana mahakama
ya nchini Malawi kwa kuonyesha ukakamavu wao katika kupingana na matakwa ya
rais banda na kuamuru matokeo yahesabiwe tena ambapo amesema kuwa kama hilo
lisingefanyika basin chi ya Malawi ingeingia katika machafuko makubwa sana.
Thursday, May 29, 2014
EXCLUSIVE--BAADA YA JANA KAMBI YA UPINZANI KUMTUHUMU ZITTO KABWE KWA UFISADI MKUBWA TANAPA NA NSSF,SASA ZITTO AMEJIBU,SOMA MANENO HAYA YA ZITTO HAPA
Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma
AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.
Leo tarehe 29 Mei, 2014 Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni amenituhumu kuhusika na kinachoitwa ufisadi katika Shirika la TANAPA na NSSF.
Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka. Kwa sasa nitatoa maelezo kwa ufupi ili kuondoa upotoshaji.
Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii 15 ambapo kila mmoja ana hisa 5% ambazo niliwalipia ili waweze kushirikiana katika kazi zao. Hisa 25% zilizobakia zinamilikiwa na kampuni ya Gombe Advisors ambayo ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara (not for profit company). Hivyo Mimi binafsi sina maslahi yeyote ya kifedha zaidi ya kuwasaidia wasanii hawa katika kazi zao mbalimbali.
HABARI ILIYOWAHUZUNISHA WATANZANIA WENGI LEO--MSANII RECHO AAGWA VIWANJA VYA LEADERS KATIKA PICHA
Sehemu lilipowekwa jeneza la msanii Recho. |
habari kuu toka bungeni----HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
Mheshimiwa Spika, napenda
kuchuku nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema na kwa kunitumia
kama chombo cha mabadiliko hasa katika kutetea haki za wanahabari, vijana,
wanamichezo na wasanii. Namshukuru Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Mhe.
Freeman
TP MAZEMBE YAWAACHIA SAMATTA NA ULIMWENGU KUJA STARS
SAMATA, ULIMWENGU KUIONGEZEA NGUVU STARS
Klabu ya TP Mazembe imewaruhusu wachezaji wake Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu kujiunga na timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo tayari imewasili Harare, Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika.
Taifa Stars itacheza na Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mechi ya marudiano raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare.
Samata na Ulimwengu watawasili Harare kesho (Mei 30 mwaka huu) saa 3.40 usiku kwa ndege ya Kenya Airways. Watajiunga na TP Mazembe mara baada ya mchezo huo ambapo Juni 2 mwaka huu watakwenda moja kwa moja Ndola, Zambia ambapo timu yao imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, MHE. DKT. FENELLA E. MUKANGARA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015
A. UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa
iliyowasilishwa leo kwenye Bunge
2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda
kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kunipa nguvu ya
kutekeleza majukumu yangu na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu
kuwasilisha bajeti hii.
MBEYA CITY FC WATINGA ROBO FAINALI YA CECAFA NILE BASIN CUP MJINI KHARTOUM
MBEYA City imetinga Robo Fainali za michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea nchini Sudan baada ya sare ya bila kufungana na Enticelles ya Rwanda usiku wa jana katika Uwanja wa Khartoum.
Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City imalize hatua ya makundi kwa kujikusanyia pointi nne baada ya mechi tatu, lakini ipo katika nafasi ya pili nyuma ya miamba ya soka nchini Kenya, AFC Leopards walioongoza kundi kwa pointi 9.
Mchezo wa mwingine wa usiku, AFC Leopard walishinda bao 1-0 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi na kushinda kwa asilimia 100 katika kundi lao.
Wednesday, May 28, 2014
kama ulikosa---WANACHAMA WA SIMBA WAANDAMANA NA KUFUNGA NJIA ZA MSIMBAZI WAKITAKA WAMBURA ARUDISHWE KWENYE ORODHA YA WAGOMBEA
Mashabiki wa Timu ya simba wakijikusanya nje ya jengo la klabu hiyo kongwe kupinga wambura kuondolewa kwenye uchaguzi unakuja hivi karibuni
Hapa mashabiki wakizidi kujikusanya kwa wingi mchana huu
Subscribe to:
Posts (Atom)