Monday, December 23, 2013
WABUNGE WAANZISHA MKAKATI MPYA WA KUMNG'OA WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANDA PINDA KISA UTENDAJI MBOVU WA KIONGOZI HUYO KATIKA SERIKALI YA RAIS JK.
Wednesday, December 18, 2013
BREAKING NEWZZ:MV MAGOGONI YANUSURIKA AJALI
Kivuko kikubwa cha Mv Magogoni kinachofanya safari zake kati ya
Kivukoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam kimekosa muelekeo majini
katika bahari ya Hindi kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake
kushindwa kufanya kazi,Mpaka sasa sababu ya injini kushindwa kufanya
kazi hazijatoka. Shuhuda anasema ‘Tulikua wanatoka Dar kwenda Kigamboni,hatua chache kabla ya kufika Kigamboni injini zilizima,baada ya kuzima zikaja Tag kwa ajili ya kutuvuta mpaka ng’ambo ya pili ambayo ni Kigamboni,na ilituchukua dakika 45 mpaka kuvutwa ng’ambo ya Kigamboni’ Taarifa kamili zinafata endelea kufatilia kupitiaHABARI24 BLOG |
HIKI NDICHO KIINGILIO RASMI CHA MECHI YA MTANI JEMBE JUMAMOSI
JANGA LINGINE CHADEMA,WARAKA MWINGINE WA SIRI WASAMBAZWA TENA,SASA UNAMUHUSU MBOWE,WAAINISHA UFISADI WAKE MWANZO MWISHO,USOME HAPA WOTE,ALIYEUANDIKA NI HABIBU MCHANGE
Imeandikwa na
Habibu Mchange
0762178678:
Habibu Mchange
0762178678:
-------
Juzi
niliandika kuhusu unafiki wa MBOWE kuwahadaa Watanzania ya kwamba yeye
hanunuliki, nilitoa ushuhuda wa MBOWE kupokea million 100 kutoka kwa
ROSTAM AZIZ aliyekuwa mwanamkakati muhimu wa ushindi wa Urais kwa
mgombea wa CCM mwaka 2005 Mheshimiwa JAKAYA KIKWETE, ambapo pesa hizo
zilipokelewa mwezi oktoba 2005 na kumfikia mbowe kupitia kwa mke wake ndugu LILIAN MTEI MBOWE, na kumfikia MBOWE ambaye kipindi hicho alikuwa anagombea URAIS kupitia CHADEMA,
hapa mbowe sio tu kwamba alinunuliwa, alihongwa ama kutumiwa kuwadhoofisha wapinzani waliokuwa na nguvu kipindi hicho, bali pia alidhihirisha namna gani yeye ni mpinzani mtiifu kwa CCM (alikubali kutumika) na ni MNAFIKI ALIYETUKUKA.
Leo tarehe 18.12.2013, Magazeti kadhaa yameripoti juu ya muendelezo wa unafiki wa MBOWE na vibaraka wake.
Magazeti yameandika pamoja na mambo mengine, kwa ufupi kabisa hivi ifuatavyo.
ENDELEA KUUSOMA HAPA-----------
hapa mbowe sio tu kwamba alinunuliwa, alihongwa ama kutumiwa kuwadhoofisha wapinzani waliokuwa na nguvu kipindi hicho, bali pia alidhihirisha namna gani yeye ni mpinzani mtiifu kwa CCM (alikubali kutumika) na ni MNAFIKI ALIYETUKUKA.
Leo tarehe 18.12.2013, Magazeti kadhaa yameripoti juu ya muendelezo wa unafiki wa MBOWE na vibaraka wake.
Magazeti yameandika pamoja na mambo mengine, kwa ufupi kabisa hivi ifuatavyo.
ENDELEA KUUSOMA HAPA-----------
BREAKING NEWS:WATU 200 WALIOKUWA WAKISAFIRI KWA NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE WANUSURIKA KUFA BAADA YA KUTUA DHARURA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA ARUSHA
Taswira ya picha eneo la tukio
Habari
iliyoifikia hivi punde toka jijini Arusha, inaeleza kuwa Ndege ya
abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian
Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani
hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa
Arusha,hali iliyopelekea Ndege hiyo kusimama nje kabisa ya uwanja huo
huku abiria zaidi ya 200 wakiwa ndani ya ndege hiyo mpaka sasa bila ya
kushuka.
Wataalam
wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza
kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege
hiyo iweze kuruka.
Globu ya Jamii inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo,na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa itakavyokuwa ikitufikia.
PICHA NA MDAU WETU KUTOKA ARUSHA
CHANZO: BLOG YA PAPARAZI
|
Tuesday, December 17, 2013
TAARIFA MUHIMU KUTOKA TIGO,YAWATANGAZIA NEEMA WATEJA WAKE
Na Karoli Vinsent
KAMPUNI ya Simu za mkononi Nchini ya Tigo imewatangazia
Neema wateja wake baada ya kuzindua promosheni kabambe iitwayo “Cheza kwa
Furaha Unaposhinda kitita”itakayowawezesha watumiaji wa huduma ya Tigo pesa
kujishindia zawadi mbalimbali za fedha taslim zenye jumla ya shilling bilioni moja.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo,Meneja Mawasiliano wa Tigo Bw.John Wanyacha amesema
kwamba promesheni hii mpya inatokana na kampuni
hiyo kuweka kipaumbele kuwapa wateja wake sababu ya kutabasamu na fursa
ya kuweza kubadilisha maisha yao kupitia
huduma za kutuma na kupokea pesa.
“Jumla ya
shilingi milioni 150 itashindaniwa.Kutakuwa na zawadi na fedha taslim milioni10
kila mwezi kwa wateja 10 kila mmoja,fedha taslim shiling milioni mbili kila wiki
kwa wateja 20 kila mmoja na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa wateja
50 kila mmoja”alisema Wanyancha
ENDELEA HAPO CHINI--------
KUELEKEA MWISHO WA MWAKA KAMANDA MPINGA ATOA ONYO KWA MADEREVA
WANAHABARI WAKISIKILIZA KWA MAKINI |
TANZANIA NA KANADA ZASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO MUDA HUU KATIKA OFISI ZA WIZARA YA UCHUKUZI
BALOZI WA KANADA NCHINI TANZANIA ALEXENDER LEVEQUE ALKISAIN MKATABA WA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO BAINA YA NCHI YAKE NA TANZANIA MUDA HUU KATIKA OFISI ZA WIZARA YA UCHUKUZI JIJUINI DAR ES SALAAM |
TUNAKABIDHIANA--KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI TANZANIA BI MONICA MWAMUNYANGE AKIKABIDHIANA NABALOZI WA KANADA NCHINI MIKATABA WALIYOSAINI MUDA MFUPI ULIOPITA |
Monday, December 16, 2013
AZAM TV YAANZA RASMI KUHUDUMIA WATEJA WAKE LEO,TIZAMA HABARI NA PICHA
JB AU BONGE LA BWANA ALIKUWEPO |
MKURUGENZI MKUU BW RHYS TORINGTON AKISALIMIANA NA WASANII WA BONGO MUVIES KATIKA MAKAO MAKUU YA AZAM LEO ASUBUHI |
AzamTV
leo imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo barabara ya
Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Huduma
za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6,
2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi kungalia bure hadi
hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa
mwezi.
Kwa
kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu
za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo
ni:
· Azam
One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa
lugha ya Kiswahili.
· Azam
Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia
· SinemaZetu
– Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
Kwa
pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya
michezo, tamthilia, watoto na maisha.
Ofisi
ilifunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media
Ltd.
“Ofisi hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni
kielelezo cha nia thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika
shughuli ya utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango
cha juu kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika.
Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema
Bakhresa
Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema:
“Naona faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV ipo sokoni kwa ajili ya kila
mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote
nchini. Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – situ katika ofisi hizi lakini pia
kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa. AzamTV
ni ya kudumu”
Azam
Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake
tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa
Tanzania.
YUSUFU AKIWA NA BAADHI YA WASANII WA BONGO MUVIE AMBAO NAO WALIKUWA MIONGONI MWA WALIOSHUGHUDIA TUKIO HILO |
MKURUGENZI MTENDAJI WA AZAM TV BWANA YUSUFU BAKHRESA AKIKATA UTEPE KUASHIRIA KUANZA RASMI KWA HUDUMA ZA AZAM TV |
CLABU YA SIMBA HAKUKALIKI, MASHABIKI WAJIANDAA KUVAMIA KLABU YA YANGA, WATAKA KULIPA KWENDA KUMNYOFOA EMMANUELI OKWI, WADAI AMEWASALITIU
HAPA WAKIWA WANAJADILIANA BILA KUPATA MAJIBU YA UHAKIKA, HATA HIVYO MASHABIKI HAO WAMEISHIA KUPIGA DOMO HUKU MCHEZAJI HUYO AKITAMBULISHA LEO HII KATIKA KLABU YA YANGA |
HAPA WAKIFAFANUA KWA HISIA, WANACHAMA HAO WAMESEMA RAGE HAIFANYII FAIR KLABU YAO NA NDIO MAANA WACHEZAJI WOTE MUHIMU WANAONDOKA KUELEKEA KLABU PINZANI |
HUYU NDIO OKWI AKISAINI YANGA MIAKA MIWILI
exclusive---HIVI NDIVYO MABINA WA CCM MWANZA ALIVYOUWAWA NA WANANCHI JANA
Aliyekuwa
mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi
wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini
Mwanza.Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi
wananchi hao
na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama
alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wananchi
wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja
hivyo ilhali kesi ipo
Saturday, December 14, 2013
SAKATA LA KUFUNGIWA MWANAHALISI LAIBUKA BUNGENI,NAIBU WAZIRI MAKALA AMPINGA RAIS JK WAZI WAZI
Na Karoli
Vinsent
NAIBU Waziri
wa Habari na Michezo Amosi Makala amepingana hadharani Rais Jakaya kikwete kuhusu sakata la
kulifungia Gazeti la mwanahalisi.
Hayo
yaligundulika wiki hii katika vikao vya bunge vinavyoendelea mkoani Dodoma
katika kipindi cha maswali na majibu,ambapo mbunge wa Mbinga Mashariki kapteini
John Komba(CCM) alipokuwa anauliza swali kuhusu utaratibu uliotumiwa na
serikali katika kuyafungia magazeti ya mtanzania pamoja mwanahalisi.
“kwanini Serikali ilitumia nguvu katika kuyafungia
magazeti ya Mwanahalisi pamoja na Mtanzania wakati tayari serikali ilikuwa
imeshawaonya wahariri hao na hao
wahariri wa magazeti hayo wakakubali kosa na kuomba Radhi”aliuliza Komba
ENDELEA HAPO--------
EXCLUSIVE----CCM YAWAJIA JUU MAWAZIRI MIZIGO,NAPE ATOA TAMKO KALI KWA JK LEO,ATAKA WAFUKUZWE MARA MOJA,AWATAJA KWA MAJINA
PICHA NA MAKTABA |
NA KAROL VICENT ------ CHAMA cha
Mapinduzi (CCM) kimemtaka Rais Jakaya kikwete kuwatimua malamoja moja mawaziri mizigo kwa kushindwa kuwatumikia
wananchi na Kuendesha Siasa za umangi meza.
Hayo
yalisemwa na Katibu wa itikadi na
uwenezi Nape Nnauye wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, makao
makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam,Nape alisema kamati kuu ya chama cha
mapinduzi ya CCM imefikia maamuzi ya kumtaka Rais Kikwete kuwafukuza kazi
mawaziri hao kutokana na kutowatumikia wananchi na kuendesha Siasa za Umangi
meza katika wizara zao.
ENDELEA KUSOMA HAPO CHINI--------
Friday, December 13, 2013
EXCLUSIVE---WANAWAKE WAWILI WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA ZAIDI YA KETE 200 ZIKIWA TUMBONI,NI UWANJA WA NDEGE WA JK NYERERE,WALIKUWA WANAPELEKA CHINA
Thursday, December 12, 2013
AJALI MBAYA MKOANI TANGA: BASI LA BURUDANI LAPATA AJALI MBAYA LIKITOKEA KOROGWE KUELEKEA JIJINI DAR,WATU ZAIDI YA 12 WAHOFIWA KUFARIKI NA MAJERUHI ZAIDI YA 50. PICHA ZA TUKIO HIZI HAPA
Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.
Basi la Burudani leo limepata ajali kijiji cha Taula Wilaya ya Handeni, Imeripotiwa mpaka sasa watu zaidi ya 12 wamefariki na majeruhi zaidi ya 55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.
Hospitali ya wilaya ya Korogwe.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo ( kushoto) akiangalia mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu.
Manesi wakiendelea na matibabu kwa majeruhi.
Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa kwenye benchi.
Wananchi wakiwa eneo la Hospitali.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA MKUU WA WILAYA YA KOROGWE, MRISHO GAMBO.
Subscribe to:
Posts (Atom)