Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA), Burchard Rwamtoga (wa pili kushoto), akimkabidhi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),moja ya ufunguo wa gari kati ya magari manne na pikipiki 20 vyote vikiwa na thamani ya sh.261,105,615, Dar es Salaam leo, zilizotolewa na shirika hilo kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupambana na magonjwa hayo nchini. Wanashuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Palanjo na Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe.
Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe (wa pili kulia), na viongozi wengine wa wizara hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Charles Palanjo, Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando na Mkurugenzi Msaidizi Afya na Usafi wa Mazingira, Elias Chinamo.
Pikipiki zilizotolewa kwa serikali.
Magari yaliyotolewa kwa Serikali.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Dk. Deus Leonard katika hafla hiyo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid akijaribu kuwasha moja ya magari hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid(kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Kitabibu wa Ilala, Dk.Mbarouk Seif.