Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,makao makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam. HABARI KAMILI CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa furaha Chama cha Frelimo kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu. Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Frelimo, Mhe Filipe Nyusi ameibuka kidedea na sasa ndiye Rais Mteule wa Msumbiji ambaye baada ya kuapishwa atashika mikoba itaakayoachwa na Rais anayemaliza muda wake, Armando Gwebuza. |
Friday, October 31, 2014
MPYA KUTOKA CCM LEO
KUTOKA TFF LEO
Makocha 35 wameteuliwa kushiriki kozi ya ukocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) itakayofanyika mjini Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.
Kozi hiyo itaendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni na itafanyikia Mchikichini College ambapo washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ukocha vya ngazi ya Kati (Intermediate) pamoja na vyeti vya kitaaluma vya elimu ya sekondari (academic).
samahani kwa picha inayohuzunisha--AJALI MBAYA MTO WAMI MUDA HUU
HABARI ZA HIVI PUNDE... Ajali mbaya daraja la Wami basi la Simba Mtoto na Lori baada break za Lori kufeli, Dereva wa Lori amepoteza maisha hapohapo... Habari ambazo tumepenyezewa hapa kutoka daraja la wami ni kuwa lori moja moja limefel breck na kuvaana na basi la simba mtoto maeneo hayo na kusababisha kifo cha dereva wa lori hilo |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: GADNER. G. HABASH ATUA RASMI EFM
Mtangazaji mahiri Gardner.G. Habash,amejiunga na kituo cha Radio kinachokuja kwa kasi hivi sasa EFM 93.7 cha jijini Dsm ili kuongeza nguvu katika kikosi chao.
Akizungumza leo na waandishi wa habari afisa habari wa EFM Kanky Mwaigomole amesema wameamua kumchukua Gardner kwasababu ni
miongoni mwa watangazaji hodari nchini mwenye kipaji cha hali ya juu hivyo kuongeza chachu ya mafanikio katika kituo hicho kipya.
“Gardner ataendesha kipindi kiitwacho Ubaoni kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa moja kamili jioni kuanzia Jumatatu ya tarehe 03 mwezi wa 11 mwaka huu”alisema Kanky.
Gardner alimaarufu “KAPTENI” alianza kazi na kituo cha Radio Clouds fm na baadaye Times fm ambapo kwa sasa ametua Efm akitanguliwa na wakongwe kama Dj Majey,Dizzo One,Sos B,Denis Ssebo,Maulidi Kitenge,Omari Katanga,Scholastica Mazula na Kanky Mwaigomole
MSIBA--HUYU NDIYE MTANGAZAJI MAARUFU ALIYEFARIKI LEO TANZANIA
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam(RTD) ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo au maarufu Ben Kiko (pichani) amefariki duania.
Mwandishi huyo mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Ben Kiko alihamishiwa katika hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.
VIONGOZI WA MSONDO WAMTEMBELEA RAIS KIKWETE IKULU
Tuesday, October 28, 2014
AMKA NA PICHA HII--SIASA HAIKOSI VITUKO
HIVI NDIVYO MSANII CHID BENZ ALIVYOPANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KUDAKWA NA UNGA
Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande) |
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi Abdallah Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae. |
HUYU NDIYE MCHEZAJI BORA WA MWEZI HUU LIGI KUU TANZANIA BARA
Kiungo wa timu ya Azam, Salum Abubakar amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Abubakar ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) aliwashinda wachezaji wengine 20, huku wanne kati ya hao wakichuana naye kwa karibu.
Wachezaji hao ni Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Najim Magulu wa JKT Ruvu Stars.
Kwa kuibuka mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.
Monday, October 27, 2014
SERIKALI IPO NJE YA NCHI,RAIS KIKWETE VIETNAM MH PINDA OMAN ZIARANI
TAMASHA KUBWA LA TIGO WELCOME PACK LAFANA JIJINI ARUSHA.PICHA ZIKO HAPA
Mmoja kati ya watu waliojitokeza kwenye tamasha la welcome pack akipokea zawadi toka kwa mfanyakazi wa Tigo.
|
HABARI KUBWA JIJINI--ACT WAWAUNGA MKONO UKAWA,WAMWAGA PONGEZI KWA MUUNGANO WAO,NAO KUZUNGUKA NCHI NZIMA KUHAMASISHA KURA YA HAPANA KWA KATIBA
Katibu mkuu wa chama cha ACT TANZANIA--SAMSON MWIGAMBA akizungumza na waandishi wa habari ofisi za chama hicho kijitonyama jijini dar es salaam muda huu kuhusu mambo mbalimbali katika chama hicho |
Ikiwa imepita siku moja tangu umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA kusaini makubaliano ya kuunganisha vyama vyao kwa lengo la kuwa
na nguvu zaidi ya kisiasa katika chaguzi zijazo nacho chama kipya katika siasa
za Tanzania cha ACT-TANZANIA kimeibuka
na kupongeza hatua hiyo na kuunga mkono harakati hizo za kisiasa za kuunganisha
nguvu ya upinzani kwa kusema kuwa kufanya hivyo itawasaidia kukiangusha chama
cha mapinduzi kirahisi huku akitoa tahadhari kwa muungano huo.
Akizungumza na wanahabari muda huu katika ofisi za
chama hicho kuhusu maadhimio ya mkutano wa kamati kuu ya chama hicho katibu
mkuu wa ACT Samson mwigamba pamoja na kutokuweka wazi kuwa chama chake kipo
tayari kujiunga na UKAWA amesema kuwa ni hatua nzuri kwa siasa za upinzani kama
muungano huo utakuwa ni muungano wa sera na kutetea wananchi huku akisema chama
chake kitaungana na chama ambacho kipo tayari kuwatetea wanachi na sio kwa
ajili ya kuiangusha CCM ili wagawane madaraka ya serikali.
“Muungano wa ukawa ni hatua nzuri katika siasa ila tunatoa tahadhari sana kwa muungano huo
usije ukawa ni muungano wa kugawana madaraka, sisi tutaungana na yeyote ambaye
yupo tayari kuwatetea wananchi ila hatutaungana na watu ambao watakuwa wanataka
kuiangusha CCM ili kuingia ikulu na kugawana madaraka”Amesema MWIGAMBA.
Aidha akizungumzia katiba iliyopendekezwa katibu mkuu
huyo amesisitiza kile ambacho na UKAWA walisisitiza kwa kusema kuwa katiba
iliyopendelezwa ni wizi na udanganyifu mkubwa kwa wananchi ambao umefanywa na
chama cha mapinduzi hivyo nao wanatangaza rasmi kuzunguka nchi nzima
kuwahamasisha wananchi wote kupiga kura ya hapana kwa katiba iliyopendekezwa
kwa kile walichodai kuwa haijakidhi mahitaji nya watanzania kwa sasa.
“Chama cha ACT kwa nia moja tumeamua kuzunguka kwa
watanzania wote kuhamasisha kura ya hapana kwa watanzania na zoezi hilo litaanza
mara moja kwa kuwa katiba hii iliyopendekezwa haijakidhi matarajio na maoni ya watanzania wote.
Akikizungumzia cha hicho kipya amesema kuwa ACT
kitazinduliwa rasmi tarehe 5 december mwaka huu jijini Dare s salaam ambapo kwa
mujibu wa katiba ya chama hicho kutafwatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara wa
uzinduzi wa chama hicho ambao utafanyika jijini mwanza.
SOMA TAMKO LAO LOTE HAPA----
Sunday, October 26, 2014
CCM NAO WALIUNGURUMA HUKO ZANZIBAR KIBANDAMAITI JANA,PICHA ZIKO HAPA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyeekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakifuatana katika mkutano hadhara uliofanyika leo katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja,[Picha na IkuRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi na Wanachama wa CCM katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja leo.[Picha na Ikulu.]
Wananchi na WanaCCM waliofirika katika viwanja vyaDemokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja wakiwa katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo ambao umeweka bayana na kufanya uchambuzi baadhi ya vifungu vya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.[Picha na Ikulu.]Wananchi na WanaCCM waliofirika katika viwanja vyaDemokrasia Kibanda maiti Mjini Unguja wakiwa katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein leo ambao umeweka bayana na kufanya uchambuzi baadhi ya vifungu vya katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.[Picha na Ikulu.]
YAMETIMIA UKAWA--HII NI HISTORIA YA SIASA ZA TANZANIA,CHEKI PICHA ZA KUSAIN MAKUBALIANO HAPA
Wenyaviti wa vyama hivyo kwa pamoja wakisaini makubaliano hayo ambayo yanawaweka pamoja na kufanya siasa ya Tanzania kuingia katika historia nyingine kubwa na ambayo haijawahi kutokea |
Mamia ya wanachama waliojitokeza hapa |
Naibu katibu mkuu zanzibar chaderma salum mwalim akizungumza lugha ya tatu. PICHA NYINGINE ZA TUKIO HILI ZIKO CHINI HAPO |
PICHA 14 ZA AWALI HISTORIA WANAYOWEKA UKAWA LEO VIWANJA VYA JANGWANI ZIKO HAPA
Saturday, October 25, 2014
KUTOKA UKAWA LEO
Subscribe to:
Posts (Atom)