Mshindi wa kwanza upande wa wanaume wa mbio za kilometa 21,Tigo Kili Half marathon, Emmanuel Giniki kutoka Tanzania akimaliza mbio hizo, mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Kilimanjaro.
|
Tuesday, February 28, 2017
MASHINDANO YA TIGO KILI HALF MARATHON YANOGA MJINI MOSHI
RUVU SHOOTING V YOUNG AFRICANS KESHO LIGI KUU YA VODACOM
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano ambako mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali ya mchezo huo mmoja kwa siku ya Jumatano, ligi hiyo ambayo ni michuano mikubwa nchini, itaendelea mwishoni mwa wiki hii ambako kwa siku ya Jumamosi Machi 4, mwaka huu Simba itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
WAZIRI NAPE AWATANGAZA ALIKIBA NA DIAMOND KWEMO KATIKA KAMATI YA HAMASA SERENGETI BOYS
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb), ametangaza Kamati ya watu 10 watakaohamasisha kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia timu ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys.
Mheshimiwa Nape alitangaza kamati hiyo itakayoongozwa na Mtangazaji mkongwe wa habari na Mpira wa miguu nchini, Charles Hilary mbele ya wanafamilia ya mpira wa miguu waliohudhuria kongamano ya kujadili juu ya ushiriki wa Tanzania katika michuano ya kimataifa.
MEYA ILALA AFUNGUA RASMI DARAJA LA BONYOKWA-KINYEREZI
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akihutubia wananchi baada ya kufungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonesti (Chadema) akihutubia wakati wa ufunguzi wa daraja hilo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akikiwa amekata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
BOHARI YA DAWA (MSD) YAPIGA HATUA KUWEZESHA UZALISHAJI DAWA KWA NJIA YA UBIA NA SEKTA BINAFSI (PPP)
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana, Laurean Bwanakunu (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba 400,000 Dar es Salaam leo, ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani.
Muonekano wa chumba cha mkutano wakati wa hafla hiyo ya kutiliana saini. Pichani ni maofisa kutoka Halmshauri ya Kibaha na MSD.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka, akizungumza wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa MSD kuzungumza katika hafla hiyo.
Mkutano ukiendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu, akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Kibaha, Bi Jenifa Omolo.Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Kibaha, Bi Jenifa Omolo (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo (wa pili kulia), wakisaini makubaliano ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba 400,000 Dar es Salaam leo, ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani. Kulia ni Mwanasheria wa Mji wa Kibaha, Mansuetha Mbena na kushoto ni Mwanasheria wa MSD, Christopher Kamugisha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Leonard Mlowe (kulia), akisaini hati hizo za makubaliano.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo wakionesha hati baada ya kusaini makubaliano hayo.
Picha ya pamoja.
Monday, February 27, 2017
Breasking Newz--LEMA MGUU NJE MGUU NDANI,MAHAKAMA IMEAMUA HAYA LEO
Sunday, February 26, 2017
RAIS MAGUFULI AMTEUA NUNDU KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TTCL,AMWAPISHA ANDENGENYE KUWA KAMISHNA JENERALI JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Bw. Omary Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Omary Rashid Nundu umeanza tarehe 24 Februari, 2017.
Bw. Omary Rashid Nundu anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Prof. Tolly Salvatory Augustine Mbwete.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Thobias Emir Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali Thobias Emir Andengenye anachukua nafasi ya Kamishna Jenerali Pius M. Nyambacha ambaye amestaafu.
Pia, Mhe. Rais Magufuli amewaapisha Mabalozi wanne walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kama ifuatavyo;
Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Nairobi, Kenya ambako anachukua nafasi ya Mhe. John Haule ambaye amestaafu.
Mhe. Silima Kombo Haji ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Khartoum, Sudan ambako anakwenda kufungua Ubalozi.
Mhe. Abdallah Abas Kilima ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Muscat, Oman ambako anachukua nafasi ya Mhe. Ali Ahamed Saleh ambaye amestaafu.
Mhe. Matilda Swila Masuka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Seoul, Korea Kusini ambako anakwenda kufungua Ubalozi mpya
Aidha Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mabalozi wote wanne wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa ummakilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
MBUNGE APATA AJALI AKIWA KWENYE ZIARA NA NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA MKOANI MANYARA
Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.
MANENO YA KISHUJAA YA RIDHIWAN BAADA YA KUKUTANA NA LOWASA
Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwan Kikwete, amesema siasa ni shule ambayo haina mwisho na ndiyo maana anaendelea kujifunza mengi kutoka kwa wanasiasa wenzake hususani waliomtangulia bila kujali chama.
Kikwete alitoa ujumbe huo jana mara baada ya kukutana na kuteta na aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2015, Edward Lowassa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga.
Kikwete ambaye ni mwanachama na kiongozi ndani ya klabu ya Yanga, alimfuata Lowassa alipokuwa amekaa na kufanya naye mazungumzo ambayo hajayaweka wazi, na kisha kurudi sehemu yake huku akishuhudia timu yake ya Yanga ikilala mabao 2-1.
SPIKA MSTAAFU WA ZANZIBAR, PANDU KIFICHO AONGOZA MAHAFALI YA NNE YA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO (UB), KAWE JIJINI DAR ES SALAAM
Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, akimtunuku Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), Fadhil Innocent baada ya kuhitimu katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu. Kificho alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho (katikati), akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Jaji mstaafu Steven Bwana baada ya kuwasili kwenye mahafali hayo.
Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), katika chuo hicho, Fadhil Innocent (wa kwanza kushoto), akiwa na wahitimu wa wengine katika mahafali hayo.Saturday, February 25, 2017
TIGO YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA KITUO CHA AMANI MKOANI KILIMANJARO
TIZAMA MBOWE,LOWASA RIDHIWAN NA WEMA NA NAPE WALIVYOKUTANA TAIFA LEO YANGA IKILALA GOLI MBILI
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Siasa leo walikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia mpambano kati ya watani wa jadi Simba na Yanga katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ambapo mnyama Simba ameibuka kidedea kwa kuibamiza Yanga goli 2-1 licha ya kuwa pungufu kwa muda mrefu.
Viongozi hao ni pamoja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Jamal Malinzi na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
KIPYENGA CHA UCHAGUZI DRFA CHAPULIZWA,MCHAKATO KUANZA RASMI KESHO
Kamati ya uchaguzi ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,imetangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa kuwapata viongozi wa chama hicho watakaokiongoza kwa kipindi kingine cha uongozi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Yusuph Kaiwanga,amesema mchakato huo wa uchaguzi ulipangwa kuanza tangu jana tarehe 24 mwezi februari lakini kutokana na pilika pilika za mchezo wa Simba na Yanga wameamua kusogeza mbele kwa siku moja hadi kesho tarehe 25 mwezi februari.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ni kwamba maandalizi yote kuelekea uchaguzi huyo yamekamilika na ndiyo maana wameamua kupuliza kipyenga na kuwataka wale wote wenye sifa zinazohitajika kujitokeza kuchukua fomu.
Ratiba nzima ya zoezi hilo itabandikwa katika ubao wa ofisi za DRFA,na fomu zitaanza kuchukuliwa kesho hadi tarehe 03 mwezi machi ambapo zoezi la kupitia majina ya walioomba.
Imetolewa na kitengo cha habari na wasiliano DRFA.
TECNO L9+ MKOMBOZI WA WATANZANIA.
Kampuni ya simu yenye asili ya China, Tecno Mobile
imekuja na ufumbuzi wa tatzo la simu janja (smart phone) kutokaa na chaji kwa
muda mrefu.
Tecno wanajulikana kwa kua na simu zinazokaa na
chaji kwa muda mrefu lakini zikiwa na ubora mkubwa, inatazamiwa hivi karibuni
Tecno wataingiza sokoni simu itakayokua
mkombozi wa watanzania, simu hii inatoka
kwenye mfululizo wa matoleo ya L, ikitanguliwa na L8/l8 plus hii inakuja ni L9
plus .
Tecno L9 plus inatarajiwa na kua betri lenye uwezo mkubwa
Zaidi simu zilizoko sokoni za aina yake,
ikiwa ni 5000 mAh, kwa ukubwa wa betri hili pamoja na matumizi makubwa
kusikiliza au kuangalia video, kupiga picha na kutumia mitandao ya kijamii simu hii inaweza kufika masaa 72 ambayo ni sawa
siku tatu ndipo mtumiaji anaweza kuchaji tena.
Pia Tecno L9 plus pamoja na kua betri kubwa inakuja ikiwa na
uwezo mkubwa kuchaji haraka, mtumiaji akichaji kwa muda wa dakika tano anaweza
kuitumia simu kwa kupiga picha Zaidi ya 1000.
Kwa watanzania walioko mikoani simu hii inawafaa
Zaidi hasa ukizingatia matatizo ya umeme kukatika katika kwa muda usio julikana,
pia kupunguza kadhia ya kutembea na
vibeba umeme, power bank.
Tecno L9 plus inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni pia
ina usalama wa alama ya vidole maarufu kama finger print hali kadhalika wemba
wemba mzuri utakao mpa mtumiaji urahisi wa kuitumia.
Inatabiriwa kufanya vizur sokoni na wataalamu wa vifaa
vya mawasiliano, Tecno L9 plus inasubiriwa kwa hamu na watanzania wengi.
Friday, February 24, 2017
TIZAMA MSANII WEMA SEPETU ALIVYOPOKELEWA RASMI CHADEMA LEO
Msanii wa filamu nchi Tanzania Wema Sepetu ametangaza rasmi kukihama Chama cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)a
Akizungumza na waandishi wa habari leo akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania.
Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.
"Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana". Amesema Wema Sepetu
Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.
"Sijachukua pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike" - Amesema Wema
Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" -Wema Sepetu
Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia amerudisha kadi ya CCM na kusema"Tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo CCM haikumtendea haki
Kuhusu sauti zilizosambazwa mitandani zikionesha Mama Wema akiongea na Steve Nyerere, mama Wema amesema "Kuhusu sauti zinazosemwa kuwa ni mimi na Steve Nyerere, siwezi kulizungumzia hilo maana sijazisikia"
==>Msikilize hapo chini akiongea
KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AENDESHA KIKAO CHA IDARA ZA WIZARA HIYO JIJINI DAR ES SALAAM
KAMPUNI YA RESOLUTION INSURANCE IMEWADHAMINI KAWE JOGGING CLUB KUSHIRIKI MASHINDANO YA KILI MARATHON 2017
Katibu
Mkuu wa Kawe Jogging Club, Al Haj Seif Muhere (wa kwanza kushoto) akitoa
shukrani kwa Kampuni ya Resolution Insurance kwa niaba ya klabu yake.
|
MAFUNZO YA UKAKAMAVU KIDATO CHA KWANZA JITEGEMEE JKT SEKONDARY YAFUNGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM
Mgeni rasmi wa kufunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Jitegemee Sekondari Mgulani JKT, Meja Haule (katikati), akiwa na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Ofisa Tawala wa Kombania wa shule hiyo, Kepteni Zaujia Shemahonga, Msanifu wa Shule, Meja Rehema Wanjara, , Makamu Mkuu wa Shule Utawala, Kepteni Benitho Lubila na Makamu Mkuu wa Shule Taaluma, Ema Mosha.
Thursday, February 23, 2017
TAARIFA ZA WEMA KUJIUNGA CHADEMA ZIMEDHIBITISHWA AU BADO?--KAULI YA MBOWE HII HAPA
Hii ilikuwa taarifa ya chama mchana kuhusu kumpokea wema
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kunatarajia kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo na chama hicho akiwemo msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu (28).
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa chama hicho kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo Wema Sepetu.
Wema pamoja mama yake, leo aliongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.
AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUENDELEA KESHO
Baada ya Simba kutangulia robo fainali ya Kombe la Shirikisho la
Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup kwa kuifunga African Lyon kwa bao
1-0, mechi nyingine za kuwania nafasi hiyo zitaanza kuchezwa kesho Ijumaa
Februari 24, mwaka huu.
Simba iliilaza African Lyon katika mchezo wa hatua ya 16 bora
uliofanyika Februari 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
LIGI KUU YA WANAWAKE SASA KUANZA FEBRUARI 26
Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) hatua ya 6 Bora itaanza
rasmi Februari 26, 2017 kwenye kituo kimoja cha Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Ilala, Dar es Salaam.
Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens
ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi
“A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na
Panama ya Iringa.
RAIS MALINZI AELEZA MIKAKATI, NAPE AIPONGEZA TFF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi ameelezea mikakati mbalimbali ya maendeleo
ya soka nchini akisema hiyo ndiyo sababu ya Kamati ya Utendaji kubuni na kuunda
Mfuko wa Maendeleo ya soka.
Katika Risala yake aliyoitoa jana
mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye
katika uzinduzi wa mfuko huo, Rais Malinzi alisema wamefanya hivyo kwa lengo la
kutimiza ndoto za Tanzania kushiriki michuano mbalimbali ya soka.
“Kwa kipindi kirefu Tanzania hatujafanikiwa
kucheza fainali kubwa za mpira Barani Afrika. Mara ya mwisho kupata mafanikio
makubwa kwa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ilikuwa ni mwaka 1980 Tanzania
ilipofuzu kucheza fainali za Afrika (AFCON) nchini Nigeria,” amesema Rais
Malinzi na kuongeza:
Wednesday, February 22, 2017
MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM MWITA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KUPITISHA BAJETI YA MWAKA 2016/17 AMBAYO NI SH.BILIONI 13.18
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza na wajumbe wa baraza la madiwani wa jiji hilo katika Ukumbi wa Karimjee leo,wakati wa kupitisha makisio ya bajeti ya matumizi ya ndani ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016-17 yenye jumla ya Sh.Bilioni13.177 ambayo ni sawa na asilimia 72%. Kulia ni Mkurugenzi wa Jiji hilo,Sipora Liana na Naibu Meya wa Jiji,Mussa Kafana. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam,Sipora Liana,akitoa taarifa ya makisio ya bajeti ya matumizi ya ndani ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2016-17 yenye jumla ya Sh.Bilioni13.177 ambayo ni sawa na asilimia 72%. Kushoto kwake ni Meya wa Jiji hilo,Isaya Mwita na Naibu Meya,Mussa Kafana.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akizungumza katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji hilo.
MALINZI AZIPONGEZA SINGIDA UNITED, NJOMBE MJI
Mara baada ya wiki iliyopita Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kuipongeza timu ya Lipuli ya Iringa, leo Jumanne Februari 21,
mwaka huu kwa mara nyingine, Rais wa TFF Jamal Malinzi amezipongeza kwa mpigo,
timu za Singida United ya Singida na Njombe Mji ya Njombe kwa kupanda daraja.
Subscribe to:
Posts (Atom)