Friday, April 3, 2015

VIJANA WA CHADEMA WAPO NJIANI WANAENDA BUTIAMA,SOMA KINACHOWAPELEKA HUKO



Baadhi ya vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kutoka wilaya  za Nyamagana, Magu, Busega na Bunda wameanza matembezi ya siku sita  kuelekea katika kijiji cha Butiama kwenye kaburi la hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa lengo la kuwahamasisha watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa  ajili ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajia  kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Thursday, April 2, 2015

MAGAZETI YA LEO IJUMAA KUU

UMESOMA MANENO YA BUSARA YA NASSARI BAADA YA UCHAGUZI WA NIGERIA

Nimependa sana ukomavu wa kidemokrasia wa Goodluck Jonathan na mpinzania wake Jenerali Buhari na wafuasi wao. Uchaguzi umeisha kwa amani na aliyeshindwa ameshindwa na kukubali bila hila zozote!
****
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria,INEC, Attahiru Jega amemtangaza rasmi Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari kuwa Rais wa taifa hilo kubwa barani Afrika baada ya kumbwaga rais wa zamani Goodluck Jonathan.

Tayari rais anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan amekwisha kubali kushindwa kwake baada ya kumpigia simu mpinzani wake, Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.
Ni vyema wenzetu wa ccm hususani wale wanaoamini kuwa wana hati miliki ya kutawala milele wakajifunza. Mjiandae kisaikolojia kwa lolote litakalotokea mwezi Oktoba mwaka huu.
TEAM UKAWA

KUTOKA TFF LEO HIZI NDIZO HABARI KUBWA


TWIGA STARS KUIVAA SHE-POLOPOLO

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) ijumaa ya tarehe 10, Aprili  mwaka huu, itashuka dimbani  Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakarisbisha timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (The She-Polopolo).

Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage iliingia kambini mwishoni mwa wiki na kikosi cha wachezaji 25 katika hostel za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za michezo ya Afrika mwaka huu.

Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Lusaka Zambia, Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, mabao yaliyofungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).

Mshindi wa jumla katika mchezo huo atafuzu moja kwa moja kwa fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanya nchini Congo - Brazzavile kuanzia Septemba 13 mwaka huu.

COASTAL YAIPIGIA HESABU PRISON, YAWEKA MIPANGO YA KUHAKIKISHA POINTI TATU ZINABAKI MKWAKWANI


Timu ya Coastal Union ameanza kuzipigia hesabu pointi tatu muhimu zawapinzani wao Tanzania Prison ili kuweza kuhakikisha wanazichukua
wakati watakapokutana kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani ikiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo ikielekea lala
salama.

Akizungumza leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo
yanayo endelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini
hapa,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kikubwa zaidi
wanachojivunia ni kuendelea kuimarika kikosi hicho.
 Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga,Jamhuri
Kihwelu "Julio"amimnyajua chini mlinda mlango wa timu hiyo,Shabani
Kado jana mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo.



Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuiwezesha timu hiyo kupata
matokeo mazuri katika mechi zote zilizosalia ikiwemo kuwataka
wachezaji kutimiza wajibu wao wa kuipa ushindi timu hiyo.

Amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kupambana kufa na kupona ili
kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi tatu za juu kwenye michuano hiyo
ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.

Hata hivyo amewataka mashabiki pamoja na wapenzi kujitokeza kwa wingi
katika michezo yao iliyosalia ikiwemo ya ugenini na nyumbani ili kuipa
hamasa timu hiyo kufikisha malengo yao.



NEWZZ--HAKUNA KURA YA MAONI TANZANIA


Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)imetanga rasmi kuhairisha kura maoni juu ya  Katiba inayopendekezwa ambayo ilitarajiwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu mpaka pale watakapotangaza tarehe maalum baada ya kujiridhisha kuwa mchakato wa uandikishwaji wa daftari la kudumu bado haujakamilika.

 NA KAROLI VICENT
  Akitangaza kuhairisha zoezi hilo leo  jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakati wa Mkutano na vyombo vya Habari ambapo amesema  tume hiyo imefikia maamuzi ya kuhairisha kura ya maoni kutokana na sababu zilizojitokeza kwenye uandikishaji Mkoani njombe.
       
    Jaji Lubuva ameongeza kuwa kutangazwa kwa tarehe husika kutategemea maushauriano na tume ya uchaguzi wa taifa ya Zanzibar (ZEC).
     

TAARIFA KUHUSU TAHADHARI YA KIUSALAMA KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA 2015.


 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeweka mikakati ya mpango kazi kama ifuatavyo:-

·       Limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto na uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi, Vikosi vya uokoaji wakati wa majanga, na vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza.

·       Tumejipanga kwa ulinzi wa hali ya juu kwa kutumia askari wetu wa doria za miguu, doria za magari, kikosi cha mbwa na Farasi, kikosi cha wanamaji, Usalama barabarani, askari wa upelelezi, Helkopta ya Polisi, n.k.
·       Zitakuwepo doria za Magari, doria za pikipiki na doria za miguu katika barabara zote muhimu.


Wednesday, April 1, 2015

VIDEO-GWAJIMA JANA AKIWA KANISANI KWAKE,SIKIA ALICHOKIZNGUMZA

G16-G7Askofu Dr Gwajima baada ya kutolewa jana ostarbey alipokwenda kuhojiwa,leo majira ya saa kumi na mbili kasoro alizungumza na Kanisa lake na kueleza kile kilicho tokea hadi kupelekea yeye kukaa kwenye kiti na kushindwa kutembea.Akiongea na maelfu ya waumini walio jitokeza katika ibada ya leo Askofu Gwajima alisema haya….NANUKU
“Najua kinacho endelea namuombea mtu mmoja aliyeko hapa nasema nakufahamu vizuri nakujua vizuri na kwambia utafanikiwa kwa jina la Yesu…..huta fanikiwa kwa jina la Yesu.Usifurahi leo kuniona nimekaa kwenye kiti hiki bado nina maumivu,bado sina nguvu lakini nimesema leo lazima niende nyumbani mwa Bwana.

Wewe ni mtoto mdogo ujatoka mbali….mimi nimewahi kua sitembei kwa miaka 6,huyu aliye nifanya nitembe hawezi kukubali nikae kwenye hiki kiti tena…unatakiwa ujue”Mwisho wa Nukuu

MAGAZETI LEO ALHAMISI APRIL 2,2015.YASOME HAPA

UMESKIA ZAWADI AMBAYO SIMBA WATAMPA MCHEZAJI BORA MWAKA HUU,SOMA HAPA

Uongozi wa Klabu ya Simba umepanga kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo katika sherehe za Simba maarufu 'Simba Day' inayofanyika kila mwaka Agosti 8.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Rais wa Simba Evans Aveva alisema kuwa chini ya uongozi wake wameanzisha tuzo hizo kwa wachezaji wa Simba ili kuibua morali ya wachezaji na kuthamini mchango wao na hiyo imekuja baada ya klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi kuingia mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya EAG ambao watakuwa na jukumu la kuiwezesha Simba kupata mapato kwa njia mbali mbali ikiwemo udhamini kutoka makampuni mbali mbali.
Aveva alisema pia mbali na kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo pia kutakuwa na tuzo ya mchezaji bora anayechipukia, kiungo, mshambuliaji bora na mchezaji mwenye nidhamu.

"Mchezaji bora atapata gari, mchezaji bora chipukizi atapata Sh5 milioni waliosali watapata Sh2 milioni ikiwemo mwenye nidhamu.

WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA TIGO WATEMBELEA WATOTO WA KITUO CHA SINZA MAALUM NA KUTOA ZAWADI YA PASAKA

Meneja mkuu wa Kampuni Tigo Tanzania Cecile Tiano, akimuangalia mtoto Godfrey Alistides wa kituo cha watoto wenye ulemavu cha Sinza Maalum akichora mfano wa basi,wakati wa hafla ya wafanyakazi wa kampuni ya Tigo walipotembelea kituoni hapo kutoa zawadi ya vitu mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka
 Tigo Tanzania jana imetoa vitu vya aina mbalimbali katika shule maalumu ijulikanayo kama Sinza maalumu iliyopo jijini Dar es salaam katika kusherehekea mapumziko ya sikukuu ya pasaka. Kampuni ya Tigo pia imelipia gharama ya matumizi ya umeme ya hapo shuleni kwa mwaka mmoja.
Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael, akiongea na waandishi wa habari, wafanyakazi wa Tigo na watoto wa Kituo cha Sinza Maalum wakati wa hafla ya kutoa vitu mbalimbali kwa kituo hicho chenye watoto wenye ulemavu. Wafanyakazi wa Tigo walijitolea vitu hivyo ikiwa sehemu ya kusheherekea sikukuu ya Pasaka pamoja na watoto.
 Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo, Meneja mkuu wa Tigo Cecile Tiano alisema, vitu vilivyotolewa ambavyo ni pamoja na nguo, viatu, kinga na pedi ni ishara ya upendo na hali ya kujali kwa kampuni na wafanyakazi wa Tigo kutoa msaada kwa jamii ya watu wasiojiweza katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka.

Meneja mkuu wa Kampuni Tigo Tanzania Cecile Tiano, akiongea na waandishi wa habari, wafanyakazi wa Tigo na watoto wa Kituo cha Sinza Maalum wakati wa hafla ya kutoa vitu mbalimbali kwa kituo hicho chenye watoto wenye ulemavu. Wafanyakazi wa Tigo walijitolea vitu hivyo ikiwa sehemu ya kusheherekea sikukuu ya Pasaka pamoja na watoto. 
 "Pia tumetambua umeme wa kudumu ni moja ya hitaji muhimu sana hapa shuleni ndiyo maana Tigo imeahidi kulipa gharama zote za matumizi ya umeme ya hapa shuleni kwa mwaka mmoja kupitia Tigo Pesa," alisema Bibi Tiano. Shule maalum ya Sinza maalum inahudumia watoto 88 na vijana wenye umri wa miaka kati ya 9 na 25 ambao wanatoka katika familia zenye mazingira magumu au wanaoishi na mzazi moja au wanaishi na wazee.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Watoto wenye ulemavu ya Sinza Maalum iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam akiongea na waandishi wa habari, wafanyakazi wa Tigo na watoto wa Kituo cha Sinza Maalum wakati wa hafla ya kutoa vitu mbalimbali kwa kituo hicho chenye watoto wenye ulemavu iliyofanywa na Wafanyakazi wa Tigo. Pembeni kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa Tigo Catherine Olaka. 

Wasanii Christian Belle na Barnaba wakiwa pamoja na watoto wa Kituo cha Watoto wenye Ulemavu cha Sinza Maalum, wakati wa hafla ya kukukabidhi vitu toka kwa Wafanyakazi wa Tigo kwa kituo hicho kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka
 Meneja mkuu alifuatana na wafanyakazi wa Tigo na wasanii watano wa Bongo flava akiwemo msanii Fid Q,Menina, Christian Bella na Barnaba katika tukio ambalo lilikuwa la kusisimua na kupendeza kutokana na burudani ya moja kwa moja iliyotolewa na wanamuziki.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw.Simon Milobo alitoa shukrani zake za dhati kwa kampuni ya Tigo,” hii sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Tigo kutusaidia uwa wanakuja mara kwa mara kutusaidia tunawashukuru sana, naomba na makampuni mengine yaweze kujitokeza na kuiga mfano wa Tigo” alisema. 
Msanii Menina akiangalia vitu mbalimbali vinavyotengenezwa na watoto wa kituo cha Sinza Maalum, wakati wa hafla ya kukukabidhi vitu mbalimbali toka kwa Wafanyakazi wa Tigo kwa kituo hicho kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka. 

Mtaalam wa Mitandao ya Kijamii toka Tigo Samira Baamar akiwaonyesha jinsi ya kutumia iPad watoto wa Kituo cha Watoto wa Sinza Maalum, wakati wa hafla ya kukukabidhi vitu toka kwa Wafanyakazi wa Tigo kwa kituo hicho kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka. 

Msanii Fid Q akicheza nyimbo maalum ya kituo cha watoto wenye ulemavu cha Sinza Maalum na Mwalimu wa kituo hicho, wakati wa hafla ya kukukabidhi vitu toka kwa Wafanyakazi wa Tigo kwa kituo hicho kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka. 

Vifaa mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka kwa Kituo cha Sinza Maalum toka kwa wanyakazi wa Tigo. 

Msanii Christian Belle akionyesha watoto jinsi ya kutumia upawa wa kuchotea chakula

ACT SASA NI JINO KWA JINO,WATANGAZA KUIZUNGUKA TANZANIA,NI KUTANGAZA AZIMIO LA ARUSHA,NA HAPANA YA KATIBA MPYA.

Mwenyekiti wa ACT wazalendo mama ANNA MGHWIRA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimio ya kamati kuu ya ckama hicho iliyoketi jana 
Baada ya kufanya uchaguzi wa chama na uzinduzi wa chama kwa mafanikio makubwa chama kipya cha ACT-wazalendo nchini tanzania leo kimetangaza kuanza kuishambulia mikoa kadhaa nchini kwa lengo la kutangaza azimio la arusha baada ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho kuamua kufanya hivyo.

AkizUngumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa ACT wazalendo mama ANNA MGHWIRA amesema kuwa kamati kuu ya chama imeamua kuanza ziara ya ambayo ni ziara ya kwanza na kupita katikia mikoa takribani kumi yenye lengo la kutangaza azimio la arusha lililiuhishwa baada ya kupitishwa na vikoa vya chama ambapo amesema kwa sasa azimio hilo lipo katika hatua ya kuchapishwa.

Ziara hiyo ambayo itawahusisha viongozi wakuu wa chama itapita katika mikoa ya Ruvuma,njombe,iringa,morogoro,Dodoma ,singida,tabora,shinyanga,mwanza na mara,ziara ambayo amesema kuwa inatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa katika chaka kutokana na mapokeo ya chama hicho kuwa ni makubwa kwa watanzania.